eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 15,653
- 13,794
- Thread starter
- #21
Haya mambo ya kulialia kila siku kwa madhara ysliyotokea karne mbili zilizopita,Wala hayatusaidii,sisi weusi sio jamii pekee iliyotendewa ndivyo sivyo,hata waisrael waliuwawa,wa vietnam walipigwa,wanawake wa kichina walibakwa sana na Wajapan,huku kulialia Wala hakusaidii,
Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Mkulu sidhani kama umesahau udhalimu wa magharibi ambao umekuwa ukifanywa katika nyanja mbalimbali kwa miaka mingi. Uharamia wao ni endelevu. Siyo kama unavyodai kwamba ni wa karne mbili zilizopita. Udhalimu unaendelea, lkn kwa namna na mtindo ulioboreshwa zaidi.
Kumbuka udhalimu uliofanywa katika nyakati zetu huko Libya. Je tutasema kile kilichotendeka Libya ni haki? Kimeboreha hali? Libya ya kabla na baada ya kushambuliwa ipi ina ustawi na hali njema kwa raia? Nani walikuwa nyuma ya uhalamia huo?
Tukitafakari maswali haya yatatusaidia kuelewa kama magharibi ina nia njema na watu wa bara hili.