Amempaka mtoto mchanga mkorogo ili awe mweupe

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Aisee Bongo kuna mambo

Kuna huyu Dada anasema jiran yake anampaka mwanawe lotion kali ili awe mweupe mwambie ampelekee hii story from Idd makengo

=======

INASIKITISHA SANA: MAMA, WATOTO WADOGO HATUNA DHAMBI!

Nakumbuka wakati huo ndiyo Facebook ilikua inaanza, tena kwa kutumia Compiter sio simu, nilikua natumia Laptop ya mume wangu, nilikua napiga picha kwa kutumia kamera na kuzihamishia kwenye computer kisha napost. Kuna dada mmoja nilikua namfuatilia Facebook, alikua na watoto wake mapacha wakike, wawili, kila akipost picha za watoto wake watu walikua wanachanganyikiwa, wanasifia, wanampingeza kuwa ana watoto wazuri.

Kama wanangu wanae walikua na miaka kama minne hivi, walikua waodogo kama wangu, tofauti ilikua ni moja, tu, wanae walikua ni weupe. Yaani alikua akiweka picha ni dakika mbili wanawake watakua bize kumsifia, hali hiyo ilikua inaniumiza, mimi nilikua na watoto wawili, mmoja wa kika na mwingine wakiume, wa kiume alikua na miaka mitano na wakike alikua na miaka mitatu.

Nilikua nawapost kila siku lakini hakuna aliyakua anacomment, sanasana nikipost na picha yangu basi ndiyo naona watu wananisifia mimi na si wanangu. Wanangu wamefanana na mimi lakini weusi wamechukua wa Baba yao, mimi ni mweupe na ni mzuri, kila mtu ananisifia na kila mtu ananipenda. Hali hiyo ya wanangu kutokusifiwa katika mitandao iliniumiza sana, nilikua naumia ziadi nikimuona yule dada anasifiwa.

Wanangu ni weusi, wazuri na na wapenda lakini niliona kama vile watu hawawapendi hivyo bila kujijua nikajikuta naanza kuwachukia. Nikajikuta nataka kuwabadilisha, nilianza kwa kumsuka huyu mdogo, kwakua nywele zake ni kama za Baba yake si kama zangu, yaani ni kipilipili basi niliamua kumuweka dawa, Baba yake mwanzoa lishtuka lakini nilimuambia ni mafuta tu ya kawaida, basi zikalainika na kweli nikawa namsuka, anapendeza watu wanamsifia.

Nikawa nikipost picha basi utasikia nywele zak4e nzuri, kapendeza, hali hiyo ilinipa faraja sana, nikaamua kuhamia kwa mtoto wa kiume, nikawa naye nampaka dawa nywele, namnyoa kisasa anapendeza, watu wanamsifia. Lakini watu walikua wanamsifia tu nywele, sio muonekano, pia nikilinganisha na watoto wa yule dada niliona kama vile wanangu ni wabaya, nilianza kufuatilia ni kitu gani naweza kufanya ili wanangu kuwa weupe kama mimi na kusifiwa katika mitandao.

Basi katika kufuatilia fuatilia kwneye mitandao ndiyo siku moja nikaona dada mmoja anauza mkorogo, ni mafuta ya kupaka. Nilimtafuta inbox na kumuuliza kama yanaweza kupakwa hata na watoto waodgo, aliniambia kuwa hamna shida, akanitumia na picha za wanae akiniambia kuwa anawapaka na wanakua weupe bila shida. Basi nilimuamini na kuanza kuwakapa wanangu, kweli haikuchukua miezi miwili, wanangu wakawa wanabadilika rangu, wanakua weupe kama mimi.

Nilijikuta nakua na furaha kwani niliona kama watu wanawapenda, nilifuta ppicha zote za zamani katika mitandao na kubaki na picha mpya tu, nikawa nikipost watu wanasifia, ikaja Instagram, hapo nakumbuka nilikua na ujauzito wa mtoto wangu wa tatu. Niliamua kuwabadilisha kabisa wanangu, nilitaka wawe weupe kama mimi. Nilikua nawapaka cream kalikali, ikiish ahii nikiona haina matokeo nabadilisha, yaani ilikua ni kubadilisha mpaka watoto wakawa weupe.

Mume wangu hakua akifuatilia sana, alikua anashangaa watoto wanakua weupe namtania kuwa wameamua kumfuata Mama yao. Kwakua sura walikua wanafanana na mimi kila nikienda sehemu na hasa mwangu wakike na watu kunisifia kuwa ni mzuri basi nilijisikia vizuri. Nilikua na ujauzito na kila siku nilimuomba Mungu kunijaalia mtoto mzuri kama mimi, mtoto mweupe, mtoto wa kupost Instagram.

