Amenipa mwezi mmoja niwe nimeshamuoa vinginevyo ananiacha, sina mahari nifanyeje

Spanishboy

Senior Member
Apr 24, 2011
118
65
Habari ndugu, mimi na mchumba wangu tumedumu kwa miaka 8 sasa, hatukufunga ndoa kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo ya kimasomo, mwenzangu amemaliza chuo mwezi wa sita mwaka huu na mimi ndo nimemaliza mwezi uliopita, kinachosubiriwa ni kwenda kulipa mahari ili kufunga ndoa, kwa kuwa nilikuwa masomoni sijajipanga vizuri kwa maana ya pesa za kulipa mahari, nimemwambia mpenzi wangu anivumilie nigangegange maana hata mahari najilipia mwenyewe, lakini cha ajabu ameniambia amechoka kusubiri, amenipa mwezi mmoja niwe nimekamilisha taratibu za kumuoa, vinginevyo ataniacha, nifanyeje ndugu zangu, nisaidieni!
 
Huyo ana mtu mwingine anamsumbua huko duniani,jiulize mwenyewe kama anakupenda kweli na anajua ulikuwa masomoni kwanini asikuvumilie mpaka usimame?swali lingine?
 
jamani..miaka 8 mlianza sijui mkiwa level gani.............

atakuwa kachoka we miaka 8 mkoo kwenye uchumba tu....na nyie vijana haamkawii kubadilika

jaribu kuongea nae.....umweleze khaali halisi!!!!!!!!!maisha ya ndoa inabid uwe umejipanga
 
Habari ndugu, mimi na mchumba wangu tumedumu kwa miaka 8 sasa, hatukufunga ndoa kwa sababu ya kutaka kutimiza malengo ya kimasomo, mwenzangu amemaliza chuo mwezi wa sita mwaka huu na mimi ndo nimemaliza mwezi uliopita, kinachosubiriwa ni kwenda kulipa mahari ili kufunga ndoa, kwa kuwa nilikuwa masomoni sijajipanga vizuri kwa maana ya pesa za kulipa mahari, nimemwambia mpenzi wangu anivumilie nigangegange maana hata mahari najilipia mwenyewe, lakini cha ajabu ameniambia amechoka kusubiri, amenipa mwezi mmoja niwe nimekamilisha taratibu za kumuoa, vinginevyo ataniacha, nifanyeje ndugu zangu, nisaidieni!

Poleni, Nadhani hakuna kitu cha kusiubiriana, Kama haiwezekani kusubiri mwambie aendelee tu, huyo ashapata mtu mwingine hayo masharti unayopewa ni magumu kama yale IMF wakati wa Nyerere. Kama kweli mmekaa naye miaka 8 anajua uwezo na hali yako, Kama sasa anadai ufanye haraka huyo anakuzuga tu anaye mtu wake tayari hapo ushaliwa ndugu yangu Jipange tu kwa kumtafuta mtu mwingine.

Mwisho hayo mahusiano mliyokuwa nayo si afya kwa ndoa, Mtasumbuana mpaka ujute kuzaliwa, Hakuna dini inayoruhusu mchezo huo afu ndo kisha mfunge Ndoa. Kasome Biblia kitabu cha Mwanzo Sura ya 24:1-67
 
nasikia harufu ya risasi hapa
 
Eh ndo mana cpendagi mahusiano ya mda mrefu aisee,akikutosa mtu una'wonder uelekee wapi..km kashakuchoka saiv kifungo cha maisha cha nin,heri kuvunja uchumba kuliko ndoa,mnawah wapi btw taften faranga kwanza jmn,muelimishe mpenzio
 
hujamuoa masharti kibao ukimuoa itakuaje,kama kaweza vumilia kwa miaka 8 anashindwa nini kuvumilia huku mkiani mlikofika?,angalia usije muoa alafu mkiwa ndoani anakuambia 'usiponunua nyama leo naenda kwetu'.Akili ni nywele na kila mtu ana zake.
 
mnh huyo ana lake ,kidumu kilikuwa kinasaidia masomo kule chuo....nakutania,kiukweli dada wa watu kachoka kusubiri, mjipange miaka kibao kwa event ya siku moja,ongea nae mfanye harusi ya kawaida inayoakisi budget yenu au unaweza tembeza bakuli watu wakupe tough ufanye hio harusi acha kufa na tai shingoni....cha muhimu mkishaoana msizae kwanza mpk muwe mmejiandaa ,i
 
Wala asikupe presha jipange mwenyeo taraatibu uweke maisha yako vyema.....kama anakupenda kweli atakuvumilia na kukusubiria
Ameshajua kuwa bado hujajipanga ana maana gani kukwambia hivo? Au ukaibe? Achana na huo upuuzi wake... Na atafute huyo wa kumuoa kama rahisi..
 
huyo mwanamke kiboko,hahaaaaa anataka na yeye chicken party,(kitchen party) loools,kampa mwenzie ultimatum, inabidi kujichunguza upya asije akawa ni wale wanaopenda kucomand,hawapendi kushirikiana kimawazo.....
 
Aisee ujue miaka nane ni mingi sana kwa uchumba..
Pengine kuna msukumo unaofanya alazimishe ndoa,labda kutoka ndani ya familia au kwa marafiki..
Anahisi hautaki kumuoa ndo maana unaweka vikwazo..
.....na pengine kuna mwingine ameshamtongoza na ahadi ya ndoa juu
.....zungumza nae miaka 8 ya uvumilivu ni mingi kufanya maamuzi ya haraka..ikiwezekana muombe msaidiane kutafuta pesa ili mtimize ndoto zenu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom