Amina Chifupa kupokea vitisho na hatimae kufariki. COINCIDENCE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amina Chifupa kupokea vitisho na hatimae kufariki. COINCIDENCE?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Azipa, Jul 11, 2012.

 1. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Chifupa atishiwa kuuawa
  2006-11-16 09:03:34
  Na Rosemary Mirondo na Beatrice Philemon

  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Amina Chifupa, ametishiwa kuuawa na watu wasiojulikana kupitia simu yake ya mkononi.
  Madai ya mbunge huyu aliyatoa jana alipozungumza na waandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka Dodoma alikokuwa akihudhuria kikao cha Bunge kilichomalizika jana. Alisema amepokea vitisho kupitia vijikaratasi alivyoandikiwa akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge, vikimuonya aachane na suala la wauza unga.

  ''Sambamba na ujumbe huo, kupitia simu yangu ya mkononi nilitumiwa ujumbe mfupi wa maneno wa kunitishia kuniua.'' Mbali na hayo, ndani ya ukumbi wa Bunge kwenyewe nimepokea ujumbe wa vikaratasi visivyo na majina vikisema kwamba ninajifanya najua kuongea'', aliongeza kusema mbunge huyo ambaye alisisitiza bado hatetereki kwa vitisho hivyo.

  Ujumbe mwingine unasema "we Amina wewe acha wewe, usijifanye unajua sana, ukiwa kwenye jumba la vioo usirushe mawe wakati na wewe umo ndani, tunaanza kukuchunguza kuanzia leo unapata wapi pesa, ni SISI USALAMA WA TAIFA Hivi wewe Amina unajiona wewe ni msafi sana? Au kwa kuwa sisi tumekaa kimya. Wewe ni mchafu sana , na sisi tukiamua kuanza kukuchafua hapatakalika hapa. Dawa yako iko jikoni inachemka, ndio utajua sisi ni nani umeyataka mwenyewe usimlaumu mtu. Wameshindwa wakongwe wewe mtoto wa juzi.

  Aidha Bi.Amina alipigiwa simu inayoonyesha kutoka nje ambayo ilisomeka call kwenye simu yake yenye matusi ya nguoni yakimuonya aache kuropoka. Vitisho dhidi ya mbunge huyu jasiri na chipukizi, vimekuja siku moja tu baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai nchini, Bw.Robert Manumba kuahidi kuwa Jeshi la Polisi litamlinda na lipo tayari kupokea taarifa zinazohusu vinara wa uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini.

  Aidha, Bi. Amina alisema amepokea simu kutoka kwa mtu aliyejitaja kuwa ni polisi, akimuonya asiongee na mtu yeyote kuhusu suala hilo, mpaka atakapotoka bungeni na kumshauri mara atakapotoka Dodoma aende moja kwa moja kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Bw. Robert Manumba, kuonana naye.

  Hata hivyo, Bi. Amina hakutaka kutaja jina la polisi huyo. Bi. Amina alisema pamoja na kupokea vitisho hivyo, hataacha kufichua wafanyabiashara hao kwa sababu wanachangia kuwaangamiza vijana ambao ni taifa la kesho.

  Alisema baada ya kutangaza bungeni kuwa yupo tayari kuwafichua vigogo wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, ameanza kupata ushirikiano kutoka kwa wabunge wachache wanaochukizwa na biashara hiyo.

  Nipashe ilipoongea na Kamishna Manumba jana kuhusu vitisho anavyopokea Mbunge huyo, alisema yeye hajapata taarifa zozote mbali na kusema kuwa suala hilo linahitaji kushughulikiwa kitaalamu.

  Hata hivyo, alisema kwa sasa anaweza kuwasiliana na kituo cha polisi Dodoma au kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya. "Pamoja na ujasiri wa Mbunge huyo, pia tunahitaji watu wengine wajitokeze kutoa majina ya wafanyabiashara hao ili tuweze kutokomeza biashara hiyo inayoleta madhara nchini," alisema Bw. Manumba.

  Kamishna Manumba alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na biashara hiyo nchini, unahitajika ushirikiano kutoka serikalini na watu binafsi kwani suala hilo litashughulikiwa kwa siri kwa ajili ya kuwalinda watoa taarifa. "Serikali ishirikiane kupiga vita suala hilo kisiasa na sisi tutalishughulikia kitaaluma," alisema Kamishna Manumba.

  Alisema hilo ni tatizo la kimataifa hivyo inakuwa ni vugumu kuwabaini vigogo halisi wanaohusika na kilimo na kutengeneza madawa hayo kwani hapa nchini wanaohusika na madawa ya kulevya ni mawakala. Alisema kuwa wazalishaji wakubwa wapo nchi za nje kama Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, Latin America na Afghanstan.

  Aliongeza kuwa kama serikali za nchi za Afrika na Bara la Ulaya zitakuwa imara, vyombo vya serikali vitaweza kufanyakazi zake vizuri katika kuweka mikakati ya kupambana hatimaye kupunguza tatizo hilo la madawa ya kulevya.

  Hata hivyo, Kamishna Manumba alisema kuwa hadi sasa hawajapata ushahidi unaoonyesha kwamba vigogo wanaotoka serikalini au taasisi wanashiriki katika uuzaji wa dawa za kulevya ila wamebaini kuwa kuna wafanyabiashara wakubwa ndio wanaoongoza kuingiza madawa ya kulevya nchini kama mawakala.


  SOURCE:
  Nipashe
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  UKIMWI

  Na Mwendapole alitishwa?
   
 3. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hatuwezi kujua tunakokwenda kama hatujui tunakotoka
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  stick to the point! Mtu anatishiwa na usalama wa taifa halafu anakufa kifo cha ajabu.Crazy govt invòlved!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi kila siku Serikali za dunia zinatangaza kuwa UKIMWI unaua, unatisha. Bado huoni wala husikii na wala hujui kuwa Amina na Mumewe Mpondamali walikufa kwa UKIMWI?

  Nini mnachotaka kukificha au kujidai hamjui?
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hivi mume wake bado yupo?
   
 7. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  come to your senses
   
 8. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Alinyonyoka nywele na kubabuka ngozi wafukue mwili wapime mifupa nina mashaka...............................................
   
 9. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  quote frm dci Manumba "jeshi la polisi litamlinda" how comes alikufa ktk mazingira km yale?mikono ya serikali hii inanuka damu za watu.
   
 10. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  nae ashafariki ktk mazingira ya ajabu ajabu,wameacha watoto wadogo wasiokuwa na baba wala mama.
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Rip amina
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Muanzisha hii thread umeleta thread ili ufananishe na kutishiwa kuuwawa kwa Slaa, na Mnyika...Amin alifariki kwa maradhi ya kibinadamu wala hakuwawa.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Go search for yours it seems you have lost them.
   
 14. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  mizimu ya mauaji yanaizonga sana ccm. Sokoine....Kolimba....Amina....nk
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Na ngoz ya mwakyembe je????
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Mtu anaweza kuumwa malaria akadungwa sindano yenye virusi vya ukimwi makusudi ili aonekane amekufa kio cha kawaida.
   
 17. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Aids? Sure? Thibitisha with documents.Are u a doctor?
   
 18. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ritz, binafsi sijui kama aliuawa ama la, ila naelewa kuna maradhi ya 'kibinadamu' yanayosababishwa na binadamu kwa kusudi la kuua bila kuchochea udadisi.
  Say Renal failure sababu ya sumu labda (kumbuka, inaweza kuwa na sababu zingine za kibinadamu) au hata wale wanaosema UKIMWI, coz basically ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini, ambapo kuna several causes to this as well za 'kibinadamu', lakini pia sumu inayoweza kuathiri sehemu seli za mwili zinapotengenezwa (bone marrow) ikiwa moja wapo. Hapa mtu hupata upungufu wa kinga na dalili zote ambazo zinahusika nao.

  Kwa hiyo basi unaweza kuuwawa kitaalamu kwa kupewa kitu kinachoweza kusababisha maradhi ambayo bila uchunguzi wa kutosha, hasa katika mazingira kama yetu (yasiyo na vipimo mahsusi na yaliyojawa na magonjwa yanayodhaniwa kuwa ya 'kawaida kwa watu fulani') huonekana ni 'matatizo ya kibinadamu' na hivyo kufifisha udadisi zaidi.

   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna dokta duniani anaetoa habari za mgonjwa wake akiwa na magonjwa ya aibu ila tu, hajambo, kafa, anaumwa sana.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi.

  Dokta, Lema na Mnyika mmesha wapima?
   
Loading...