Ameshaanza kuunga mkono juhudi na kukiri kwamba tuko kwenye right track kuelekea kuwa kama Ulaya

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,623
2,000
Hii likizo ya siku saba inaonekana anaitumia vizuri kujifunza kuelewa nchi yetu sasa hivi iko hali gani baada ya kuiacha miaka mitatu iliyopita. Ndani ya siku moja tu ameshaanza kuunga juhudi za Magufuli kwamba tuko kwenye right track kuelekea kuwa kama ulaya kwa mfano:

1.Kwa mfano amekubali kuwa barabara za mwendo kasi ndizo hata huko ulaya wanatumia kwenye majiji yao. Tofauti tu ni kuwa huko ulaya ziko nyingi. Ameahidi akichaguliwa atazijenga nyingi jijini DSM. Ambacho hajajua ni kwamba JPM alishaanza kuzijenga nyingi tu jijini DSM.

2. Ameahidi pia akichaguliwa atajenga pia reli za jijini (city railways) na city ferries. Ambacho hajajua ni kuwa tayari JPM tayari alishajenga na anaendelea kujenga hizo city railways and ferries. Ingefaa katika kipindi hiki cha likizo wampeleke akazione pia.

3. Ameahidi pia kuwa atabomoa nyumba kadhaa jijini DSM ili kujenga maeneo ya kupumuzikia (city gardens) na kuegesha magari (parking areas) kama ilivyo huko ulaya. Ambacho hajajua ni kwamba JPM tayari alishaanza kufanya kazi hiyo. Aende akatembelee maeneo hayo ambayo yako tayari.

4. Alipotembelea soko la Kariakoo amejifunza kuwa hizo utitiri wa kodi alizokuwa akizilalamikia kwenye kampeni zake hazikuwa za kweli. Amejifunza kuwa mfanya biashara mkubwa (mwenye mtaji unaozidi millioni 20) kodi anayotakiwa kukusanya ni VAT tu ambayo kiwango chake huwekwa na bunge. Mfanya biashara wa kati ambaye mtaji wake ni kuanzia milioni 4 hadi ishirini kodi yake haizidi milioni 5 kwa mwaka na hukokotolewa kutokana na risiti za mauzo yake na mashine za kielekitroniki anazopewa bure na TRA.

Mfanyabiashara mdogo aka machinga ambaye mtaji wake hauzidi shilingi millioni 4 yeye hulipa gharama ya kitambulisho tu cha shillingi elfu 20 kwa mwaka. Hii wala siyo kodi bali ni gharama ya kuchapisha kitambulisho hicho. Mfanyabiashara wa aina hiyo ni kama yule dada aliyemuuzia yale maparachichi ambaye alikuwa na furaha tele kutokana na kitambulisho hicho. Anamshangaa anapokilalamikia kwenye kampeni zake.

5. Alipokuwa ndani ya bus la mwendokasi amejifunza kuwa watanzania wanaishi kwa raha na uhuru tele. Hawamuogopi mtu ye yote hadi wale dada walimuchukulia kama cerebity tu na wakaenda kukaa kuchat naye na kupiga selfie. Mke wake itakuwa roho ilimuuma. Huko ulaya hakuna kitu cha namna hiyo. Ukiingia kwenye basi hawasemazani, unasoma gazeti au kitabu tu. Halafu wanasema eti nchi yetu haina furaha eti wao ndiyo wenye furaha, nonsense.

6. Amekubali kuwa ile barabara yetu ya njia 8 hadi 12 ya kutoka Dar hadi Kibaha ni nzuri na kubwa sana ambayo hata huko ulaya hawana.

Hivyo kwa muda mfupi sana baada ya kuona machache sana yaliyofanywa na JPM katika kipindi cha miaka 3 aliyokuwa hayupo nchini, ni wazi kwamba ameshaanza kuunga juhudi. Ameshaanza kukiri maemdeleo ya vitu na kuanza kuahidi kuwa na yeye akichaguliwa atajenga mavitu. Hii likizo ya lazima aliyopewa ni blessing kwake.

 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
52,927
2,000
City Ferries? Mv Dar Es Salaam. What a shame?
MAGUFULI alinunua chombo hiki kwa gharama kubwa Sana na kukikizindua kwa mbwembwe, siku ya uzinduzi kilitumia masaa nane kutoka Dar Es Salaam Hadi Bagamoyo.
Kwa aibu akawapa Jeshi ili tusihoji.
Tunaposema MAGUFULI ni baba wa matumizi mabaya ya fedha za wananchi, fisadi na anayelitia hasara Taifa muwe mnatuelewa.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,060
2,000
Lissu hajui kuwa kuna usafiri wa reli jijini? Maskini Lissu iko ya TRC na ya Tazara

Yaani hajui vitu kibao eti anataka kuwa Rais Dar tu hajui kama kuna treni za abiria jijini huyu Mbelgiji anajua ya Ubelgiji kuliko ya Dar anapoishi
 

MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
488
500
Tuache kwanza kupiga kelele ndani yetu kuwa tunashinda, tunashinda, bali tunyamaze ili tusikie kelele za walioko nje yetu, ni :-

Je, zina vyanzo vingi kuliko zetu?

Na kama kuko kimya je wametuhakikishia kushindwa kwa kunyamaza?

Je, kelele za upande wetu ni zetu sisi tu, hazina wageni warudio kwao?

Je, humu tuliwaambia waje tu wa upande wetu tu?

Na tunautambua vipi Ukimya wa watu wale wasioenda kokote kwenye makutano? Wana uwingi gani?

Tulikasanya mamilion au maelfu elfu tu!

October 28.2020 -
November 05, 2020.
 

Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
1,118
2,000
Magufuli ni muharibifu tu wa pesa za Umma, mwizi na fisadi hawezi kuliendeleza Jiji kwa namna yoyote ile.

Magufuli alipokua Waziri aliiba pesa za MV Bagamoyo - Dar. Akaleta meli mbovu.
Magufuli na MaCCM yote hayajawahi kuitakia mema nchi yetu.
 

DURACEF

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
755
1,000
Kaa kwa kutulia....uhalisia ndio ndio utaamua nani ashinde...kama ni Rais Magufuli au Mh TAL.
Usichoshe watu kwa sababu huna jipya.
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,341
2,000
Hivi kuna mtu bado anafikiria Lisu atashinda kweli? Yeye mwenyewe anawashangaa wanaowaza hivyo.

Mmemuona anavyoenjoy mwendokasi, na bado kuna mengi atayaona na ajue hizo ndio kazi za CCM.

October 28 kura zote ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,118
2,000
Hivi kuna mtu bado anafikiria Lisu atashinda kweli? Yeye mwenyewe anawashangaa wanaowaza hivyo.

Mmemuona anavyoenjoy mwendokasi, na bado kuna mengi atayaona na ajue hizo ndio kazi za CCM.

October 28 kura zote ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Kwani Lissu amepinga mwendokasi??? Usafiri wenyewe mmeudumaza vibaya sana alafu mnapiga kelele humu???

Kwa sababu huna akili huwezi kumwelewa Lissu anaposema, uhuru, haki na maendeleo ya watu

Jiandae tu, Tundu Antiphas Lissu ndo Raisi wako wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,341
2,000
Kwani Lissu amepinga mwendokasi??? Usafiri wenyewe mmeudumaza vibaya sana alafu mnapiga kelele humu???

Kwa sababu huna akili huwezi kumwelewa Lissu anaposema, uhuru, haki na maendeleo ya watu
Uhuru ?

Tanganyika 1961 pioneers TANU, wewe unasema uhuru gani?

Haki - kwani Mahakama hazipo? Na ni haki gani unazizungumzia mbona wananchi haki zao zinazingatiwa?

Maendeleo- Muulize Lisu jana alikuwa picnic atakupa mrejesho na hiyo ni Dar tuu.

Sasa hivi unatoka Mtwara mpaka Bukoba mkeka tuu yaani unaweza kukodi hadi Taxi.

October 28 kura zote ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom