Amini Usiamini Atafuta Mtu wa Kufariki Naye Kwenye Internet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amini Usiamini Atafuta Mtu wa Kufariki Naye Kwenye Internet

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Sep 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Friday, September 24, 2010 1:17 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ambaye alitangaza kwenye internet kuwa anatafuta mtu wa kufariki naye, amekutwa amefariki ndani ya gari pamoja na mwanaume aliyejitolea kufariki naye. Katika tukio hilo lililotokea jumanne, maiti za Joanne Lee na Steve Lumb zilikutwa kwenye gari ambalo lilikuwa limeegeshwa pembeni ya barabara huku likiwa limebandikwa vipeperushi vinavyowaonya watu wasilifungue gari hilo.

  Taarifa ya polisi ilisema kuwa Joanne na Steve walifahamiana siku ya jumatatu kwenye internet na siku hiyo hiyo walikubaliana kujiua kwa pamoja na siku hiyo hiyo walijiua.

  Joanne na Steve walijiua kwa kujifungia ndani ya gari ambalo ndani yake walilijaza gesi ya sumu.

  Taarifa zaidi zilisema kuwa Joanne Lee alijitangaza kwenye internet kuwa anataka kujiua lakini hana ujasiri wa kujiua mwenyewe hivyo anatafuta mtu wa kujiua naye.

  "Sina ujasiri wa kujiua peke yangu sijui la kufanya, natafuta mtu wa kujiua pamoja nami, vifaa vyote vitakavyohitajika kwaajili ya kujiua mimi nitajitolea", alisema Joanne mwenye umri wa miaka 34.

  Dereva wa lori, Steve Lumb alijibu ujumbe wa Joanne na kuamua kusafiri umbali wa kilomita 320 ili akutane na Joanne.

  Miili ya Joanne na Steve ilikutwa ndani ya gari ambalo lilikuwa limejazwa gesi za kikemikali.

  Mume wa Joanne akiongelea kifo cha mkewe alisema kuwa alikuwa hana habari yoyote kama mkewe alikuwa na mpango wa kujiua mwenyewe.

  Majirani wa Joanne walisema kuwa Joanne alikuwa akijikondesha sana kwa kujinyima chakula kiasi cha kwamba alikuwa dhoofu sana.

  Polisi wanaendelea na uchunguzi wa vifo hivyo.
  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  :sad::sad::sad::sad:
   
 3. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  life rolls
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Oct 16, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kazi Kweli kweli.
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :mmph:
   
Loading...