Amenifungia nguo na kuweka kwenye begi eti nimpishe kwake japo kodi nalipa mimi

Asemavyo

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
312
821
Mkuu Naomba unisaidie kuomba ushauri huko

Ni week sasa nimempisha lakin anaomba msamaha nirudi

Ishu yenyewe iko hivi, mwaka huu nilimpata Dada mmoja nesi tukapendana nilikuta amepanga nyumba, nami kwakuwa nilikuwa kwenye shughuli za kikazi maeneo yale nilikuwa nimefikia nyumba ya wagen kabla ya kumpata

Nilivyompata akanishawish kukabidhi rum kwenye gest house nikae kwake, nikasema ngoja kwanza nikamilishe kazi

Nikakamilisha kazi nikasafiri kuipeleka sehem husika alinisindikiza hadi uwanja wa ndege na kulia sana kwamba namuacha,

Nikapiga moyo konde ndani ya Emirates nikafika huku mawazo ya hapa na pale yakitawala,

Baada ya kumaliza miezi 4 nikaamua kurudi Tanzania nikakuta kanisubiria kawaida

Kufika nyumbani nikakaa week jamaa akaja kuniambia yaliyokuwa yanaendelea nikakaa kimya nilichofanya nikaenda Kwa rafiki yake wa kike nikajifanya kuomba simu kumpigia mtu,
Nilijua fika kwamba hawezi fichana na rafiki au awez fanya jambo bila rafiki yake kujua,

Nikakuta wanayochat na shoga yake wakizungumzia yanayofanyikaga nikiwa sipo, niliumia

Nilipomuuliza akasema nipishe kwangu

Akanipangia nguo na kunitolea nje ilikuwa saa 5 usiku,

Nikatafta piki PIKI nikatafta nyumba ya wageni,

Sasa analia eti turudiane mara anakili kosa , Kuwa nimsamehe

Huku akishikiria msimamo wa kwamba alisingiziwa zilikiwa hasira

Msimamo wangu simrudii ni aibu dume kuwekewa nguo kW begi huko kodi nililipa miezi 5 na biashara nikamfungulia,

Au mnanishaurije
 
Pole sana mkuu, hawa viumbe wagumu sana kueleweka. Hali kama yako iliwahi kunipata, nyumba nimemlipia akaniletetea habari za nimpishe, nilimgomea na nikasubiri wakati muafaka, kodi ilipoisha na nikiwa na uhakika ana hali ngumu financially... Nikasepa.

Acha nae kabisa.
 
Back
Top Bottom