Ameuteka Moyo Wangu!!!!

BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,371
3,699
Huyu kaka nafanya nae kazi ametokea kweli kuuteka moyo wangu, sidhani kama anaelewa hilo ila ninaongea nae kama marafiki wa kawaida. Yani sijawahi kujisikia kama hivi kwa mwanaume mwingine.
So far nimevutiwa nae kwa jinsi alivyo pia hobbies zetu zinaendana. Ni kaka mcheshi, mkarimu, anavaa vizuri&smart(sidhani kama ni mzaire yani anang'aa nje ya nyumba tu).
Sijui kama yupo ''attached'' japo hajaoa kutokana na maongezi tunayokuwa nayo.
Je nimwambie ukweli? au atanifikiriaje?Nitaanzaje?Au nimsubiri azisome hisia?how?

NB: Nipo serious mana naamini hisia zangu za nguvu, namuwazia kuwa baba wa watoto wangu tukijaliwa kuwa wote:)))
 
Mu-sir

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,621
1,621
Hizi ni zama za ukweli na uwazi kama ni understanding atakuelewa tu ukimweleza hisia zako lakini uwe makini asije kukuona kicheche.
 
Fab

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
762
14
vunja ukimyaaa!...'mtokee'....au tukupe mistari???hahahahah
 
Dena Amsi

R I P
Aug 17, 2010
13,084
4,220
Mweleze tu BJ unaogopa nini akikuona mcharuko poa tu lakini roho yako itatulia unajua ukisema ukweli unatoa dukuduku moyoni linalokutesa
 
BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,371
3,699
Hizi ni zama za ukweli na uwazi kama ni understanding atakuelewa tu ukimweleza hisia zako lakini uwe makini asije kukuona kicheche.

Kweli kabisa, mi mwenyewe naamini mtu ukiwa na hisia juu ya mtu unamwambia ili uwe free ila akinifikiria hivyo je na mimi ni mwanamke?! Inabidi niwe na kifua kweli kweli cha kumwambia.
 
seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
Huyu kaka nafanya nae kazi ametokea kweli kuuteka moyo wangu, sidhani kama anaelewa hilo ila ninaongea nae kama marafiki wa kawaida. Yani sijawahi kujisikia kama hivi kwa mwanaume mwingine.
So far nimevutiwa nae kwa jinsi alivyo pia hobbies zetu zinaendana. Ni kaka mcheshi, mkarimu, anavaa vizuri&smart(sidhani kama ni mzaire yani anang'aa nje ya nyumba tu).
Sijui kama yupo ''attached'' japo hajaoa kutokana na maongezi tunayokuwa nayo.
Je nimwambie ukweli? au atanifikiriaje?Nitaanzaje?Au nimsubiri azisome hisia?how?

NB: Nipo serious mana naamini hisia zangu za nguvu, namuwazia kuwa baba wa watoto wangu tukijaliwa kuwa wote:)))

Duh, hapo kwenye red inayonyesha unalo jibu tayari, uko serious, unaamini hisia zako na tayari umeshaenda mpaka kuwaza habari za watoto....yaani watoto si ni mapenzi ya Mungu. What if hutawapata, je utamchukia huyo ambaye sasa hivi unamfia....mmmmhhhhhh patience, wisdom, prayer....dada haraka haraka zitakupeleka kubaya. Upendo wa kweli hauna speed hiyo yako. Ila nahushangaa unauliza wakti unasema unaamini hisia zako, basi mwambie ila akisema yuko booked tayari angali isije ikawa sasa ni kulia na kupata hysteria, ita-affect kazi yako...ndio maana ni vizuri kuwa na busara na kwenda slow....
 
The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,607
5,966
BJ Acha kuugulia moyoni hebu tema hizo lyrics kusudi mauzo ya singo yaende platinum
 
mfarisayo

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
5,160
2,001
Tafuta mahali na muda muafaka umueleze ukweli atakuelewa tu, ukishindwa tumia njia nyingine za indirect kama kuwa naye close mara nyingi sio tu ofisini bali hata siku za weekend tafuta jinsi ya kukutana naye, pia tumia vizuri mawasiliano ya simu baada ya muda wa kazi kumuandikia sms kumjulia hali yake na mambo mengine ya kawaida atakusoma tu baadae.
 
Edgartz

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
241
20
We mweleze 2 ila tatizo la sisi vidume hata akiwa na mpenzi mtalajiwa hawezi kukueleza zaidi atataka ukumege mchezo uishe uwe makini kwa hilo angalia kwanza msimaso wake!
 
cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
492
nakushauri usimwambie!
kama anakuhitaji atakwambia sbb lazima tu kuna vidalili umemuonesha!
kumuanza mwanaume ni big no nooo hamna cha zama za uwazi wala cha nini nioneni mshamba tu lkn huo ni mtazamo wangu!
wengine hata kama alikua anapanga jinsi ya kukuanza ukimtongoza tu unamkata stimu zote.
anyway Belinda huu ni ushauri tu wewe ndio utakayeamua upi wa kufuata na upi wa kupotezea ila nakutakia kila la kheri!
 
BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,371
3,699
Mweleze tu BJ unaogopa nini akikuona mcharuko poa tu lakini roho yako itatulia unajua ukisema ukweli unatoa dukuduku moyoni linalokutesa

Dena Amsi nina wakati mgumu sana..ipi bora kumtext au live? au nifanye viji-actions kama kutoka wote anaweza kuwa connected na yeye?
 
Zneba

Senior Member
May 12, 2010
192
7
mwaya usimueleze jikaze tu ila kuwa nae karibu ili ujue nae anahisia zozote na ww au,unajua siku hizi wanawake tumekuwa warahisi sana unaweza kumueleza akaona nawe ndiyo walewale so avunjike moyo kabisa please jikaze my dear ushauri wa cheusi mangala pia muhim
 
BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,371
3,699
BJ unaogopa kutekwa?
Naogopa mana huyu mtu amezingira kichwa changu.. Niambie ukweli wewe mwanaume ukiambiwa unapendwa unamchukuliaje mwanamke?

Duh, hapo kwenye red inayonyesha unalo jibu tayari, uko serious, unaamini hisia zako na tayari umeshaenda mpaka kuwaza habari za watoto....yaani watoto si ni mapenzi ya Mungu. What if hutawapata, je utamchukia huyo ambaye sasa hivi unamfia....mmmmhhhhhh patience, wisdom, prayer....dada haraka haraka zitakupeleka kubaya. Upendo wa kweli hauna speed hiyo yako. Ila nahushangaa unauliza wakti unasema unaamini hisia zako, basi mwambie ila akisema yuko booked tayari angali isije ikawa sasa ni kulia na kupata hysteria, ita-affect kazi yako...ndio maana ni vizuri kuwa na busara na kwenda slow....

Asante mkuu, kweli mambo mengine ni majaliwa na always tunafikiria kujaliwa..nitaenda polepole japo naziamini hisia zangu!!..nitakuwa mwngalifu kwa utendji wangu kazini ambao mpaka sasa haujatetereka...busara mbele, shukrani za dhati

BJ Acha kuugulia moyoni hebu tema hizo lyrics kusudi mauzo ya singo yaende platinum
Yani natamani ingekuwa rahisi hivyo..au nifanye ile liwalo na liwe!!..hata akisema huyo na mtu ningependa tuendelee marafiki, sijui itawezekana?!! haya najiandaa na singo

Tafuta mahali na muda muafaka umueleze ukweli atakuelewa tu, ukishindwa tumia njia nyingine za indirect kama kuwa naye close mara nyingi sio tu ofisini bali hata siku za weekend tafuta jinsi ya kukutana naye, pia tumia vizuri mawasiliano ya simu baada ya muda wa kazi kumuandikia sms kumjulia hali yake na mambo mengine ya kawaida atakusoma tu baadae.

Sawa Mfarisayo, labda kuwa nae karibu inaweza kumletea automatic hisia juu yangu pia..Haonyeshi kujisikia ila asijekunifuta kwenye ramani ya ubongo wake na kuwa maadui..

mwambie ukweli usiogope
Haya nitajitahidi sana..huenda ikanisaidia kushusha mzigo hata kama mwelekeo sijajua

We mweleze 2 ila tatizo la sisi vidume hata akiwa na mpenzi mtalajiwa hawezi kukueleza zaidi atataka ukumege mchezo uishe uwe makini kwa hilo angalia kwanza msimaso wake!

Usiniambie, kwahiyo anaweza kuona chakula hichoo na kukubali kumbe ana wake? hapo pia pagumu nikiwaza..nitakuwa makini,thanx

Dinner could a good plan there is a way as you go on lazima atajua tu you are interested in him usiogope
Yani acha tu, naona vitendo viongee zaidi ya live ila bado najipanga..akikubali dinner itakuwa walaaah
 
TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
2,199
1,695
Mtoe out usiku, usiongee mengi, kuwa msikivu zaidi, msifie, mwambie unapenda uwe na mtu kama yeye... ataelewa somo
Huyu kaka nafanya nae kazi ametokea kweli kuuteka moyo wangu, sidhani kama anaelewa hilo ila ninaongea nae kama marafiki wa kawaida. Yani sijawahi kujisikia kama hivi kwa mwanaume mwingine.
So far nimevutiwa nae kwa jinsi alivyo pia hobbies zetu zinaendana. Ni kaka mcheshi, mkarimu, anavaa vizuri&smart(sidhani kama ni mzaire yani anang'aa nje ya nyumba tu).
Sijui kama yupo ''attached'' japo hajaoa kutokana na maongezi tunayokuwa nayo.
Je nimwambie ukweli? au atanifikiriaje?Nitaanzaje?Au nimsubiri azisome hisia?how?

NB: Nipo serious mana naamini hisia zangu za nguvu, namuwazia kuwa baba wa watoto wangu tukijaliwa kuwa wote:)))
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom