Ametumia taulo langu kama dekio. Je, anafaa kuwa mke kweli?

Jamani inategemea taulo lilikuwa na rangi gani mengine yanafanana na madekio tuuu. Ukizingatia ni bachela
 
Sasa kama taulo limekomaa kama dekio afanyaje? Sidhani kama lingekua safii+jeupee angeanza kulitumia kama dekio mkuu. Usafi ni muhimu😀 usimtafutie sababu ya kumwacha bure
 
Acha ujinga ungemuonyesha dekio au ungempa dekio yote haya yasingekuwepo kwa mawazo yako finyu
 
Hakufai, ameonesha dharau kubwa sana kudekia taulo la mume mtarajiwa.
Huwezi jua siku nyingine atadekia kitu gani tena muache haraka.
Wanawake ni kweli hampendani aisee

Sasa usikute hilo taulo ni kama la kwangu tangu mwaka 2013 bado lipo
Nunua jingine tu
 
Back
Top Bottom