Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

Ruta. Ni kweli ni matatizo ya Kimfumo, lakini ni nani alyekuwa Mratibu mpaka mfumo huo ukawa kama ulivyo ? Kwa maana kwamba huyo tayari ameishasababisha watu kukata tamaa na watu wake; hivyo, kwa mfumo huo huo tutashuhudia idadi ndogo ikijitokeza kupiga kura kwa kisingizi kuwa mfumo utatoa viongozi wale wale wasiofaa kwa hiyo ni afadhali mtu akae mtaani akipiga soga kuliko kushiriki kuchagua kiongozi asiyefaa

sawabho tatizo ni kuwa huyo anajiandaa kumrithi anakuja na mfumo uleule....tutakimbilia wapi akiisha kamata dola kwani atarudia madudu yaleyale.......
 
Last edited by a moderator:
Unataka wawaige CCM? muhimu ni kukomesha Ufisadi na Rushwa hata ukiwa na wabunge wasio viongozi kama Badwel wa BAhi nchi itaenda wapi?
Kifupi rudi ukafanye tena huo 'Upembuzi Yakinifu' tangu 2010.
Mambo ya msingi kimaamuzi yaliyofikiwa hapa kwetu, yamefikiwa kwa nguvu ya CHAMA gani?
Na mambo hayo hayo yalikuwa yakipingwa na CHAMA gani?
Na kama hautakuwa na aibu ebu jaribu kutaja mashujaa 10 wa kisiasa wapigania haki za wananchi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita hapa nchini!.

Kyaiyembe hilo swali lako linanithibitishia bado hujanielewa................cdm ni ccm-b kimfumo wa uendeshaji wa chama hicho sawa na vyama vyote vya upinzani.........................

matatizo ya ccm ni ya kimfumo na hivyo cdm inayo ila hayaonekani kwa sababu bado hawajakamata dola na watakapokamata dola ndipo yatajitokeza kuwa hakuna uthibiti wa wanasiasa kutoka ndani ya chama na hujithibiti wao wenyewe........................
 
Last edited by a moderator:
lemonade...dhamira haipo lakini angalau hata wameanza na cdm wako wapi katika kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa chama chao kwa kutenganisha shughuli za chama na za serikalini ambalo ndilo chimbuko kuu la ufisadi?.wanadai vua gamba vaa gwanda ........................gwanda lipi ambalo lina gamba la mfumo wa ki-ccm?...............let us be serious and talk some serious issues about governance inside cdm.......................nobody knows anything there apart from cashing in on our poverty...............

First and formost naomba tukubaliane kuwa CCM washapoteza moral authority zamani mno na chochote wanachokifanya sasa ni kujaribu kutukosha tu
Nakubaliana na wewe Rutashubanyuma kuwa tunahitaji transparency na kurekebisha lakini sikubaliani na wewe kuipa CCM benefit of the doubt yani kwa sasa iko beyond repair....nashauri tujikite kuwa na CDM bora na sio kwa ku mock tu ebu utoe constructive opinion kuliko kuponda tu
 
Last edited by a moderator:
sawabho tatizo ni kuwa huyo anajiandaa kumrithi anakuja na mfumo uleule....tutakimbilia wapi akiisha kamata dola kwani atarudia madudu yaleyale.......

Hilo ni tatizo ambalo limekuwa likikumba nchi nyingi na taasisi nyingi; watu wanachoka na mfumo fulani wanafanya mabadiliko, anayekuja kumbe naye kalelewa na mfumo huo huo napoingia anaendeleza huo huo tena zaidi ya aliye toka !!! Rejae vitabu .....the Beautiful Ones are not yet Born... Not Yet Uhuru...... An Enemy on the People..........Pa kukimbilia ni kuchukua tahadhari wakati wa kufanya mabadiliko au kuanza na mabadiliko madogo kama sehemu ya somo kwa wahusika ili wabadilike. Wakishaindwa kubadilika, mnafanya mabadliko makubwa bila kuchukua tahadhari kwa maana kwamaba liwalo na liwe. Chukua mfano wa Wabunge wa Upinzani wanavyoongezeka, ni somo tosha kuwa mabadiliko madogo madgo yameanza.
 
Nibakizie nafasi ya kuchangia baadaye.
Ngoja nikafanye kazi ya boss
 
Kyaiyembe hilo swali lako linanithibitishia bado hujanielewa................cdm ni ccm-b kimfumo wa uendeshaji wa chama hicho sawa na vyama vyote vya upinzani.........................

matatizo ya ccm ni ya kimfumo na hivyo cdm inayo ila hayaonekani kwa sababu bado hawajakamata dola na watakapokamata dola ndipo yatajitokeza kuwa hakuna uthibiti wa wanasiasa kutoka ndani ya chama na hujithibiti wao wenyewe........................
Naona nitakuwa mchoyo kama nitakuwekea nukuu tu chache! sasa ingia hapa
http://www.google.co.tz/url?sa=t&rc...8PitDA&usg=AFQjCNE-QlR_eSRq2y1aCO0tINmr6PHvRA
Ukurasa wa 11 Ibara ya 6.1. Au soma yote ikusaidie
Mimi sijawahi kuwa manachama wa CCM. Naijua kidogo lakini hazifanani kimuundo katu.
 
Lemonade...​unaonekana ni mwanamke mwenye muamko wa kisiasa...nahitaji casual friend kama wewe...
 
KUna great thinker fulani hapa muda umepita aliifannanisha CDM na wale characters ( especially Napoleon) wa kitabu cha animal farm...
 
Ndugu Rutashubanyuma sasa naona Noshubenyuma......Tofauti na maana ya kikwetu juu ya jina lako.....
Mimi nawasiwasi na uchambuzi wako katika siasa za hapa kwetu Tanzania kwakutumia kigezo cha chako kisichokuwa na mashiko!!CCM imekuwa madarakani nadhani zaidi ya miaka 40 Iweje leo ufananishe na chadema yenye miaka 5 ya maendeleo??CCM kwa ufupi ni madikiteta kuliko chama chochote Tanzania kwanza udikiteta wao nikatika mfumo mzima wa uongozi wa nchi kama haujatambua.......Kifupi ni juu ya kauli za Nape alivyoenda Kusini na kumuagiza Waziri!!aliyeteuliwa na Rais!!!Hapo unaona udikiteta wapi umejikita CCM tazama walivyo kwapua mali za nchi hii!!Bado nasikitika kuwa mtazamo wako kwa upinzani siyo linganifu!!!....Nidemokrasia unaruhusiwa kuonge chochote bila kuvunja sheria!!

Unajua tatizo Rutashubanyuma amejikita sana kwenye thread za malavidavi leo karudi kwenye siasa kumbe yupo 2 years behind.Mkuu Ruta uko behind mzee embu ji update urudi tena na posti nyingine ila kama umeanzisha thread kupima upepo haina shaka kwa sasa sina mengi
 
Mkuu@Rutashubanyuma Kwa Mawazo yangu mimi Ningependa Rais wa nchi asitoke chama chochote kile kiwe cha chama cha C.C.M. Au CUF au Chadema au TPL. Au NccR Mageuzi kama ningelikuwa mimi mmoja wapo wanayepanga kutunga

Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania ningelitowa huo ushauri wangu. Nasema hivyo kwa sababu zangu si umeona Rais wa C.C.M. mpaka hii leo kuna maendeleo gani hapo nyumbani? zaidi ya umasikini uliojaa kila sehemu ? Sasa hata ikifika wakati wa uchaguzi ujao

kwa mfano chama chochote kile cha upinzani kitakacho shinda hakutokuwa na mabadiliko yoyote yale ya haraka kwa sababu Rais atakaye kuwepo madarakani ndie anacho kiongoza hicho chama kilichoshinda katika uchaguzi hata Mkimlaumu vipi mabadiliko

hayawezi kuja kwa haraka kama mnavyo mnavyotaka. Lakini ikiwa Rais hatakuwa na chama chochote kile ila tu huyo Rais kachaguliwa na Wananchi huyo Rais atakuwa hana upendeleo wowote ule kwani atakuwa ni Rais Mkweli na Muadilifu na asiyekuwa na chama chohote

anacho kipendelea na huyo Rais akifanya kosa ni Rahisi kukosolewa au hata kujiuzulu kuliko Rais anayechaguliwa na chama kinachotawala akikosea mna mngojea mpaka wakati wa uchaguzi ndio mumng'owe madaraka yake huo ndio ushauri wangu mimi asante.

Huyo Rais asiyefungamana na vyama utamtoa wapi? Atatumia mfumo gani wa kiutawala kusimamia watu wanaofungamana na vyama?

Chama hakiwezi kuwa bora kwa 100% na ndio maana kuna kitu kinaitwa dira ya taifa ambayo hiyo vyama ndo vinatakiwa kuandika ilani zao ya jinsi gani zitatufikisha pale Dira inapotaka tufike tofauti na sasa ambapo kila chama kinajiandikia tu vile kinavyoona inafaa kuwazuga wananchi. Dira ya taifa ishakuwepo sasa ni sera za vyama jinsi ya kuitekeleza hiyo dira ya taifa. Haya ndio yanayofanya huko USA vyama viwe vinatoana madarakani, ni katika mbinu za kutekeleza Dira ya Taifa.
 
Unapokuwa na mawazo yenye uzuri fulani weka mbali unafiki.

Tanzania inahitaji kiongozi imara na siyo kiongozi nafuu wa ufisadi toka ccm. Kama utasema democracy ipo ccm,je ni kweli kwamba J.K alifanya kazi nzuri sana awamu yake ya kwanza kiasi cha wanachama kutochukua fomu ya kugombea uraisi? Au kulikuwa na dirty game behind the scene? Jambo la msingi ni kushauriana kama vyama vyenye malengo ya kuwatumikia wananchi japokuwa kwa sasa ccm wanatuibia wananchi, Ili tuboreshe mifumo ya demokrasia ndani ya vyama vyetu.

Tunakubali kuwepo kwa madhaifu kadhaa kwenye demokrasia ya upinzani lakini sikubali kwamba udhaifu huo unaweza kutupatia raisi dhaifu sana kuliko yule ambaye atatoka magamba.
 
Sangarara hebu tueleze hivi katika khali hii ya Chadema kuiga mfumo wa kiutawala kutoka ccm wanao ubunifu wa kutupatia viongozi bora au kama siyo kuangalia ccm wanafanya uppuzi gani nao kukemea tu?

Rutashubanyuma naona kama unafanya mambo ya kimtego tego, Inamaana haujui kwamba kuna Hybrid Kibao za Democrasia?? Nadhani unafahamu vizuri namna wachina wanavyochagua Rais wao, hiyo ndio wao wanaita democrasia, hicho unachoona kama udictator ndani ya chadema hiyo ndio brand yao ya democrasia na sina hakika kama ni kweli CHADEMA wameiga mfumo wa CCM sababu hata namna walivyotuletea DR SLAA 2010 ni kwa mfumo tofauti kabisa na uliotumika ndani ya CCM na bado he was the best candidate way off kulinganisha na wa CCM.

Kwamba ni lazima chama kifuate mfumo fulani wa kujiendesha sidhani kama ni hoja yenye mashiko kwa sababu katika hii dunia hakuna kitu kinaitwa BEST PRACTICE japo kitu hiki kimekuwa kikilazimishwa kama unavyofanya wewe hapa, hata tukizungumzia dhana ya mabadiriko au kujivua gamba inategemeana na chanzo cha nguvu za kujivua gamba ama mkakati mzima wa kujivua gamba, ama sivyo badala ya kujivua gamba/kubadirika chama kinaweza kujikuta kinajimaliza kama ilivyo kwa CCM sasa.

Hivyo basi, Mimi naona mfumo unaofuatwa na CHADEMA uko SAFI KABISA na ushahidi ni kwamba chama hiki hakionekani kuwa na tatizo lolote la kutisha katika namna kinavyojiendesha zaidi tunashuhudia mafanikio baada ya mafanikio kila kukicha, ninaamini hiki chama kinaelekea Ikulu 2015.
 
huyo rais wa kutoka ccm atakuwa na wakati mugumi sana,maana atatakiwa afanye yale wakuu wake walichomwagiza.

Hebu ona, ccm hii ninayoijua haina desturi ya kuwajibishana, mtu akaitenda tofauti na wajibu wake wa kazi, anahamishwa kitengo ili akaharibu sehemu ingine, pia kuna hili la kurithishana vyeo, ambalo nalo ni tatizo kubwa,wabadhilifu wa fedha za uma wanawalea na wakati mwingine wanawatetea wakidai eti ni watendaji wa chini ndio wanaosababisaha ubadhilifu, utasikia kila anaeombwa (maana kwao lazima uelezwe kirafiki, wakuu hawataki lawama bwana) kujihudhulu, eti sio yeye ila watendaji wa chini.

Kwa hali tuliyonayo nchini sasa,tunapaswa tuwe na viongozi amabo watasimamia mapato na matumizi ya serikali kwa hali ya juu, urafiki, asante, bakshishi, mtoto wa dada,inabidi viepukwe kwa kiwango kikubwa sana, ambacho ndo CCM imefanya hali hii iwepo. Kila tukisikia mradi wowote nchini. Ni kwamba tumesaidiwa na watu flani au nchi flani, sisi pesa yetu inafanya nini? Watu waliajiriwa ndo wanaolipa kodi effectively, wawekezaji wakubwa hawalipi kodi kabisa,utasikia mwaka huu mara paradise,baada ya mda JB.

Tunahitaji kupata viongozi wasifungamana na mambo haya ili nchi iendelee.na ikitokea ccm ikatoa raisi 2015, basi hali ya wananchi itakuwa mbaya mara tano zaidi ya sasa. Watu wengine wanaongea,hawajui wananchi wa kawaida wanaishi vipi hiko vijijini,
 
Sasa nimshagundua nini maana ya kuwa na mgombea binafsi!

Ndallo wewe una busara sana.....................lazima tupange tukutane hapa A-Town
 
Last edited by a moderator:
:biggrin1: ni kweli lakini.... yani rushwa sasa hivi iko kila mahali sio serikalini sio bungeni sio mahakamani sio TPA,TRA,TAKUKURU,TAZARA...hivi kuna shirika lolote la serikali ambalo liko safi??

mtotowamjini........umegusa pabaya..........na hilo wapenzi wa cdm hawataki kulisikia wanafikiri cdm hakuna ufisadi........duh
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom