Amini Usiamini, Ukitenda Wema, Mema Yatakurudia. Kisa cha Rafiki Yangu Aliyeishi Dar.

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Hki ni kisa cha kweli kilichotokea Dar es Salaam kwenye miaka ya tisini na.... Na kilishawahi kuandikwa mahali na pengine baadhi ya wanaMMU wanakifahamu. Haya tuanze.
Huyu rafiki yangu, naomba tumwite James, alikuwa mtu aliyenipita sana umri na tulifahamiana wakati mimi nasoma chuo kimoja kilichopo Dar.Alikuwa anafanya kazi wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa na kuishi Mwenge.
Kipindi fulani alitakiwa kwenda Afrika Magharibi kuhudhuria mkutano. Safari yake ikaandaliwa vizuri na ilikuwa apande ndege toka Uwanja wa ndege wa kimataifa Dar-es-Salaam.Siku ya safari akaondoka Mwenge asubuhi kama saa tatu hivi kuelekea uwanja wa ndege akiendesha gari yake. Njiani, maeneo ya Kinondoni, akaona kundi la wanawake, mmojawao akimwashiria kuomba lift. Jamaa akaanza kuwaza, Hawa wamama wana tatizo gani? Na ntawezaje kuwasaidia ilhali nakimbilia ndege ya kwenda mkutanoni?
Kitu kikamwambia asimame awasikilize, na kweli akafanya hivyo. Kumbe mama mmoja mjamzito alikuwa kwenye hali mbaya ya uchungu alihitajika kukimbizwa Muhimbili kujifungua. James akashindwa kukataa, akamchukua mgonjwa na huyooo mpaka Muhimbili. James hakuondoka hospitali mpaka taratibu zote za kumpokea mgonjwa zilipoisha na mgonjwa kulazwa wodini.Alipotazama saa yake, ilikuwa saa tano kasoro muda ambao ndege ilikuwa imeshaondoka. kwa hiyo safari ya Afrika magharibi ikawa imekufa! Jamaa hakuwa na jingine la kufanya ila kujirudia nyumbani.Kesho yake alienda kazini akiwa na kisingizio kikali kwa nini hakuenda safari. Akaendelea na kazi mpaka kile kisa cha lift akaanza kukisahau kwa jinsi miaka ilivyosonga mbele.
Ilipofika mwaka 1999 James akastaafu kazi. Katika kumudu maisha ya kustaafu, akaamua atafute shamba ili ajenge na kulima.Akaulizia mambo ya shamba kwa marafiki zake, na mmoja akamwambia kwamba kuna shamba linauzwa maeneo ya Boko.
James na rafiki yake wakapanga kwenda Boko Jumamosi moja na rafiki akampeleka kwa muuza shamba. Muuza shamba alikuwa mwanamke, na James alistuka sana kwa jinsi yule mwanamke alivyokuwa anamtazama wakati wanazungumza.Yule mwanamke aliacha mazungumzo na kumwambia James," Kama nakufananisha naomba unwie radhi, lakini unafanana sana na baba mmoja aliyenipa lift ya kwenda muhimbili niliposhikwa na uchungu wa mwanangu Joyce" James akajibu,"Ndiyo, hiyo lift naikumbuka sana ila huyo mwanamke simkumbuki" "Ilikuwa ni mimi! Mimi!" Yule mama alisema kwa furaha huku akirukaruka na kuendelea kusema,"Kama shida yako ni shamba babangu,njoo huku kuna shamba lako nimeakuandalia na wala sitaki shilingi ya mtu." James alikabidhiwa shamba la ekari sita.
 
Fe Lady,kutenda ubaya ni hatari sana. Wala hutakiwi kufikiria hivyo!
 
Not always. . . wakati mwingine unaweza ukajuuuuuuuta kumsaidia huyo mtu. Muhimu wewe saidia bila kutegemea chochote ili akikulipa kwa wema au kwa ubaya uone sawa tu.

Hongera kwa rafiki yako!!

Sawa kabisa! Unaweza msaidia mtu akaja kukutukana baadaye. Saidia, sahau! Ila hadithi kama hiyo hapo juu inaweza kabisa kutokea, dunia si kubwa sanaaa
 
Not always. . . wakati mwingine unaweza ukajuuuuuuuta kumsaidia huyo mtu. Muhimu wewe saidia bila kutegemea chochote ili akikulipa kwa wema au kwa ubaya uone sawa tu.

Hongera kwa rafiki yako!!
Sawa Lizzy na asante. Hongera zimepokelewa. Halafu Lizzy hebu nenda kule Jukwaa la Elimu, kuna thread inahitaji mchango wako.
 
Fe Lady,kutenda ubaya ni hatari sana. Wala hutakiwi kufikiria hivyo!
Kuna mtu mmoja mara kwa mara ananitendea ubaya,Namwomba Mungu kila siku amuadhibu walau avunjike hata kiuno,cha ajabu jamaa anadunda kila siku,ndo maana nkauliza
 
si kila unayemsaidia anakuwa na moyo kama huyo mama, wengine wanaishia kukufanyia vituko ile mbaya....
 
Kuna mtu mmoja mara kwa mara ananitendea ubaya,Namwomba Mungu kila siku amuadhibu walau avunjike hata kiuno,cha ajabu jamaa anadunda kila siku,ndo maana nkauliza
Wee msanehe tu Fe Lady. Kumtakia mbaya wako mambo mabaya ni sawa na kulipiza kisasi.Matokeo yake utaumia we mwenyewe kwa sababu ukiona anadunda unaumia roho. Utautesa mwili wako kwa kuumia roho kila wakati.
 
Ni mmoja kwa mia wengi wanalipa dharau na unyama.
Saidia uende zako usingoje shukrani!
 
Not always. . . wakati mwingine unaweza ukajuuuuuuuta kumsaidia huyo mtu. Muhimu wewe saidia bila kutegemea chochote ili akikulipa kwa wema au kwa ubaya uone sawa tu.

Hongera kwa rafiki yako!!

haaah haaah Lizy wanikatisha tamaa, mm nasaidia sana hasa jinsia yako lol.
 
Mpatanishi wala usikate tamaa, we saidia tu bila kutegemea hata ahsante in return and you'll be just fine. Ukiwa na mategemeo ndio utakua disappointed. . kama huna chochote utaona sawa tu. Mi nilijifunza the hard way so I know.
 
ok lizy na ww ukiwa na shida niambie, sawa mrembo?! Nitakusaidia lol.
 
Hki ni kisa cha kweli kilichotokea Dar es Salaam kwenye miaka ya tisini na.... Na kilishawahi kuandikwa mahali na pengine baadhi ya wanaMMU wanakifahamu. Haya tuanze.
Huyu rafiki yangu, naomba tumwite James, alikuwa mtu aliyenipita sana umri na tulifahamiana wakati mimi nasoma chuo kimoja kilichopo Dar.Alikuwa anafanya kazi wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa na kuishi Mwenge.
Kipindi fulani alitakiwa kwenda Afrika Magharibi kuhudhuria mkutano. Safari yake ikaandaliwa vizuri na ilikuwa apande ndege toka Uwanja wa ndege wa kimataifa Dar-es-Salaam.Siku ya safari akaondoka Mwenge asubuhi kama saa tatu hivi kuelekea uwanja wa ndege akiendesha gari yake. Njiani, maeneo ya Kinondoni, akaona kundi la wanawake, mmojawao akimwashiria kuomba lift. Jamaa akaanza kuwaza, Hawa wamama wana tatizo gani? Na ntawezaje kuwasaidia ilhali nakimbilia ndege ya kwenda mkutanoni?
Kitu kikamwambia asimame awasikilize, na kweli akafanya hivyo. Kumbe mama mmoja mjamzito alikuwa kwenye hali mbaya ya uchungu alihitajika kukimbizwa Muhimbili kujifungua. James akashindwa kukataa, akamchukua mgonjwa na huyooo mpaka Muhimbili. James hakuondoka hospitali mpaka taratibu zote za kumpokea mgonjwa zilipoisha na mgonjwa kulazwa wodini.Alipotazama saa yake, ilikuwa saa tano kasoro muda ambao ndege ilikuwa imeshaondoka. kwa hiyo safari ya Afrika magharibi ikawa imekufa! Jamaa hakuwa na jingine la kufanya ila kujirudia nyumbani.Kesho yake alienda kazini akiwa na kisingizio kikali kwa nini hakuenda safari. Akaendelea na kazi mpaka kile kisa cha lift akaanza kukisahau kwa jinsi miaka ilivyosonga mbele.
Ilipofika mwaka 1999 James akastaafu kazi. Katika kumudu maisha ya kustaafu, akaamua atafute shamba ili ajenge na kulima.Akaulizia mambo ya shamba kwa marafiki zake, na mmoja akamwambia kwamba kuna shamba linauzwa maeneo ya Boko.
James na rafiki yake wakapanga kwenda Boko Jumamosi moja na rafiki akampeleka kwa muuza shamba. Muuza shamba alikuwa mwanamke, na James alistuka sana kwa jinsi yule mwanamke alivyokuwa anamtazama wakati wanazungumza.Yule mwanamke aliacha mazungumzo na kumwambia James," Kama nakufananisha naomba unwie radhi, lakini unafanana sana na baba mmoja aliyenipa lift ya kwenda muhimbili niliposhikwa na uchungu wa mwanangu Joyce" James akajibu,"Ndiyo, hiyo lift naikumbuka sana ila huyo mwanamke simkumbuki" "Ilikuwa ni mimi! Mimi!" Yule mama alisema kwa furaha huku akirukaruka na kuendelea kusema,"Kama shida yako ni shamba babangu,njoo huku kuna shamba lako nimeakuandalia na wala sitaki shilingi ya mtu." James alikabidhiwa shamba la ekari sita.

Stori yako ni nzuri na inafundisha ila imekaa kama imetungwa maana unavyosema huyo mama alikuwa amemwandalia shamba wakati alikuwa hana mawasiliano nae alijua je atajakutana nae?
 
Back
Top Bottom