Amenishitaki police kisa nimemchapa makofi mawili

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
6,495
12,586
Habari za weekend ndugu zangu?

Hapa nilipo naandika huu uzi nikiwa mafichoni, kuna single mother nilikua nadate nae, sasa muda sio mrefu asubuhi ya leo kaniletea ujinga flani nikamlamba makofi, kumbe akakimbilia police station kwenye dawati la jinsia kunishtaki kuwa nimempiga.

Bahati nzuri nimetoka na police nao ndio wakaingia ndani kuja kunikamata, hizi habari nimepewa na mama mwenye nyumba wangu kuwa natafutwa na police kwa kosa la kumpiga huyo mwanamke.

Issue yenyewe ni kwamba nilimkataza huyu mwanamke asiwe anawasliana na huyo mzazi mwenzake na tukakubaliana mimi ntamtunza yeye na huyo mtoto ila sharti ndio hilo moja, kumbe mwenzangu anawasliana kisirisiri na hilo takataka lake ambalo halimsaidii kitu chochote.

Ushahidi ninao na baada ya kumuonyesha huo ushahidi ananijibu jeuri. Nikapandwa na hasira za ghafla ndo nikamzaba makofi, sasa wakuu hapa nilipo nipo kwa jamaa yangu flani nimejificha nisikilizie hii issue inavyoenda.

Nisaidieni mawazo wakuu hili swala nalimaliza vipi maana naona kama siku ya leo nitaimalizia lock up, na vipi hii kesi huwa ina dhamana kweli au ndio moja kwa moja magereza?
 
Mkuu pole Sana, kosa Kama hilo najua ni ngumu kuwepo ushahidi wa moja kwa moja labda kama atakuwa na alama usoni lkn ukienda usikiri kosa waambie tulipishana kauli na mwenzangu Ila sikumpiga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole Sana, kosa Kama hilo najua ni ngumu kuwepo ushahidi wa moja kwa moja labda kama atakuwa na alama usoni lkn ukienda usikiri kosa waambie tulipishana kauli na mwenzangu Ila sikumpiga

Sent using Jamii Forums mobile app
NASIKIA KACHUKUA ETI PF3,SASA SIJUI KAENDA KUTIBIWA NINI HUKO HOSPITAL
 
Kama mtoto ni wa mzazi mwingine ni haki ya baba kumjulia hali mtoto wake.
Na wewe inabidi kucheza part yako na kukubali hayo.

Hayo ni mambo ya kawaida. Hayahitaji hasira hata kama baba wa mtoto atakuja kumuona mwanae ni sawa ana haki

Punguza hasira na umuone uliempiga kabla hujaenda polisi, mbembeleze na umwambie mkafute kesi kwani ugomvi wa wapendanao ni vigumu kufungwa labda polisi waamue tu
 
NA CELLO NAWEZA NIKAWEKWA MKUU?
Ukifika yaani ndio hatua namba mbili baada ya kuvua mkanda na viatu!
kimbia mafichoni hivyo hivyo ikifika kesho tu mkeo ataipotezea na hatarudi tena polis

D.A "Mwanaume mashine"
 
Mkuu wewe kama mwanaume...kuna vitu utavipitia hasa kama ukiwa na mwanamke pasua kichwa...

Cha kwanza ni USTAWI WA JAMII...Hapa ndio kimbilio la hawa dada zetu

Cha pili ni DAWATI LA JINSIA NA WATOTO

Cha nne ni polisi/selo...

Alafu ukiona mwanamke anakupeleka polisi anza kujichunguza mapema huyo hastahili kuwa mke!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom