Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jun 6, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Nimevipima vyama vya upinzani kwenye mizania yangu ya upembuzi yakinifu na kubaini bila ya mashaka yoyote yale bado havipo tayari kimfumo kutupatia Raisi bora na hizi ndizo nondo zangu zilizonifikisha hapo..:-

  a) Vyama vyote vya upinzani vimeiga mfumo mbovu wa kidemokrasia wa ccm na vinaendeshwa kibabe-kibabe mno na huku wenzao wa ccm kuanzia 2010 walianza kujivua gamba la udikteta pale waliporuhusu wabunge wake wachaguliwe na wananchi moja kwa moja...ingawaje bado wana safari ndefu kwenye hili lakini lazima niwapongeze ccm kwa angalau kujaribu....rushwa na kuingiliwa na ngazi za juu katika maoni ya wananchi ni changamoto ambazo ccm itabidi waendelee kuzitafutia muarobaini wake.

  Kwenye hili vyama vya upinzani wapo nyuma na tumeona hata chadema bila ya kupitisha kura ya maoni kwa wapigakura wa Arusha wakitumia kauli za kidikteta kukejeli kura za wanachama wao Arusha pale kamati kuu yao ilipotengua madiwani wakaidi wa Arusha...well, chadema worshippers...that was not democracy at all...it was dictatorship.........face it now before it is too late.....Only the truth will set you free

  b) Vyama vyote vya siasa vyenye wabunge Bungeni vimekumbwa na dhoruba kali la wizi na ubadhirifu wa ruzuku ya hazina na hakuna uthibiti wa aina yoyote ile!!!!!

  Kwa mtazamo wangu kama wapinzani wameshindwa hata kusimamia kidogo ambacho tumewapa ni kwa upuuzi upi utushawishi kuwakabidhi nchi yote?

  Njaa ya viongozi wa upinzani ni kali kulikoni ya viongozi wa ccm ambao pamoja na bandubandu kweli humaliza gogo lakini ccm hawana uchu wa kututafuna kama upinzani walionao.....ccm vibosile wake wamekwisha shiba njaa siyo kali sana kwa kipimo cha malinganisho.................lol

  c) Mchakato wa katiba mpya umenifungua macho hila na upofu wa wapinzani ambao waliipinga tume kwa vile wao hawajaweka mrija wao ndani yake na kunyonya Hazina baada ya CCM kuwaingiza kingi - au niseme mkenge? - hakuna anayehoji uhalali wa Tume ya kukusanya maoni.

  Wote wanaimba wimbo wa CCM wa ya kuwa tume tajwa haina uwalakini na sasa wamehamia kwenye mabunge mawili ambako wanaona mirija yao ni michache na kwa hiyo wanatafuta namna ya kuiongeza.

  Hii siyo demokrasia hata chembe bali ni ubinafsi tu...period. Mwanamageuzi wa kweli atadai haki hata kama yeye ni mwathirika wa hayo mageuzi siyo yule ambaye hujigeuza mpiga filimbi ya Hamelini pale anapoona masilahi yake yamepigwa na tufani kali sana...anachofanya ni kulinda tonge lake la ugali lisidondokee pabaya tu....lol hao kweli ni wababaishaji tu hawatufai kabisa.........

  USHAURI:

  Hivyo chama chochote kile cha siasa ambacho kitashirikisha wanachama wake katika kuteua viongozi watakaopeperusha bendera za vyama vyao katika ngazi zote ikiwemo ya URAISI, UBUNGE, UDIWANI hadi UENYEKITI WA KITONGOJI kina nafasi njema ya kutupatia viongozi bora...na kutumia utaratibu huohuo katika kuwavua madaraka itakuwa imepiga hatua katika demokrasia shirikishi.

