America vs aliens

  • Thread starter mzalendo namba moja
  • Start date

mzalendo namba moja

mzalendo namba moja

Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
36
Likes
26
Points
25
mzalendo namba moja

mzalendo namba moja

Member
Joined Oct 26, 2018
36 26 25
Mambo vipi wadau??..binafsi nmekuwa na maswali mengi kuliko majibu kuhusu kiburi cha Marekani, katika tafuta tafuta nmekutana na hili hapa chini...
Miaka ya 1940s kumewahi tokea ajali kubwa maeneo ya Mexico vifaa Fulani kama visosi (saucers) viligongana kimoja kikatua huko north corona na kingine mahali pa mbali sana ambako haikufahamika kwa haraka mpaka mwaka mmoja baadae ..
Kile cha kwanza kikaonwa na makamanda wa Mexico na haraka wakatoa taarifa marekani na uchunguzi ukaanza Mara moja, walikuta miili mitano ya viumbe wa ajabu wenye maumbo kama ya binadamu baada ya uchunguzi walikuwa wamekufa wote na nje ya kile chombo pembeni ya mwamba mkubwa kilikutwa kiumbe cha sita ambao kilikuwa hai japo hali yake haikuwa nzuri hata kidogo
Wamarekani walikichukua kile kifaa kama kisosi ambacho kinasemwa kilitumika kama usafiri wao na miili ya wale viumbe ambapo yule mmoja alianzishiwa matibabu na wale watano waliwekwa kwenye mafriji spesho ili miili yao isiharibike.
::waliwapa jina linaloitwa EBENS (Extra terrestrial being entities) na yule aliybaki hai aliitwa EBE1, alikuwa na uwezo wa ajabu sana na mkarimu, haikumchukua muda kujifunza kiingereza na kuweza kuwasiliana na wamarekani, alikuwa wazi kuhusu kile kifaa chao cha kupaa na wamarekani walijifunza lakini kwa wakati wote ilimpa tabu kula chakula cha duniani kwa sababu sio chakula alichokizoea, lakini alikuwa na kifaa maalumu cha mawasiliano ambacho kwa muda mrefu hakuweza kuwasiliana na wenzake pamoja na kwamba alituma jumbe nyingi lakini hakujibiwa.
;::jumbe alizozituma miongoni mwazo ni
1..kufahamisha kuhusu kwamba yuko hai
2..kuhitaji chombo kingine kitumwe ili achukuliwe
3..mpango wa binadamu kutaka kupata ujuzi zaidi kutoka kwao
:::mpaka mwaka 1952 haikuwezekana kupata mawasiliano na kile kiumbe kilikufa, hapo wamarekani walijikusanyia hazina ya kutosha kuhusu lugha ya EBENS na mambo muhimu kuhusu kile kifaa
:: miongoni wa mambo waliyoyajua ni kuwa wale viumbe walitokea mbali sana 37 light years kutoka duniani mfumo wao wa sayari una majua mawili tu joto ridi lao liko juu sana na wakazi wa ile sayari ile (EBENS) ni 650000 jinsia zako ni kama za binadamu wana uwezo mkubwa kiakili na wanaabu, inasemwa safari yao ya kwanza kuja duniani ni miaka 2000 iliyopita..ni wahamiaji kwenye hiyo sayari waliyoko walihama miaka 10000 iliyopita baada ya kule walikokuwa kuharibiw na volcano... vijana wa kiEBEN hupendelea safari ya kuyazunguka malimwengu kwa kutumia vifaa vyao vyenye nguvu sana na spidi pia, EBEN hufa na kuzaliwa pia.
:::::baadae miaka 1960 mwanzoni iliwezekana kuwasiliana na wale viumbe na walikubali kuja duniani mwaka 1963 kuwachukua wenzao pamoja na kubadilishana uzoefu wakati binadamu wakiwa ndio wanufaika wakubw wa mpango hyo.
waliandaliwa watu kadhaa kwa ajili ya safari kuelekea kwenye sayari ya EBENS iliyoitwa SERPO wanawake wawili na wanaume 10 ambao walifunzwa mafunzo makali sana ya uvumilivu na ya kisaikolojia..kifaa hicho kilitua kama ilivyopangwa mwaka 1963 lakini EBENS waliahirisha kuwachukua binadamu mpaka mwaka mmoja baadae ambapo kifaa kilitua tena na kuwachukua wale 12 na wao walimwacha mwanasayansi wao mwanamke
:::safari ilichukua miezi name kukamilika wawili wallifia njiani mmoja tu alifia kulekule na wawili baada ya muda wao kuisha waliamua kubaki kabisa waliandika vitu vingi takribani page 500..raha na shida waliyopitia
Waliorudi walilindwa sana na wa mwisho alifariki 2002
Aliyetoa siri hii alijiita anonymous na anadai alikuwa n sehemu ya timu
Sasa najua umejua kiburi cha marekani katoa wapi, hii n sehm NDOGO ya siri na America..
Uliza swali nikujibu
 
mtanganjia

mtanganjia

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Messages
599
Likes
415
Points
80
mtanganjia

mtanganjia

JF-Expert Member
Joined May 19, 2018
599 415 80
Chanzo cha habari
 
AVRAM

AVRAM

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Messages
228
Likes
243
Points
60
AVRAM

AVRAM

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2017
228 243 60
Marekani anakiburi na jeuri kwasababu hajawahi kubamizwa na kupata machungu ya vita na wala sio kwa majaliwa kama haya, hiz stories ni hadithi tu kama hadithi nyengine wala hazina ukweli. Na mara zote hizi stories unazisikia USA tuu si kwengineko, wale wachina, warusi, warabu na wengineo katika ardhi zao huwa hakuna matukio kama haya, ila kwa kujifurahisha na kupeana paukwa sawa tuendelee kupeana
 
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2018
Messages
1,577
Likes
1,140
Points
280
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2018
1,577 1,140 280
ningependa kujua kwani kabla ya ujuo huo wa ebens marekan hakuwa na kiburi!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,262,508
Members 485,585
Posts 30,124,295