Amemkuta mke wake ana ujauzito wa wiki tatu wakati hakuwepo miezi miwili

Nyanda lunduma

Senior Member
Apr 10, 2015
187
68
Ndudu wana jukwaa ni kwamba ni rafiki yangu ambaye kazi yake ni mvuvi wa samaki, amekuja kwangu kuomba msaada wa kimawazo kuwa yeye alitoka kwenda kuvua samaki, familia yake akawa ameiacha, Alimuacha mke wake na mtoto wake mmoja, huko alikaa miezi miwili na baada ya kurudi tuu alimtilia mashaka mke wake kuwa amehamisha penzi kwa mwanamume mwingine na alipofika tuu mke wake alimpeleka kupima mimba.

Baada ya kufanya kipimo, mimba kama ya wiki tatu ilionekanajamaaa alikosa nguvu na baada ya hapo kaja kwangu kuomba ushauri na mimi nimemwabia kuwa ni KOSA KUBWA SANA MWANAMKE ULIYEMTOLEA MAHARI APIGWE MIMBA HALAFU WEWE UMEENDA KUPAMBA ILI ALE --HIVYO MIMI USHAURI NILIOMPA NI KUWA AMPIGE CHINI ACHANE NAYE.

KWENU WAKUU KWA MSAADA.
 
Umechemka mkuu mambo ya ndoa ni magumu sana ... Ulipaswa usikilize pande zote mbili ndio utoe uamuzi ushari wa muhimu wa tengane kwa muda tu ili kumpa nafasi kila mmoja kujitathimini

sent from HUAWEI
Nilipomuuliza jamaa kwamba kwanini ameamua afanye hivyo, mwanamke alimwambia haamini hata yeye alipoenda hivyo alipitiwa tuuu
 
Nasikitika tuu kwamba wanaume wawili lakini bado mmeshindwa kujua la kufanya. Wanaume nguvu zenu za maamuzi mnazipeleka wapi siku hizi?

Qur'an na bible vimetoa muongozo nendeni mkasome
 
Umempa ushauri mbaya sana,mke aombe radhi na amsamehe na huyo mtoto ni wake huyo mvuvi,amlee kama wake na siri hiyo ibaki miongoni mwao tu mpaka mwisho wa dunia,kwa njia hiyo tu ndio atasamehewa makisa yake na MOLA
 
Umempa ushauri mbaya sana,mke aombe radhi na amsamehe na huyo mtoto ni wake huyo mvuvi,amlee kama wake na siri hiyo ibaki miongoni mwao tu mpaka mwisho wa dunia,kwa njia hiyo tu ndio atasamehewa makisa yake na MOLA
Boss, chukulia hicho kisa ni cha kweli, na mtu aliyetenda jambo hilo ni MWANAMKE, kama unaelewa ninakoelekea


Master key ni ya kutunzwa sana, kinyume chake si sawa
 
Back
Top Bottom