Amezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili kumchunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,672
2,000

Nyoka wa Anaconda hupatikana zaidi katika msitu wa Amazon

Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.

Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.

Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.

Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la Nyoka huyo.

Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya kushindwa na kusalimu amri
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.

Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.

Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''

''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''

Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa anaumizwa.

''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.

Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa tatu.

Chanzo:BBC
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,044
2,000
''Nahisi kama mifupa
yangu inasagwa sagwa,
njooni mniondoe
hapa.'' alisema Paul.
:::::''
chezea chatu wewe?
nadhani vazi lilijaa mavi hahaha
 

Githeri

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
814
500
Alitolewaje humo tumboni Mwa Anaconda ? Huyo Anaconda aliuawa? Mhhh!! Utafiti mwingine!!!
 

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
14,945
2,000
Hii stori sivo. Paul ni mwana mazingira ambaye anajihusisha kuhifadhi mazingira ya Amazon forest. Kituko cha kumezwa na Anaconda kimelenga kuchochea uhifadhi wa mazingira ya misitu ya Amazon na siyo utafiti ya maumbile ya Anaconda.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,642
2,000
Kwahiyo wametunga story! Ndio maana mwisho wake haueleweki, yaani alitolewa/okolewa vipi.
Ngoja nikupe kwa ufupi mwisho wake ulikuwaje.

Baada ya joka kujivingirisha kwenye mwili wake kwa takribani saa zima likapanua mdomo wake na kutaka kuanza mchakato wa kumeza.

Lakini, nadhani ingekuwa ni vigumu sana jamaa kumezwa kwa sababu ya mabega. Licha ya hivyo, huo mchakato wa kumeza huwa ni wa taratibu sana huku joka likuwa bado limejivingirisha.

Kwa hiyo, kilichotokea ni kwamba baada ya kuwekwa kwenye kabali na hilo joka kwa karibu saa zima, jamaa alianza kusikia mkono wake kama unakufa ganzi/ kuvunjika ndipo alipo 'tap out' (alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na wenzake waliokuwepo mita chache kwa umbali) na jamaa zake wakaenda wakalitoa hilo joka.

Hata kichwa cha jamaa kilikuwa bado hakijaingia mdomoni mwa hilo li anaconda. Walipolitoa kutoka kwenye mwili wa jamaa wakaliachia likarudi zake msituni na jamaa wakamcheki kuona kama mkono wake na afya yake iko salama.

Hivyo ndivyo kipindi kilivyoishia. Hivyo, kusema kwamba alimezwa na anaconda ni kupotosha ingawa najua mwanzoni kabla ya kukirusha walikinadi hicho kipindi kwa kusema 'eaten alive' ili kuvutia watazamaji wengi, kama sijakosea.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,642
2,000
Inaelekea nawe ni mpenzi wa Discovery channel.
Oh yeah, mi ni devotee wa Discovery, A&E, na HGTV (kile kipindi chao cha House Hunters International nakipenda sana).

Vipi, hukuangalia Eaten Alive jana?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
101,868
2,000
Niliangalia kiasi, nimeyafahamu mambo mengi sana ya wanyama mbali mbali duniani kupitia Discovery channel.

Oh yeah, mi ni devotee wa Discovery, A&E, na HGTV (kile kipindi chao cha House Hunters International nakipenda sana).

Vipi, hukuangalia Eaten Alive jana?
 

kahtaan

JF-Expert Member
Jul 11, 2009
17,627
2,000
Oh yeah, mi ni devotee wa Discovery, A&E, na HGTV (kile kipindi chao cha House Hunters International nakipenda sana).

Vipi, hukuangalia Eaten Alive jana?
Nyie ndio wale Mkiijiwa na tapeli akadai kuwa yeye ni Scientists basi mnaolewa bila mahari!

Sasa we unadhani Kujiita Devotee wa Discovery channel ni Ujanja!

Ovyoooo! We kabebe box huko acha kuiga iga watu unao waabudu. Utapoteza Utu wako bure!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom