Jana jioni iliingia sms kwa simu yangu, "tafadhali nipigie..". Nikajua labda ni mtu anayenifahamu, nikapiga. Ilipopokelewa tu swali la kwanza, "wewe nani?" Nikawa mkali kidogo maana yeye kama hanifahamu alinitumiaje sms ya please call me?. Baadaye huyo mdada akazuga zuga weeeee, hatimaye akajitambulisha. Tulihitimisha maongezi kwa yeye kusema basi samahani nimekosea namba.
Baadaye kidogo, ikaingia sms, "tafadhali niongezee hela..". Wakati huo niko home napata msosi, Nikaangalia tuu ile sms, nikapotezea. Mara ikaingia tena mara ya pili.... Nikapotezea, ikaingia tena sms ya tatu. Nikahamaki mweee! Uvumilivu ukanishinda, nikamjibu tu "Sawa nitakutumia. Ila kama ilivyoandikwa kwenye noti, fedha halali kwa malipo ya shilingi elfu ......, na wewe uniambie kwa kazi gani halali uliyonifanyia nikuongezee hela?"
Hebu fikiria, mtu hata humjui, humfahamu, hata yuko mkoa au nchi gani hujui alafu umtumie vocha. Jamani dunia tambara bovu kweli aisee.