  Have your say too...unaridhika na demokrasia ndani ya vyama vya siasa hasa hivi vya upinzani hata sasa kuviamini kutupatia Raisi na viongozi wengineo bora bila ya kutushirikisha grassroots?
   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mbona umegeuka wakati jina lako ni "RUTASHUBANYUMA" yaani "Asiyerudi nyuma"?
  Kwa hiyo kwako wewe, CCM kuwavumilia/kuwaogopa mafisadi ndani ya chama na kuwaambia kuwa wapime na kuamua wenyewe ndiyo demokrasia?

  Ndugu yangu Ruta, hiyo unayosema kuwa demokrasia si demokrasia ni "Anarchic democrasy" ambayo inaweza kumpa uhuru baba mtu kumbaka binti yake huku ikiwanyima watu uhuru wa kuhoji hilo tendo. Think twice!
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,258
  Trophy Points: 280
  Ndugu Rutashubanyuma sasa naona Noshubenyuma......Tofauti na maana ya kikwetu juu ya jina lako....

  Mimi nawasiwasi na uchambuzi wako katika siasa za hapa kwetu Tanzania kwakutumia kigezo cha chako kisichokuwa na mashiko!!CCM imekuwa madarakani nadhani zaidi ya miaka 40 Iweje leo ufananishe na chadema yenye miaka 5 ya maendeleo??CCM kwa ufupi ni madikiteta kuliko chama chochote Tanzania kwanza udikiteta wao nikatika mfumo mzima wa uongozi wa nchi kama haujatambua...

  Kifupi ni juu ya kauli za Nape alivyoenda Kusini na kumuagiza Waziri!!aliyeteuliwa na Rais!!!Hapo unaona udikiteta wapi umejikita CCM tazama walivyo kwapua mali za nchi hii!!Bado nasikitika kuwa mtazamo wako kwa upinzani siyo linganifu!!!....Nidemokrasia unaruhusiwa kuonge chochote bila kuvunja sheria!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu tupo wote mie siongelei ufisadi kwa sababu uko kwenye vyama vyote kama nilvyobaini ila ccm wao kwa vile wako madarakani ni rahisi kwa wapinzani kuibua mapungufu yao ambayo wao wakiingia madarakani leo watakuwa ni kioja nikiona jinsi ambavyo wanedesha mambo yao kwa ubinafsi mkubwa mno............

  hiyo hoja yako ya pili mie sijaielewa....................kuhusu kugeuka mie sitetei chama chochote kile hata ccm huwa nawaangushia makombora lakini lazima niweke hadharani mapungufu ya vyama vya upinzani kuwa havipo tayari kukamata dola mpaka pale vitakapopanua demokrasia ndani ya vyama vyao na kuwa bora kuzidi ya ccm..............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rutashubanyuma Kwa Mawazo yangu mimi Ningependa Rais wa nchi asitoke chama chochote kile kiwe cha chama cha C.C.M. Au CUF au Chadema au TPL. Au NccR Mageuzi kama ningelikuwa mimi mmoja wapo wanayepanga kutunga

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania ningelitowa huo ushauri wangu. Nasema hivyo kwa sababu zangu si umeona Rais wa C.C.M. mpaka hii leo kuna maendeleo gani hapo nyumbani? zaidi ya umasikini uliojaa kila sehemu ? Sasa hata ikifika wakati wa uchaguzi ujao

  kwa mfano chama chochote kile cha upinzani kitakacho shinda hakutokuwa na mabadiliko yoyote yale ya haraka kwa sababu Rais atakaye kuwepo madarakani ndie anacho kiongoza hicho chama kilichoshinda katika uchaguzi hata Mkimlaumu vipi mabadiliko

  hayawezi kuja kwa haraka kama mnavyo mnavyotaka. Lakini ikiwa Rais hatakuwa na chama chochote kile ila tu huyo Rais kachaguliwa na Wananchi huyo Rais atakuwa hana upendeleo wowote ule kwani atakuwa ni Rais Mkweli na Muadilifu na asiyekuwa na chama chohote

  anacho kipendelea na huyo Rais akifanya kosa ni Rahisi kukosolewa au hata kujiuzulu kuliko Rais anayechaguliwa na chama kinachotawala akikosea mna mngojea mpaka wakati wa uchaguzi ndio mumng'owe madaraka yake huo ndio ushauri wangu mimi asante.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kuhusu swala la madiwani wa Arusha.

  Mkuu, nadhani hapa tunatafsiri vibaya demokrasia. Tunawachagua viongozi wa kutuwakilisha. Na tunawachagua wale tunaoamini watawakilisha mawazo yetu. Madiwani wa Arusha walionekana dhahiri kuwa kuna harufu ya rushwa na wananchi walikuwa wanasema waziwazi hapa jijini. Waliposhauriwa, walipoonywa hawakusikia.

  Viongozi wetu wanajua tulichokuwa tunahitaji na kwa niaba yetu wakatimiza mahitaji yetu! Yaani wametuwakilisha kwenye ngazi ya maamuzi. Sidhani kama demokrasia ni kura ya maoni kwa kila jambo. Kuwa na viongozi wasioweza kutoa maamuzi pia ni tatizo kuliko demokrasia unayoisema.

  Ni hayo tu!
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  KakaKiiza......be real........ninachongelea ni mfumo wa kidemokrasia kwanza siyo kweli chadema wapo kwa miaka 5 tu walikuwepo kuanzia 1993-95 sasa hiyo ni karibu miaka 20 hivi wamefanya nini kuimarisha demokrasia ndani ya chama chao................angalia mbowe jinsi alivyojirundikia madaraka... yeye ndiye kinara bunggeni na ndani ya chama akija majukwaani anahubiri kufuta kofia mbili mbili wakati yeye kavaa tatu tau.

  Huo ni unafiki ambao lazima tuusema tu bila ya kujali mapenzi ya chama...........
   
 8. Imany John

  Imany John Verified User

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Ccm hailiki hata ikapakwa blue band
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  raisi atoke mahali popote ni sahihi hata mgombea binafsi lakini kusema asitoke kwenye vyama vya siasa hiyo itakuwa kubinya demokrasia.......................maendeleo ina maelezo mengi ya ndani na nje........kama raia wa utamaduni wa kubeza kazi hakuna maendeleo.....nasiye tukiri tu wavivu sana ....pita mji wowoteule angalia watu walivyofurika barabarani wengi wao hawataki kazi ..................... MziziMkavu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Una haki ya kusema hivyo kwa kuwa una maoni kama great thinker, binafsi naamini hawajahi kupitisha Rais asiye bora kwa mitazamo yao.....na hao marais bora wao ndiyo wameifikisha nchi mahala hapa.....kwasababu wameshindwa binafsi naona ni heri tuwajaribishe watu wengine kwasababu....wanaweza wakafeli au kufaulu, tofauti na CCM ambayo tayari tumekuwa na uhakika wa wao kufeli miaka yoote.

  Madhaifu machache ya Vyama vya Upinzani haya halalishi udhaifu mkubwa wa CCM. Hivi kweli hii ni nchi kweli Rais wa nchi anawataka watu walioiba Mabilioni ya Shiringi wayarudishe bila adhabu na hakuna ripoti itolewayo kama wanarudisha au la na kama wamerudisha ni kwa kiasi gani.

  Rutashubanyuma
  mimi na dream CCM iondoke madarakani tuwape nafasi watu wengine nao wakishindwa basi niamini na ku-conclude kwamba Tanzania tuna Tatizo la Human resources. Nichukua uraia wa Rwanda.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Filipo,

  Viongozi hawapaswi kutenguliwa na vikao ambavyo havikuwachagua.........kama viongozi wa matatazo basi tuulizwe siye na wala siyo kamati Kuu ya Chadema ambayo hakuna hata mpigakura wetu kule........wa jiji la Arusha..........hiyo ndiyo misingi ya demokrasia.... haiwezekani wakaazi wa nje ya jiji la Arusha watuchagulie nani anafaa kutuongoza huo ni uwakilisha haramu tu...... usiutetee...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Labda wagombea watokee mbinguni!
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rutashubanyuma,

  Pamoja na yote hayo unayoyasema lakini kwa sasa C.C.M. imezeeka tunataka chama kingine chochote kije kitawale mkuu hatupo sisi Urusi tupo Afrika Mashariki hatupo Zimbambwe tupo Tanzania Mkuu tunataka mabadiliko na Maendeleo C.C.M. tangu iundwe sasa yapata miaka 35 hakuna Maendeleo yoyote yale Chama cha C.C.M kimesha pitwa na wakati tungoje chama kingine Tuyavue Mkuu Magamba tuvae People in Power Mkuu kila lilio na Mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Waswahili wamesema Ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka C.C.M hu ndio mwisho wao imekalia kuti kavu mkuu samahani kama nitakukwaza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Ezan sijasema marasis wa CCM waliotangulia walikuwa bora ila sasa wanayo nafasi ya kutupatia raisi bora kama watapanua wigo la demokrasia.......ungelikuwa umenielewa ungelifahamu hao wote waliotangulia walikuwa ni bomu kwa sababu wanachama wa kawaida wa ccm hawakushiriki katika kuchagua kiongozi bora...
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Hawezi Rais Bora kutoka tena C.C.M. You Forget it. Tunataka Rais atoke sehemu yoyote ile sio tena Rais atoke C.C.M imesha zeeka Mkuu ................................ Rutashubanyuma
   
 16. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ulichosema ni kwamba CCM inajukumu hilo, hukusema wana nafasi ya kutupatia Rais bora kama ni suala la nafasi kila chama kina nafasi, ila kwasababu CCM imepewa hiyo nafasi miaka mingi na haijaitumia vizuri uwezekano wa kupewa nafasi hiyo tena ni mdogo sana watu tupo tayari ku-take risk kwa chama kingine hata TLP
   
 17. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sikubaliani asilani na hoja za Watanzania wengi wenye uoga wa kubadili mfumo wa utawala kwa maelezo chapwa eti heri tuendelee na wezi hawa hawa tuliowazoea (Chama Cha Magamba) kuliko kuleta wezi wapya wa Upinzani. Astaghfilullah!! Hivi ndo kusema wizi ni sifa kuu ya Watanzania? Kwamba kila anayeingia madartakani lazima aibe?

  Kama hivi ndivyo bado tunadhani ipo haja ya kuwabadili 'wezi' kwa sababu wapinzani wana sera ya kuunda serikali ndogo na hivyo kupunguza mianya ya wizi kuliko hawa Chama Cha Magamba ambao ukubwa wa serikali hauelezeki maana wapo viongozi rasmi na wasio rasmi. Wasio rasmi ni kama watoto, mashemeji, vidosho, mabest, makada, nyumba mbhoke.......Na woote hawa ni wezi kama alivyobainisha Rutashubanyuma
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  wengine tunaamini katika mfumo wa kidicteta ndugu yangu, na katika hili ninaamini kwamba mfumo wa kimocrasia sisi tumerukia gari kwa mbele, mfumo wa kidemocrasia unaambatana na elimu, ni katika jamii zilizoelimika pekee ambako asilimia kubwa ya wananchi wanafanya rational decisions ndiko wanakofaidika na mfumo wa kidemocrasia.

  Moja ya tatizo la democrasia ni kama ulilolionyesha wewe, kwamba umefumbia macho matatizo yoooote ambayo CCM imelifikisha Taifa letu na kuangalia weaknesses za kuhesabu za wapinzani kisha umeamua kwamba CCM ni bora zaidi ya wapinzani, katika hili umejiweka kundi moja na wale wanaofanya maamuzi baada ya kula wali na kugombania kanga.
   
 19. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Rutashubanyuma WAGAISA,chonka wagaima omugusha!

  • :clap2:
  ,
   
 20. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Sasa nimshagundua nini maana ya kuwa na mgombea binafsi!
   
Loading...