Amini usiamini upo mgawanyiko mkubwa ndani ya JWTZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amini usiamini upo mgawanyiko mkubwa ndani ya JWTZ

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 7, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Kauli ya mnadhimu mkuu wa JWTZ inayoashiria jeshi hilo kukiuka katiba ili kulinda ajira ya JK na CCM kwa visingizio vya kulinda amani kazi ambayo ni ya polisi wa kawaida imeongeza mgawanyiko uliokuwepo ndani ya jeshi hilo. Mgawanyiko huo ni wa kimapato.

  Wakubwa wachache ambao JK na CCM yake wamewalinda kwa ulaji kemukemu kutokana na ufisadi unaoendelea nchi nzima wanafurahia hilo agizo kwa asilimia mia. Lakini wengi wa makamanda hao ambao ni hoehae kwa kuathirika na ufisadi huo wamechukizwa na kauli ya bosi wao na wapo ambao watakuwa wagumu kutii amri inayokiuka katiba ya nchi hii.

  Hoehae hao, ndiyo vibosile ndani ya jeshi hilo wanawategemea wafuate amri hizo batili. Mazingira haya yanaashiria migawanyiko ya kimapato haipo uraiani tu bali huko jeshini hali ni hiyo hiyo tu
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kauli ya akina Shimbo yatua kwa Mabalozi

  [​IMG] Chadema yawasilisha malalamiko [​IMG]
  [​IMG] Mashirika ya kimataifa pia yaelezwa
  [​IMG] FemAct nao watoa kauli, walaani


  Kauli iliyotolewa na vyombo vya usalama Ijumaa iliyopita na kusomwa hadharani na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, juu ya Uchaguzi Mkuu imezua mambo mapya na sasa Chama cha Demokrsia na Maendeleo kimelalamika rasmi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa kuna njama za kuvuruga uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
  Waraka wa Chadema wenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/SG/02/79 uliochapishwa Oktoba 4, mwaka huu na umesainiwa na Mwenyekiti wa Kampeni za urais za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na kupelekwa kwa kiongozi wa mabalozi walioko nchini.
  Pia umenakiliwa kwa ofisi zote za kibalozi zilizopo nchini, mashirika ya kimataifa yaliyo nchini, wagombea urais wote na vyombo vya habari.
  Waraka huo unasema kuwa Chadema wameguswa na kauli ya Luteni Jenerali Shimbo alipowatahadharisha Watanzania kwamba majeshi na vyombo vya usalama wamejiandaa kuzikabili vurugu zozote zitakazotokea wakati wa uchaguzi huo.
  "Pasipo kutoa uthibitisho, Luteni Jenerali Shimbo alieleza hisia kwamba vyombo vya usalama vimepokea taarifa za kiintelijensia zikionyesha kuwepo vyama vya siasa vinavyojiandaa kwa ajili ya vurugu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu nchini," alisema.
  Profesa Baregu ameelezea katika waraka huo kuwa ni kitendawili kwa Luteni Jenerali Shimbo kuvitaka vyama vya siasa na wagombea wao kuyakubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
  "Pamoja na kutambua haja ya majeshi ya ulinzi kuhakikisha utawala wa sheria na taratibu vinafuatwa, hasa wakati huu wa uchaguzi, tunaamini kwamba tamko hilo kwa kipindi hiki cha kampeni za kisiasa, limetolewa kwa pupa na bila vielelezo vyovyote thabiti," alisema.
  Alisema Chadema inaliona tamko hilo ni kuingilia dhahiri mchakato wa uchaguzi na kupanga matokeo yake.
  Alisema inapaswa kueleweka kwamba tamko la JWTZ ni kinyume cha Katiba na kwa makusudi limevuka mamlaka ya kikatiba kwa kuingilia shughuli za Jeshi la Polisi.
  Pia, Profesa Baregu anasema hakuna msingi wa kutoa tamko hilo zito katikati ya kampeni, wakati hakuna uthibitisho wa tukio kubwa linalohatarisha amani na utulivu nchini.
  "Nchi hii inatawaliwa kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria nyingine zilizopitishwa na Bunge. "Kama kuna watu wanaobainika kujihusisha na vurugu na kuhatarisha amani, jambo ambalo ni kosa la jinai hapa nchini, ni lazima washitakiwe," alisema.
  Alisema Chadema haioni mantiki ya vyombo vya usalama kulalamika hadharani badala ya kuchukua hatua za kisheria kudhibiti uvunjifu wa amani na utulivu.
  "Kama vyombo vya usalama vina taarifa sahihi ama za kiintelijensia, kwamba zimebaini kuwepo shughuli za jinai, vinapaswa kuchukua hatua mapema kuliko kutoa tamko la kisiasa," alisema.
  Profesa Baregu alisema Chadema hakiamini kwamba tamko hilo lilitokana na taarifa zilizokusanywa kutoka katika vyanzo vya kiintelijensia.
  Badala yake alisema lina shinikizo la kisiasa linalokusudia kuwatisha wapiga kura na kutoa ubashiri kwamba matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao hayatatokana na kura za wananchi bali kwa hila za vyombo vya dola yakiwemo majeshi.
  "Tunaamini kwamba mchakato wa kisiasa lazima uachwe bila kuingiliwa na majeshi kama hakuna sababu za msingi kufanya hivyo," alisema. Profesa Baregu alisema ijulikane kwamba tamko la JWTZ lilitolewa wakati kukiwa na mfululizo wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010, uliofanywa na mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
  Alisema Rais Kikwete amekuwa akitumia rasilimali za umma katika kampeni zake na katika matukio tofauti alizidisha muda wa kampeni unaotambulika kisheria.
  Kwa mujibu wa Profesa Baregu, polisi na vyombo vingine vya usalama vina taarifa kwamba CCM imekuwa ikitoa mafunzo kwa kikundi cha Green Guards ambacho kinahusika kufanya vurugu kwenye mikutano ya kampeni ya Chadema.
  Profesa Baregu alitaja baadhi ya maeneo yanayosadikiwa kuwa Green Guards wa CCM walifanya vurugu dhidi ya Chadema kuwa ni katika majimbo ya Busanda, Moshi Mjini na Ubungo. "Hakuna hatua zilizochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi licha ya malalamiko yetu kadhaa," alisema.
  Pia Profesa Baregu alisema hivi karibuni gazeti la serikali la Daily News, lilitangaza matokeo ya mshindi wa urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.
  Alisema kutokana na hali hiyo, Chadema imetuma waraka kwa jumuiya ya kimataifa ambapo nakala zake zimesambazwa kwa balozi za nje na mashirika ya wahisani, ili wataimbue hali hiyo. Profesa Baregu alisema Chadema inaamini kuwa Nec itatimiza wajibu wake kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa huru na haki na kwamba uamuzi wa wananchi unaheshimiwa.
  Ijumaa iliyopita Shimbo akiwa amefuatana viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi aliwaambia waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi hilo kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu na kuvitaka vyama vya siasa na wagombea kuyakubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
  Katika tamko hilo lililoelezwa ni la pamoja kati ya JWTZ na Polisi, limezuia mjadala kwa kada tofauti nchini, huku watu wengi wakimkosoa kwa mitazamo tofauti.
  FemAct nao yalaani
  Katika hatua nyingine, umoja wa mashirika 50 ya kiraia nchini (FemAct) umelaani tamko lilitolewa hivi karibuni vyombo vya ulinzi na usalama kuwa vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kukataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu.
  Mashirika hayo yamesema kauli hiyo ina ajenda ya siri iliyojificha nyuma yake na linalenga kuvuruga uchaguzi ujao.
  Kadhalika, mashirika hayo yamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vikiongozwa na JWZT, kukataa kutumiwa na wanasiasa kuupotosha umma.
  Wanaharakati hao walisema JWTZ halina uwezo wa kumuweka madarakani mtu yeyote isipokuwa wananchi ndiyo wenye uwezo huo kupitia uchaguzi.
  Tamko hilo lilisomwa jana jijini Dar es Salaam na, Buberwa Kaiza ambapo alisema Luteni Jenerali Shimbo anajua si wanajeshi wala silaha zinazoweza kulazimisha wananchi au vyama vya siasa kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao.
  Mashitika hayo yaliweka bayana kuwa hayapo tayari kuona Tanzania inapitishwa katika machafuko ya kupandikizwa kwa lengo la kukifurahisha kikundi ama mgombea wa chama chochote cha siasa.
  Kaiza alivitaka vyombo hivyo kuacha kuingilia mchakato wa uchaguzi huo na kwamba hapakuwa na sababu yoyote ya kutolewa tamko hilo.
  Mwanachama mwingine wa FemAct, Ananilea Nkya akichangia kwenye tamko lao alisema, JWTZ haina mamlaka ya kupindua mamlaka ya wananchi.
  Alisema mamlaka ya kumuweka kiongozi madarani yapo kwa wananchi kupitia uchaguzi mkuu na sio vinginevyo na kulaani chama kinachojitangazia kwamba kitashinda kwa asilimia 80 wakati uchaguzi mkuu haujafanyika.
  Alilisifu Jeshi la Polisi kwa jinsi lilivyojipanga mwaka huu ili kuhakikisha linasimamia uchaguzi unafanyika kwa uhuru na amani.
  CHANZO: NIPASHE
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Inabidi Barua hiyo ipelekwe hadi kwa Obama ili aone alikuwa akisifia mtu wa aina gani.

  Ndiyo maana hadi leo hajaja Tanzania ingawa tuna kiherehere sana tu kwake.
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wapi na wapi JESHI- JWTZ na usalama wa raia?

  Huu ni ubabe tu!!!
   
 5. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280

  FEMINIST ACTIVIST COALITION
  (FemAct)


  C/O TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME, MABIBO ROAD,
  P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286 Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244, Email info@tgnp.org, web TGNP

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VISIINGILIE UCHAGUZI MKUU; KUVURUGA AMANI

  1. Oktoba 1, 2010, Vyombo vya Ulinzi na Usalama; Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Makao Makuu ya Jeshi ka Polisi vilitoa tamko, kupitia Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, juu ya ulinzi na usalama kuhusu amani wakati wa kampeni na uchaguzi. Kesho yake, yaani Oktoba 2, vyombo vya habari nchini vilikariri tamko hilo, na hivyo kusambaza ujumbe na maudhui yake kwa wananchi na umma kwa ujumla, kama ilivyokusudiwa.

  1. Katika ujumla wake, Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama linasisitiza umuhimu wa wadau wa uchaguzi kulinda amani na usalama, ambazo ni tunu za Taifa la Tanzania, hususan katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010. Tamko linawakumbusha wadau wa uchaguzi; wananchi, asasi za kiraia, mashirika ya dini na vyama vya siasa, umuhimu wa kutunza na kuenzi amani sawia na kushirikiana na vyombo vya usalama kulinda amani. Aidha wadau wanakumbushwa wajibu wa majeshi; JWTZ na polisi kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuwa katika hali ya amani na usalama. Hili ni jambo jema kwa faida na ustawi wa taifa letu ambalo wengi wa wananchi wake bado ni maskini sana.

  1. Hata hivyo, licha ya Tamko kuwakumbusha Watanzania umuhimu wa kuenzi na kulinda amani na usalama wa taifa lao, sisi mashirika yanayotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu na Maendeleo na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct) tumeshitushwa, hatukubaliani na tunalaani kwa jinsi na namna (mtindo) tamko la vyombo vya ulinzi na usalama lilivyotolewa, uhalali wa wahusika kutoa tamko hilo, kipindi lilipotolewa tamko hilo, mantiki yake, mwelekeo wa maudhui yake na chombo kilichotoa tamko husika kwa sababu zifuatazo:

  i). Tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama linakiuka, na ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977. Ibara 138 haibainishi kuwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama yatajihusisha moja kwa moja na masuala ya Uchaguzi wala kubainisha kuwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani Rais wa Jamhuri, anaweza kutoa amri kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama kuingilia shughuli za Uchaguzi Mkuu, au chaguzi nyinginezo. Aidha ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977, haitaji wala kutambua Majeshi ya Ulinzi na Usalama kama sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kitendo cha Majeshi ya Ulinzi na Usalama kutoa tamko kupitia vyombo vya habari ni dhahiri kinalenga kutoa vitisho, kuchochea, kuingilia mchakato, na bila shaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu unaokusudiwa kufanyika Oktoba 31. Na kama hivyo ndivyo, WanaFemAct tunalazimika kuamini kuwa tamko la vyombo vya Ulinzi na Usalama limeficha na kusheheneza malengo ya maslahi binafsi, siyo maslahi ya nchi kama umma unavyoaminishwa.

  ii). Hadi sasa, zaidi ya 'vijembe' vya hapa na pale baina ya wanasiasa na vyama vya siasa vinavyoshindana na kujinadi kwa wananchi ili kupata ridhaa ya kuongoza dola ya Tanzania, hakuna wala hakujatokea tishio lolote la kuvurugika kwa amani. Vyama vya Siasa vimekuwa vikiendelea kutangaza mipango ya sera zao, vijijini na mijini, kupitia mikutano ya kampeni; wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuhudhuria mikutano ya kampeni, kusikiliza na kuchambua ahadi mbalimbali zinazotolewa na wanasiasa na vyama vyao; vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti taarifa mbalimbali kuhusiana na mambo yanayojiri kwenye mikutano ya kampeni, na hata kampeni za nyumba kwa nyumba; asasi za kiraia, kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, zimekuwa zikiendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa makundi mabalimbali ya wapiga kura watarajiwa; Msajili wa Vyama Vya siasa amekuwa akiendelea kufuatilia utekelezaji wa Maadili ya Vyama vya Siasa Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi; na Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiendelea kuratibu kampeni, kusimamia manunuzi ya vifaa tayari kwa kusambazwa katika vituo 52 000 vya kupigia kura nchini kote, kuthibitisha usahihi wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na kuratibu wadau wengine wa uchaguzi, kwa mfano, waangalizi wa ndani na nje wa uchaguzi. Hayo yote yakiwa yanaendelea hakujatokea tishio la kuvurugwa kwa amani wala tatizo la kiusalama. Kama hivi ndivyo, wanaFemAct tunaendelea kuamini kuwa tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama lina agenda yake; ya siri. Si bure! Litakuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana iwapo Watanzania watabaini kuwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama vimeanza kutumiwa vibaya na wanasiasa na vyama vya siasa kwa manufaa ya kikundi maslahi binafsi cha vatu wachache.

  iii). Jeshi la Wananchi wa Tanzania halipaswi kujihusisha na masuala ya ndani ya usalama wa raia. Kama kweli kungekuwa na tishio la amani na usalama, basi tungetegemea kuona Jeshi la Polisi, chombo chenye dhamana ya kuhakikisha kunakuwa na hali ya usalama kwa raia na mali zao, likitoa tamko hilo; siyo JWTZ. Sasa kama hivyo ndivyo, wanaFemAct tunasikitika na kushangaa kuona Jeshi la Wananchi wa Tanzania likifanya kazi za polisi wakati askari wa Jeshi la Polisi wapo tele, pamoja na Inspekta Jenerali wao. Hali hii haieleweki na ni kinyume cha kanuni za msingi za utawala bora. Inakuwaje askari polisi waendelee kulipwa mshahara wakati kazi zao zinafanywa na wanajeshi wa JWTZ!

  iv). Ujumbe unaotolewa na tamko la Vyombo vya Usalama kuwa "vimejiandaa kikamilifu kupambana na mtu, watu, kikundi, chama au taasisi yoyote... itakayochochea kuyakataa matokeo ya uchaguzi" ni kitisho cha dhahiri, si kwa vyama vya siasa na wagombea pekee, bali pia ni dhidi ya jitihada za kujenga na kuimarisha utawala bora na demokrasia kwa ujumla hapa nchiniTanzania. Ni dhahiri Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo anafahamu kuwa si wanajeshi wala silaha zinazoweza kulazimisha wananchi, vyama vya siasa na wagombea wao wakubaliane na matokeo ya uchaguzi bali uchaguzi unaokubalika miongoni mwa washindani na wananchi kwa ujumla kuwa umefanyika kwa kuzingatia vigezo vya msingi vya chaguzi huru na haki. Katika kutimiza hili, usimamizi imara na usiokuwa na upendeleo, na vyombo vya usalama na vyombo vya habari visivyopendelea upande wowote ni nguzo muhimu kuhakikisha washindani wa kisiasa wanakubaliana na matokeo ya uchaguzi. Yaliyotokea katika nchi za Romania, Ukraine, Zimbabwe, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na kwingineko duniani ni mifano inayotoa mafunzo ya kutosha kwa raia na wanajeshi pia. Hakika hili halihitaji tamko la Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Kama hivyo ndivyo, wanaFemAct hatuoni sababu iliyopelekea Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa tamko lake, na hasa katika kipindi hiki ambacho kampeni zinaendelea vizuri. FemAct hatuko tayari kuona Tanzania inapitishwa ya machafuko ya kupandikiza kwa lengo la kunufaisha kikundi maslahi cha watu wachache.

  Kwa kuzingatia sababu zetu hapo juu, wanaFemAct tunapendekeza ifuatavyo:
  a). Vyombo vya Ulinzi na Usalama viache mara moja kuingilia mchakato wa uchaguzi kwa kuwa jambo hili linaweza kusabaisha vitisho na vurugu dhidi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla; kuchafua hali ya amani na usalama ambayo ni tunu ya Tanzania. Lakini iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo, basi sheria husika sharti zifuatwe, Jeshi la Polisi likiwa na dhamana ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

  b). Wanasiasa, vyama vya siasa na viongozi waache mara moja kujitafutia ushindi kwa kutumia mlango wa nyuma. Uongozi wa dola sharti upatikane kupitia mashindano ya wazi kusaka ridhaa ya wananchi kidemokrasia katika uchaguzi unaokubalika kuwa huru na haki, siyo kutumia vyombo vya Ulinzi na Usalama kutisha wapiga kura ili kujihakikishia ushindi.

  c). Vyombo vya habari viendelee kuhabarisha wananchi na wapiga kura juu ya mipango ya sera za vyama vya siasa na ahadi za wagombea kama inavyojiri katika mikutano ya kampeni.

  d). Asasi za kiraia ziendelee kuelimisha wananchi juu masuala mbalimbali yanayoongeza uangavu kwa wapiga kura, na wananchi kwa ujumla juu ya sheria, taratibu, kanuni za uchaguzi, haki na wajibu wa kuhudhuria mikutano ya kampeni, kusikiliza ahadi za wagombea, kufanya maamuzi na hatimaye kujitokeza kupiga kura.

  e). Wapiga kura waendelee kujibidisha kupata elimu ya mpiga kura, kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na wagombea, na kusikiliza kwa makini ahadi za wagombea wakipembua na kuchambua kati ya pumba na mchele ili kunako Oktoba 31 wafanye uamuzi kwa kihistoria kuchagua viongozi watakaoweza kushirikiana na wananchi kukwamua Taifa letu kuondokana na umaskini na kuletea Taifa heshima.


  Mwisho/

  FemAct

  Dar es Salaam, Oktoba 6, 2010.
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,200
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Ina maana hii hali ya hatari iliyotangazwa inahusu mikoa yote ya Tanzania au? LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO SASA BASI LAJA!
   
 7. l

  lwangwa Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kura yangu mimi na mke wangu tumamua kumpa mkombozi wetu DR Slaa,BABA NA MAMA YANGU YAANI NISEME UKOO WOTE TUNAPIGIA DR Slaa
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  CUF walipita humo humo, na leo wapo wapi?
   
 9. M

  Msharika JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shimbo atoswe au anachochea uhaini
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tatizo viongozi wa juu wa jeshi Tanzania wana nguvu kuliko hata viongozi wengine wa siasa na hili ni tatizo sasa JWTZ hapa inahusika nini? Hatutoshangaa kuwa wameamuriwa kuipigia CCM tena na mishahara yao ilivyoongezwa kiholela hivi karibuni basi shida tupu
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Prevention is better than cure
   
 12. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  The good thing hawataisha milele
   
 13. P

  Preacher JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JESHI na MUNGU ANAYEONA UNYONGE WA WATANZANIA - NANI MWENYE NGUVU????? KATIKA YOTE TUMTEGEMEE MUNGU PIA
  WATU WANAO SUPPORT CCM WAMESAHAU KUWA KUNA BAADHI YA NDUGU ZAO PIA WANAKANDAMIZWA KATIKA NCHI YAO WENYEWE

  SIJUI WAMESHIKWA NA USINGIZI GANI TOKA KUZIMU????????????????? :angry:
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  NEC leo wanasema hakuna tatizo lolote kwenye kampeni ni amani tupu!!!!!!! (The Guardian 07/10/2010).
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hizo taarifa za kijasusi walizopewa akina Shimbo watakuwa wamedanganywa kwani kama mkuu udangaywa tutarajie nini kwa wa chini yake? Shimbo ameshindwa kutoa uthibitisho kwa sababu taarifa hizo wamezipata kutoka kwa Shekhe Yahya!!!!!!!!!

  Kwanza kule Ngara ujambazi ni wa hali ya juu, JWTZ waliwahi au wanamsaidia Venance Tossi wa polisi? Wakajenge kambi kwenye ule msitu mnene wa Ngara ili kulinda raia dhidi ya majambazi kutoka nchi jirani! Kwanza ana elimu gani na kwa kiwango gani? Au ndio wale wanapanda cheo kwa sababu wanalenga sana shabaha kwenye range!
   
 16. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Hizo taarifa za ki-intelijensia za kuhatarisha amani anazodai shimbo mbona haziko wazi!!!!! Atuondoe wasiwasi kwa kuziweka hadharani la sivyo hio ni conspiracy tu yenye nia ya kuvuruga uchaguzi wetu......Wa-tz tusidanganyike...
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  ...........Mwaka huu hamchomoki........!!!!
   
 18. Nostradamus

  Nostradamus JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umegubikwa na moyo wa kiuana mapinduzi na umechoshwa na makosa ya viongozi wetu mpaka umekuwa kipofu wa kushindwa kuona udhaifu wa CHADEMA. kila siku najaribu kuwaelimisha watu kuwa THRE IS NO PROBLEM WITH dr SLAA lakini CHADEMA ni uozo uliooza na kuvunda kiasi cha kutisha. kumbuka,,, kama SLAA angesimama kama mgombea binafsi, basi hata mimi ningetumia nguvu zangu zote kumuunga mkono.
  lakini slaa chini ya chadema na akina MBOWE,MALISA,KOMU,LYIMO, MASAWE na CHUA.,, huku hivi sasa kikiwa kimeshajivika na kilemba kingine cha udini(ukristu) kinakosa sifa ya kuwa chama tawala kwani mgawanyiko na upendeleo utakuwa ni wa wazi na dhahiri.
  I am with DR SLAA and will always be, but not when associating him with CHADEMA
   
 19. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  unapiingiza mambo ya dini katika siasa unaonyesha dhahiri jinsi ulivyo na upeo mdogo wa kifikra na kielimu, wewe ni mnafiki, mchochezi na mdini mkubwa unahatarisha usalama wa nchi kama shimbo na jk
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wacha ile kitu ya mkoa mmoja wa kwenu. Tukiliwasha wewe lazima urudi zenji!
   
Loading...