Amini usiamini babu seya papi kocha huenda wakaachiwa hivi karibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amini usiamini babu seya papi kocha huenda wakaachiwa hivi karibuni

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jun 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  BABUSEYA.jpg Mungu kwa ukubwa wake anaendelea kumpigania galacha wa muziki wa dansi nchini, Mfalme Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, jitihada zao zinapata mafanikio na taarifa rasmi ni kwamba hivi karibuni watatinga mahakamani tena, kusaka uwezekano wa kuwa huru.

  Babu Seya na Papii, wanasubiri taarifa ya msajili wa Mahakama ya Rufaa, itakayowajulisha tarehe ya kuanza mapitio ya hukumu yao, lengo likiwa kutafuta ufumbuzi wa vifungu vinavyodaiwa kuwa na kasoro wakati wa hukumu ya mara ya mwisho.

  The Quality Paper, Ijumaa linakuwa la kwanza kuandika kwamba ombi la mawakili wa upande wa utetezi linaloongozwa na mwanasheria mkongwe, Mabere Nyaucho Marando la kutaka hukumu hiyo ipitiwe upya, limekubaliwa na kinachosubiriwa ni parapanda kulia.

  Kwa mujibu wa mtoto wa Babu Seya, Mbangu Nguza ‘Mashine’, kila kitu kipo sawa na kinachosubiriwa ni taarifa ya msajili wa Mahakama ya Rufaa.

  Nguza Mashine aliliambia Ijumaa juzi (Jumatano) kuwa anamshukuru Mungu kwa kuendelea kuipigania familia yao ndiyo maana kila mara wanapowasilisha ombi mahakamani linakubaliwa.
  Mbangu alisema: “Kila kitu kinakwenda vizuri, nina imani kubwa na mahakama, kwahiyo tumaini langu ni kwamba mapitio ya hukumu yatakuwa mazuri.”

  Mtoto huyo wa Babu Seya alisema, mfumo wa mahakama nchini upo huru na haki ndiyo maana tangu mwaka 2003, wamekuwa wakibisha hodi mahakamani mara kwa mara na shauri lao kukubaliwa na kusikilizwa hatua kwa hatua.

  Aliendelea kusema, baada ya hukumu iliyopita, Marando aliona vipengele vitatu vinavyohitaji kupitiwa upya, pia akawashirikisha mawakili wenzake wanne ambao nao walibaini vipengele vitatu ambavyo wanaamini vina upungufu kisheria.

  “Baada ya kuona vipengele hivyo, moja kwa moja akaviwakilisha kwa Jaji Mkuu (Augustine Ramadhan), akaomba hukumu ipitiwe upya chini ya majaji saba,” alisema Mbangu na kuongeza:
  “Bila shaka safari hii mapitio ya kesi yetu yatafanywa na majaji saba. Kila kitu kinakwenda sawa.

  Tunamshukuru Mungu kwa kuwezesha hatua hii, pia tunazidi kumuomba atende miujiza.”
  February 11, 2010, Mahakama ya Rufaa iliendelea kuwatia hatiani Babu Seya na Papii na kuwaachia watoto wawili wa mwanamuziki huyo, Mbangu na Francis Nguza ‘Chichi’.

  Mbangu na Chichi, walionekana hawana hatia katika kesi ya msingi waliyofunguliwa ya kubaka na kulawiti watoto 10.

  Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.

  Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru Mbangu na Chichi Februari 2010.
  Kwa habari na picha zaidi tembelea mtandao wa www.globalpublisherstz.com

  IKIWA KAMA NI KWELI JE HAKI ITAKUWA IMETENDEKA HAPO KWETU BONGO? AU NDIYO TUSEMSE KWENYE PESA MPISHE APITE. MWENYE PESA HUWA HAFUNGWI JELA?

  [​IMG]<!--n--><!--m-->[​IMG]<!--n--><!--m-->[​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]<!--n--><!--m-->[​IMG]<!--n--><!--m-->[​IMG]
  [​IMG]
   
 2. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Haiingii akilini hii kitu, wamefikia wapi?
   
 3. b

  batadume Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  duuu ina sikitisha sana wadau.....................
   
 4. M

  Magwira JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bwana wee! Wacha watoke.Mungu awasimame kama anavyowasimama Mafisadi.
   
Loading...