Nilikua na hamu sana ya mtoto wangu kuzaliwa, kumfungulia akaunti Instagram na kuanza kumposta, nilitamani sana awe mweupe, mzuri na sikutaka kabisa kuchukua sura ya Baba yake kwani sikutaka kuhangaika na michepuko. Lakini ni kama Mungu alikua ananiadhibu, sio kwamba tu mwanangu hakuwa mweupe lakini alichukua sura ya Baba yake. Yaani mara ya kwanza nimetoka kujifungua tena kwa kisu naletewa mtoto wangu ili nimuone nilihisi kuchanganyikiwa, mtoto alikua mweusi tiii kama Baba yake, alikua kafanana sura na Baba yake, yaani kwa wakati huo nilihisi kuwa nimzaa kituko.

Nilijikuta nalia, kila mtu alidhani kuwa ninalia kwasababu ya furaha mtoto kazaliwa mzima ana afya lakini ukweli nikuwa nilikua nalia kwakua sitapata fursa ya kumpost mwanangu katika mitandao. Niliruhusiwa kutoka hospitalini na kurudi nyumbani, lakini sikua na amani, yaani sikumpenda mwanangu, nilijikuta namchukia, kuna wakati nilikua natamani hata nisimnyonyeshe afe tu ili nisimuone.

Sio kwamba alikua mabya, sio kwamba mume wangu ni mbaya, hapana lakini hakua mweupe na sura haikua kama yangu, hakua mzuri kama nilivyotegemea. Mwanangu akiwa na miezi mitatu tu nilianza kumpaka mkorogo, nilimpaka mpaka anafikisha miaka miwili, lakini tofauti na wale wakubwa ambao mkorogo ulikubali na kuwa weupe huu ulikataa kabisa. Yaani kila nikimpaka akawa anakua na mabakabaka, mtoto mdogo anakua na mabakabaka kwenye mwili hasa vidoleni na kwenye magotio, baada ya kuona inashindikana niliamua kuacha.

Niliacha kumpaka mwanangu mikorogo mpaka alipofikisha miaka minne, hapo ndipo nilikutana na Post moja Instagram ambayo ilikua inahusu vidonge, nilimpigia mhusika simu, aliniambia yeye ni daktari wa ngozi na ana uzoefu wa hiyo kai kwa muda mrefu. Nilimuambia kuhusu kumpaka mtoto mdogo mikorogo, akaniambia hapana kupaka ni mbaya kwenye ngozi hivyo akanipa vidonge nikawa nawapa wanangu.

Kweli vidonge vilisaidia, mwanangu mdogo alianza kubadilika tararibu na kuwa mweupe, uzuri wake ulianza kuonekana na kwa namna flani nilianza kumpenda na kumuona kama mwanangu tena. Ingawa sikuwahi kumpost kwakua hakua sawa na hawa wengine, kwamba nilipenda kupost wanangu wawili kwani wao mkorogo uliwakubali, kwakawa waupe na kwakua nilifanana nao basi niliwaona wazuri, wakati huo walishakua wakubwa lakini bado sikuacha kuwapaka mikorogo.

Nilihofia kama nikiacha basi watabadilika na kuwa weusi kwani kuna kipindi niliacha kwa mwezi mmoja ngozi ikaanza kufifia. Dawa ya vidonge ilisaidia kwa muda, ilimsaidia mwanangu mdogo kumuondolea madoadoa lakini baada ya muda iliacha kufanya kazi, akaanza kuwa mweusi tena, nilijihisi kuchanganyikiwa, nilirudia mikorogo meingine ambayo nilikua nikiona matangazo Instagram basi nanunua.

Lakini mwaka jana wakati mwanangu anaingia miaka mitano hali yake ilibadilika, ngozi yake ilianza kuwa na matobomatovo ambayo baada ya muda yaligeuka na kuwa vidonda. Sio kama zamani ambapo ilikua na madoadoa hapana, lakini sasa hivi ilianza kuwa na matovo na hatiomaye vidonda. Hali ilizidi kuwa mbaya, nikaanza kuhangaika na mahospitalini, nilihangaika sana mpaka nikaambiwa kuwa mwananangu ana kansa ya ngozi. Madawa niliyokua nampaka tangu akiwa na miezi mitatu yalimuathiri sana.

Hapo ndipo mume wangu alishtuka kuwa, weupe wa wanangu haikutokana na kubadilika kwa kawaida au kutaka kufanana na mimi bali nilikua nawachubua kwa madawa makali. Tulihangaioka sana hospotali lakini hali ya mwanangu ilikua mbaya sana, vidonda vilikua haviponi, kikikipona hiki kinakuja kingine. Hali yake ilikua mbaya na katika kumuuguza nililazimika kuacha kazi kumhudumia, ilifikia hatua hata ukimgusa tu ni kidonda kwani ngozi yake ilikua dhaifu.

Alikua katika maumivu makali, niliacha kabisa kuwapaka wanangu wakubwa mkorogo, sikujali tena kama watakua weusi, sikujali kuhusu mitandao ya kijamii, sikujali chochote. Nilikua hata siwezi kuingia kwenye mitandao ya kijamii, yaani nilikua kama mtu aliyechanganyikiwa kwani nilijua kuwa ujinga wangu ndiyo umemuua mtoto. Mwaka huu mwezi wa pili mwanangu alipata kidonda kikubwa kichwani, nilikua kikubwa kiasi kwamba nywele zilinyonyoka, yaani kichwa kilikua kama tope.

Alikua katika maumivu makali, hawezi kulala, hawezi kujisogeza hata kumuogesha ni kwa kumfuta tu. Nilikua naumia sana nikimuona vile, kila wakati nilikua nalia, nikiwa karibu yake nikimuangalia mwanangu, binti yangu, amabye alizaliwa mzima na afya nzuri lakini alikua katika hali ile, nilikua nalia sana.

“Mama usilie sana mimi hata siumwi sana…” Nakumbuka siku moja aliniambia, nilimuona akiwa katika maumivu makali, lakini alikua ananionea huruma mimi. Wakati huo ndiyo alikua kabakiza miezi mitatu tu kutimiza miaka sita.

Wakati anaanza kuumwa alikua chekechea akijiandaa kuingia darasa la kwanza,a likua na akili sana darasani na kila mtu alimpenda kwani alikua ni mchangamfu.

“Mama unajua sisi watoto tukifa hatuchomwi, kwakua sisi hatuna dhambi. Tuliambiwa hivyo Madrsa kuwa, watoto hawan ahdambi, mimi sina dhambi, nikifa ninaenda sehemu nzuri, hivyo Mama, hata nikifa sitaki ulie, jua tu mimi nitakua sehemu nzuri.”

Nakumbuka ilikua ni siku ya Jumamosi, ya Tarehe 11 mwezi wa nne mwaka 2020, ni siku ambayo sitakuja kuisahau katika maisha yangu. Nilikua nyumbani, namsafisha mwanangu kwa kitambaa, kilikua ni kipindi cha Korona na jumamosi hivyo kila mtu alikua nyumbani. Wakubwa zake walikua sebuleni na mimi ndiyo nilikua namsafisha, mimi pekee ndiyo nilikua naweza kumhudumia mwanangu na mara nyingi alipenda kuwa na mimi, hata chakula alikua anakula nikiwepo mimi tu.

“Kwanini unasema hivyo mwanangu, hutakufa, usiseme hivyo….” Nilimuambia huku nikijaribu kuyazuia machozi, mwanangu alikua na akili sana, sana, yaani kama ni akili alichukua za Baba yake, kama alivyochukua sura.

“Hapana, Mama, nimechoka kuumwa, Mama nateseke, kila kiungo katika mwili wangu Mama kinauma, naumwa sana Mama, najua sitapona Mama, namuomba tu Mungu anichukue mapema nisiendelee kuteseka.” Aliniambia, nilishindwa kuvumilia, maneno yake yalikua ni makali sana, nililia kama mtoto mpaka watu walikua sebuleni walikuja.

Mume wangu alikua katoka kaenda kununua vitu vya nyumbani kwani baada ya mtoto kuumwa yeye ndiyyo alikua anafanya kila kitu, anaenda sokoni, ananunua chakula, dukani na kila kitu. Waliokua sebuleni alikua ni wifi yangu, wanangu wawili na binti wa kazi, walikuja wakijua mwanangu ameshakufa, lakini walimkuta anacheka mimi ndiyo nalia, waliuliza sababu akasema kuwa hamna Mama analia tu vitu vyake.

Basi niliwaambia wale wengine kutoka, nikamalizia kumsafisha. Baada ya hapo aliniambia.

“Mama leo naomba mnipikia Makande ya Bibi. Nataka tule wote.” Aliniambia, nilishangaa kwani kwa Bibi yake alienda mara moja, tena nakumbuka ni wiki kama mbili kabla ya kuumwa, basi akapikiwa Makande, hata hakuyapenda na hakula kabisa kwani yalikua ni mageni wkake, ila siku hiyo aliyataka. Basi nilimuambia kuwa nitampikia.

“Baba yuko wapi Mama?” Aliniuliza, nilimuambia Baba yake katoka, aliniambia kuwa, akirudi anaomba kuonana naye.

“Nataka nikae na Baba yangu Mama, unajua Baba anafanya kazi sana hata hatupati muda wa kumuona, nataka nikae naye.” Aliniambia, ni kweli mume wangu ni mtu wa kazi sana, mara nyingi ni mtu wa kusafiri na kuna wakati anaweza kukaaa hata mwezi hajaonana na watoto. Basi nilijikuta tu nampigia simu mume wangu na kumuambia arudi nyumbani, nilimuambia hata kama hajapata alichokua kaenda kununua arudi mtoto anamhitaji.

Basi mume wangu aliacha kila kitu na kurudi, moja kwa moja aliingia chumbani kwetu ambapo ndiyo tulimhamishia mtoto ili iwe rahisi kumhudumia. Mume wangu aliingia chumbani, mwanangu alimuomba Baba yake ampakate wakawa wamekaa kwenye kochi pale chumbani, mimi nilitoka kwenda kumpikia mwanangu Makande, nilienda kupika nilipomaliza nilirudi chumbani.

Nilikuta mume wangu kapitiwa na usingizi kwenye kochi huku kampakata mtoto ambaye naye alionekana kulala ila kajinyoosha, nilimuamsha mume wangu nikiamini kuwa mtoto naye kalala, kwakua suala la usingizi lilikua la shida nilitaka amnyanyue taratibu na kumlaza kwenye kitanda chake na kama ni chakula atakula baadaye lakini mume wangu alipoamka tu na kumuona mtoto nilisikia akisema.

“Mtoto amepoa, amekua wa baridi.” Alijaribu kumuamsha lakini hakuamka, aliniangalia jicho moja usoni nilijua mwanangu kashafariki nilidondoka na kupoteza fahamu.

Mpaka namaliza mazishi ya waangu hali yangu ilikua ni kuzimia na kulazwa hospitalini. Nimeumia sana, nimejaribu kujisamehe lakini nimeshindwa, yaani mpaka sasa hivi sipati usingizi mpaka kunywa dawa za usingizi, nilishakua teja mpaka mume wangu aliponitafutia msaada wa mwana saikolojia angalau kidogo naweza kulala. Wanangu wawili wanaendelea vizuri, tangu kuacha kuwapaka mkorogo huyu mkubwa karudi kawaida ila mdogo wakike ambaye nilianza kumpaka tangu akiwa na miaka mitatu yeye bado ana mabakamabaka namuomba tu Mungu awe salama.

Najua watu watanitukana, wataniona mjinga, watasema mengi, lakini Kaka Iddi nimeamua kuongea na wewe ili uandike kisa changu kwakua bado kuna watu ambao hawajiamini kama mimi. Kuna mtu hawezi kupiga picha kwakua ana mapele, kuna mtu anaficha mtoto kwakua anahisi ni mbaya, nataka uandike kisa changu kwakua kuna watu wengi hawajiamini kama mimi na wanawachubua watoto.

Kuna watu wanawapaka watoto wa domo wa mwaka mmoja madawa ya nywele ambayo mengi ni makemiko ili tu wapate picha nzuri za kuweka Instagram, wapo wengi, nikikumbuka kilichotokea kwa mwanangu natamani kupaza sauti ila siwezi, andika wengine wajifunze. Kuna watu hata kuongozana na watoto wao hawataki, wanalazimishia vitu vingi na kuwabadilisha watoto. Lakini akina Baba nanyie, hembu msituruhusu kufanya maujinga yetu kwa watoto.

Wanawake wengi hatujiamini, tunajichukia, tunapenda kufurahisha watu, tunapenda kuiga na kusifiwa. Ukiona mke wako anaanza kumuweka madawa kichwani mtoto mdogo badala ya kumchekea mchukue mwanao kamnyoe hizo nywele basi, ukiona anaanza kumpaka mafuta ambayo hayaeleweki basi piga marufuku. Kaka hakuna siku hata moja ambayo sijutii, sijui nitafanya nini mwanangu wakike, yaani ana mabakamabaka baada ya kuacha kumpaka mkorogo, sitaki kuambiwa dawa tena, naamini Mungu atamsaidia na atakua sawa.

MWISHO
 
Twende turudi...mijini watu wanapelekwa sana na matukio...nadhani ndo changamoto kubwa...tujifunze kua watu wa kiasi
 
Hata kama ni ya kutunga inafikirisha na pia inafundisha,dunia(walimwengu) imekuwa ya ajabu sana..leo hii uzuri umegeuka kuwa weupe! fikra hatarishi sana "mental slave" hebu jamii tubadilikeni mfano huu unapelekea chukizo kwa Mungu na fedheha kwa jamii yetu
 
Hii kali aisee.
Kama tukio la kweli basi huyo mwanamke kichwa chake kitakuwa mfano wa lile container lisilokuwa na partitions kama mdau dmkali alivyoelezea.

BTW, wanawake wengine wengi tu wana vichwa vizuri siyo kama huyu.
 
Ata kitendo cha kuwapiga vitoto vichanga picha na kuwarusha mitandaoni bila ruksa yao ni makosa Sana...

Sema ulumbukeni wa mitandao unatusumbu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom