Ameponzwa na safari za dada kuiweka ndoa yake sawa ameolewa na mganga wa kienyeji

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,959
2,000
Yametokea huku kwetu Nanjilinji. Salome alitolewa posa na kijana kutoka DSM. Tulifahamishwa mchumba wa Salome wakati tunashonewa sare za wasindikizaji harusi.

Baada yaharusi Salome alindoka kwenda DSMna mume wake. Haikuchukua muda alimtumia nauli mdogo wake Esther amfuate huko DSM. Baada ya miezi miwili ya kukaa DSM Esther alirudi Nanjilinji. Tulifurahi kweli. Esther alituletea madera na mitandio anasema alinunua Kariakoo. Pia alitufahamisha kuwa siku hizi anaweza kutoka mwenyewe Kimara mpaka Kariakoo bila kupotea.

Kumbe Esther alitumwa dawa za kumuwekea shemeji asione wanawake wengine. Alianza safari za kwenda kwa mganga huko vijijini. Esther alikuwa anaondoka alfajiri na bodaboda na kurudi jioni. Baada ya hapo alituaga kuwa anakwenda DSM.

Kumbe mganga alimpenda Esther. Baadae tulisikia Esther amerudi akiwa mjamzito. Wote tulishangaa wale watoto wa Mwalimu Thomas wapate ujauzito kabla ya ndoa, maana Baba yaowalikuwa mtu wa maadili sana.

Esther aliolewa na Mganga wa kienyeji aliyekubali uhusika wake na ujauzito wa Esther. Kwenda kumsalimu Esther kijijini kwake tulimkuta akiponda dawa za wateja maana yeye ndiyo mke wa mganga tena.
 

T 1990 ELY

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
8,707
2,000
Kwenda kumsalimu Esther kijijini kwake tulimkuta akiponda dawa za wateja maana yeye ndiyo mke wa mganga tena.

Nimejikuta nacheka tu

Kama namuona vile Esther akiwa bize kuponda dawa za mme wake mganga wa kienyeji

Enough Of No Love
 

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
4,486
2,000
Kwenda kumsalimu Esther kijijini kwake tulimkuta akiponda dawa za wateja maana yeye ndiyo mke wa mganga tena.

Nimejikuta nacheka tu

Kama namuona vile Esther akiwa bize kuponda dawa za mme wake mganga wa kienyeji

Enough Of No Love
Usituambie umaiamin iyo stori
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom