Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Polisi nchini Kenya kaunti ya Bungoma, wanamzuilia mama aliyemfungia mwanae ndani ya gari na kumuacha akafa huku akijiburudisha na mpenzi kwenye gesti.
Mwanamke huyo yasemekana kuwa, alimfungia ndani ya gari mwanawe wa miaka minane na kwenda 'kurusha roho' na mpenzi wake wa pembeni katika lojing'i iliyo karibu na eneo la Bumula.
Chifu wa lokesheni ya Mateka, Bw Julius Barasa aliwaambia wanahabari kwamba mshukiwa, Bi Christine Nasimiyu kutoka Kijiji cha Mabusi, alikuwa amekodisha chumba ili akajistareheshe.
Alimwacha mtoto ndani ya gari na kufunga vioo vyote, jambo linalokisiwa kusababisha kukosekana kwa hewa safi na kumfanya aage dunia.
"Walimwacha akiwa na chupa tatu za soda ili naye pia ajiburudishe. Lakini mtoto alifariki kwa kukosa hewa safi", alieleza Bw Barasa.
Tukio hilo lilifanyika nje ya baa ya Mareba, soko la Mateka na kuwakasilisha wakazi, ambao walitaka kuwashambulia wapenzi hao wawili lakini wakaokolewa na polisi.
Wapenzi hao walitiwa nguvuni na kuzuiliwa katika kituo cha Bumula huku mwili wa mtoto ukipelekwa katika mochari ya Hospitali ya rufaa ya Bungoma.
"Hii inashangaza na ni makosa, tumepoteza mtoto kwa sababu ya uhusiano wa kutojali", alisema Bw Lupao.
Chanzo: TaifaLeo