Elections 2015 Amini Usiamini, Kama Mwalimu Angekuwa Hai Hadi Leo!, Angemsupport Edward Lowassa!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Wanabodi,

Wakati Watanzania tukijiandaa kukumbuka kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwallimu Nyerere, naomba kutoa angalizo la kuizuia kumbukumbu hiyo isitumike vibaya kuupotosha umma eti kuna watu Mwalimu aliwakataa!, yes anaweza kuwa aliwakataa wakati ule ile kama angekuwa hai hadi leo, angewakubali sana tuu!.

Kiumri mimi ni mtu mzima nitaitafuta 50 kwa karibu!.

Kikazi, mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea!. Kwa mara ya kwanza kuingia newsroom ilikuwa ni mwaka 1990 ndani ya chumba cha habari cha gazeti la serikali Daily News, hivyo kama ningekuwa bado niko kazini mpaka leo, mwaka huu ningesherehekea miaka 25 ya uandishi wa habari!.

Katika kipindi hicho, Mwalimu Nyerere alikuwa ameishastaafu na sikuwahi kukosa kuhudhuria press conference yake yoyote, hivyo Mwalimu ninamfahamu fika!. Tena ilitokea, nadhani mimi ndio mwandishi wa habari wa Tanzania kufanya mahojiano ya mwisho na Mwalimu, ambayo niliyafanya mwaka 1998, katika ukumbi wa The Bundes House, katika mji wa Bern Nchini Uswisi, baada ya hapo alianza kuugua hadi Mwenyeenzi Mungu alipomuita kumpumzisha!, hivyo Mwalimu Nyerere huyu ninayemzungumza hapa, ni Mwalimu ninayemfahamu kwa kuzungumza naye ana kwa ana na sio Mwalimu wa kumsikia, kumuona au kuhadithiwa!.

Katika ule mkutano wake na waandishi wa habari Katika Hoteli ya Kilimanjaro, alipokuwa anazungumzia kuuzwa kwa benki ya NBC, Mwalimu alitokwa machozi kwa uchungu!, leo angekuwepo na kusikia sio tena kuuzwa kwa benki tuu bali viongozi wa umma, wenye uwezo wa kujenga nyumba zao, na baadhi yao wenye majumba yao tayari, lakini wakayachukua majumba ya umma na kujigawia bure, kwa kuweka vijisenti kidogo vya kudanganyia!, leo mtekelezaji wa uharamia huo, ambaye sio tuu alijigawia pande nono, bali pia aliwagawia na ndugu zake, rafiki zake, jamaa zake, hadi vimada wake kadhaa!, jambo kama hili, Mwalimu angekuwepo, asingelikubali!, angemchagua Lowassa!.

Nakiri nimekuwa inspired kuandika bandiko hili, kutokana na swali la mwana jf huyu,
Pasco wa JF, naomba jibu lako,

Naomba kumwuliza Pasco wa JF kuhusu Nyerere, kama Mwl angekuwepo, Je, Lowasa angegombea Urais? Ni swali ambalo nitafurahi sana wanaccm wakinijibu kwa dhamiri safi, ni maombi yangu kuwa PASCO wa JF hataingia Mtini.

WENU

Mikael Aweda.
Mkuu Shemeji,Mikael P Awedak amini usiamini, kama Mwalimu angekuwa hai hadi leo, angejiunga na Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema upinzani wa kweli, utatoka CCM!, this is that time Mwalimu aliyoisemea!.

Mimi ni muumini wa life after life!, Mwalimu huko aliko anampigania Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema, watu wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM!.

Pasco
 
Mkuu pasco mimi nimekua inspired na wasifu wako

Hope ni ukweli mtupu

Ahsante kwa kushare nasi hilo leo
 
Mnatafuta uhalali ili Lowassa akubalike kwa watu wenye fikra pana mpaka mnajaribu kuwa wapiga ramli au kuingia kwenye akili za Mwl. Nyerere.

Kuna wazee wenye Hekima na Busara kama kina Butiku ambao walifanya kazi na Mwl. Nyerere lakini mpaka leo wanasema hawakuweza kuzielewa fikra zake.

Uchaguzi wa mwaka huu tutaona na kusikia mengi!

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Simemi Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu ya kuendelea kudhoofu kifikra na kiafya, bali kutokana na historia yake mbaya katika kusimamia maslahi ya Watanzania.
 
Ni kweli Pasco. Penye ukweli ni kusema bila kumumunya maneno. Mimi ni MTU mzima mwenzio na rasmi nitapigia kura Lowassa.
 
Last edited by a moderator:
una 50+ lakini nisamehe nayotaka sema maana mm hata sikukaribii huo umri lakini punguza njaa. Kama mwandishi wa habari mzoefu hautakiwi kuomesha kabisa unaandikia njaaa njoo na hoja zinazoeleweka
 
Wanabodi,

Wakati Watanzania tukijiandaa kukumbuka kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwallimu Nyerere, naomba kutoa angalizo la kuizuia kumbukumbu hiyo isitumike vibaya kuupotosha umma eti kuna watu Mwalimu aliwakataa!, yes anaweza kuwa aliwakataa wakati ule ile kama angekuwa hai hadi leo, angewakubali sana tuu!.

Kiumri mimi ni mtu mzima nitaitafuta 50 kwa karibu!.

Kikazi, mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea!. Kwa mara ya kwanza kuingia newsroom ilikuwa ni mwaka 1990 ndani ya chumba cha habari cha gazeti la serikali Daily News, hivyo kama ningekuwa bado niko kazini mpaka leo, mwaka huu ningesherehekea miaka 25 ya uandishi wa habari!.

Katika kipindi hicho, Mwalimu Nyerere alikuwa ameishastaafu na sikuwahi kukosa kuhudhuria press conference yake yoyote, hivyo Mwalimu ninamfahamu fika!. Tena ilitokea, nadhani mimi ndio mwandishi wa habari wa Tanzania kufanya mahojiano ya mwisho na Mwalimu, ambayo niliyafanya mwaka 1998, katika ukumbi wa The Bundes House, katika mji wa Bern Nchini Uswisi, baada ya hapo alianza kuugua hadi Mwenyeenzi Mungu alipomuita kumpumzisha!, hivyo Mwalimu Nyerere huyu ninayemzungumza hapa, ni Mwalimu ninayemfahamu kwa kuzungumza naye ana kwa ana na sio Mwalimu wa kumsikia, kumuona au kuhadithiwa!.

Nakiri nimekuwa inspired kuandika bandiko hili, kutokana na swali la mwana jf huyu,
Mkuu Shemeji,Mikael P Awedak amini usiamini, kama Mwalimu angekuwa hai hadi leo, angejiunga na Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema upinzani wa kweli, utatoka CCM!, this is that time Mwalimu aliyoisemea!.

Mimi ni muumini wa life after life!, Mwalimu huko aliko anampigania Lowassa!.

Ni Mwalimu ndie aliyesema, watu wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM!.

Pasco

Pasco!!!!.!!
 
Mnatafuta uhalali ili Lowassa akubalike kwa watu wenye fikra pana mpaka mnajaribu kuwa wapiga ramli au kuingia kwenye akili za Mwl. Nyerere.

Kuna wazee wenye Hekima na Busara kama kina Butiku ambao walifanya kazi na Mwl. Nyerere lakini mpaka leo wanasema hawakuweza kuzielewa fikra zake.

Uchaguzi wa mwaka huu tutaona na kusikia mengi!

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Simemi Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu ya kuendelea kudhoofu kifikra na kiafya, bali kutokana na historia yake mbaya katika kusimamia maslahi ya Watanzania.

Mwalimu angekuwepo asingevumilia kukaa ndani ya ccm hii ya leo ambayo imejaa kila aina ya upuuzi.Lowasa ni MTU muadilifu ndio maana hata tuhuma anazotuhumiwa zinaonekana wazi ni za kupikwa lzm tumchague kuwa Rais.
 
Ni kweli Pasco. Penye ukweli ni kusema bila kumumunya maneno. Mimi ni MTU mzima mwenzio na rasmi nitapigia kura Lowassa.
Nashukuru Pasco sikupata kuwa karibu sana na Mwl kama wewe ila nilisoma Mgorombe au Butuguri S/M mwanzoni mwa miaka ya 70 ( kwa umri nakuzidi sana pasco kwani nakaribia 60). Kwa ujumla nilikutana na mwl mara nyingi kanisani magorombe (Butuguri) na mimi nilikuwa natumikia hapo kanisani. Ninaungana na ninyi wote Mwl angemsapoti Lowasa ndiyo maana na mimi namuuunga mkono Lowasa.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
With due respect mkuu, mtu akisoma posts zako kuhusu Lowassa na Magufuli hakuna consistence. Ni kama vile unabadilika kulingana na matukio. Kuna rafiki yangu mmoja mwingereza hii alipenda kuita "flip-flop".
 
Wanabodi,
Ni Mwalimu ndie aliyesema upinzani wa kweli, utatoka CCM!, this is that time Mwalimu aliyoisemea!.

Mimi ni muumini wa life after life!, Mwalimu huko aliko anampigania mtu

Ni Mwalimu ndie aliyesema, watu wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM!.

Pasco
Happy Nyerere Day!.
P
 
Back
Top Bottom