Amepoteza kitambulisho cha BVR, afanyeje?

laigwenan

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
325
79
Rafiki yangu Raheli ni mkazi wa Njombe. Alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwezi mmoja uliopita, kwa bahati mbaya jana amekipoteza na hajui cha kufanya ili apate kingine, sasa anaomba ushauri. Nini cha kufanya?
 
Yaani bora awe mpole tu, kwani kwa hasira walizonazo huko tume ya uchaguzi, juu ya matusi wanayopata kila siku leo uende eti nimepoteza kitambulisho!! wanaweza wakatoa mfano juu yako, kwa kumpa adhabu kali sana ili liwe fundisho. Kuna watu hata kukiona tu bado ye ameshapoteza!!! labda aende mkoa mwingine kama anandugu, na bado zoezi hilo linaendelea/au haujafikiwa atajiandikisha huko, ila atakuwa na uwezo wa kumchagua raisi tu, si wengine. Mpe onyo asithutu kabisa kuwaona tume, kwani hasira walizo nazo za wazee wazima kusutwa kama watoto, watammalizia yeye.
 
Mkuu sidhani kama mashine itakubali kusoma mara mbili ,
 
ameshindwa kupoteza simu anapoteza mali muhimu namna hiyo...alikuwa anazunga nacho virabuni cha nini!
 
Wakuu upotezaji wa belongings ni jambo la kawaida na linaweza kumkuta mtu yeyote na wakati wowote hivyo tungekuwa na kauli zinazoendana na shida ta mtu
Watu wanapoteza pesa mara tu wakitoka benki sembuse kitambulisho?
 
Rafiki yangu Raheli ni mkazi wa Njombe. Alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwezi mmoja uliopita, kwa bahati mbaya jana amekipoteza na hajui cha kufanya ili apate kingine, sasa anaomba ushauri. Nini cha kufanya?

jaribu kumdadisi vizuri isije ikawa ameuza kadi yake kwa wazee wa kazi wazee wa kununua shahada za kura
 
Mkuu sidhani kama mashine itakubali kusoma mara mbili ,

Kwa sasa bado hajizaunganishwa na mtandao,, za njombe ni njombe, ila kwa badaye lazima itagundulika tu mala zitakapounganishwa, Hata juzi huko mtwara, juzi walimkamata mtu amejiandikisha mala mbili na anavitambulisho viwili!!!! huu mfumo utaleta shida huko mbeleni,na walimkamata baada ya watu kumuona anavitambulisho viwili!! kwenye system hakutambulika!!
 
Siku nikikipata nakitunza kabatini kabisa na siku nikikitoa huko ni October 25 siku ya hukumu ya ccm

Hiyo mali ni heri nipoteze simu
Hapa nina kitambulisho toka 2005
 
Yaani bora awe mpole tu, kwani kwa hasira walizonazo huko tume ya uchaguzi, juu ya matusi wanayopata kila siku leo uende eti nimepoteza kitambulisho!! wanaweza wakatoa mfano juu yako, kwa kumpa adhabu kali sana ili liwe fundisho. Kuna watu hata kukiona tu bado ye ameshapoteza!!! labda aende mkoa mwingine kama anandugu, na bado zoezi hilo linaendelea/au haujafikiwa atajiandikisha huko, ila atakuwa na uwezo wa kumchagua raisi tu, si wengine. Mpe onyo asithutu kabisa kuwaona tume, kwani hasira walizo nazo za wazee wazima kusutwa kama watoto, watammalizia yeye.

Asithubutu kujiandikisha Mara mbili jela itakuwa inamtafuta mashine ikishakusoma haibahatishi tena,ukirud pingu unazo
 
Kama ni Ukawa mwambie akatoe tangazo kwenye vyombo vya habari kisha invoice aniletee ila next time awe makini.
 
Rafiki yangu Raheli ni mkazi wa Njombe. Alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwezi mmoja uliopita, kwa bahati mbaya jana amekipoteza na hajui cha kufanya ili apate kingine, sasa anaomba ushauri. Nini cha kufanya?

mwambie asubiri maboresho ya daftari la kura 2020
 
Rafiki yangu Raheli ni mkazi wa Njombe. Alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwezi mmoja uliopita, kwa bahati mbaya jana amekipoteza na hajui cha kufanya ili apate kingine, sasa anaomba ushauri. Nini cha kufanya?

Aende polisi kwanza akapate loss report...kwanza lakini kwa sasa hatoweza kupata kipya kulingana na utaratibu wa tume ulivyo maana kimsingi njombe walisha maliza zoezi!

Lakini kama watarudi tena basi anaweza akapata haki ya kupata kingine lakini kwa sasa nina hakika ameshapoteza haki yake ya kupiga kura na itabidi asubiri maboresho miaka ijayo pengine mitatu ijayo.
 
Rafiki yangu Raheli ni mkazi wa Njombe. Alijiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwezi mmoja uliopita, kwa bahati mbaya jana amekipoteza na hajui cha kufanya ili apate kingine, sasa anaomba ushauri. Nini cha kufanya?[/QUOTE
Mzembe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom