Amepata matatizo ya usikivu, anataka kuhama chuo kusomea ualimu wa 'special needs'. Je, inawezekana?

Darucha

Senior Member
Dec 28, 2020
107
250
Jamani na rafiki yangu ambaye anasoma chuo jirani na Mimi hapa Arusha yeye ilibidi aingie mwaka wa pili lakini lakini Kuna shida ilimpata ya masikio yaani kwamba masikio yaliacha kusikia miaka ya nyuma ilimtokea hii Hali na wazazi wake walikuwa wanajua lakini alivyoenda chuo Hali ikawa mbaya.

Hakufanya mitihani wala kutoa taarifa chuoni sababu ya yeye kutokana mitihani akawa amekata tamaa. Sasa kuna ushauri kapata sehemu wanamuambia akasome uwalimu wa special needs, wale wenye matatizo ya ulemavu Kama viziwi, macho na mabubu.

Sasa anataka kwenda chuoni akaombe uhamisho aende kwenye vyuo wanavyotoa hizo kozi maana kwenye chuo alichokuwa anasoma hamna hizo kozi na anataka aanze mwaka upya.

Je, hili linawezekana? Mawazo yenu ni muhimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom