Amejikata sikio wakati akiwa kwenye harakati za kujikomboa kutoka kwenye mashambulizi ya nyuki

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,548
6,102
Wakuu kama kichwa cha habari kinacho sema. Aliyejikata sikio ni mzee mmoja anayefuga nyuki katika moja ya shamba lake.

Habari nzima ipo hivi, huyu mzee ana tabia ya kila asubuhi na jioni kwenda kutembelea mizinga yake ya nyuki iliyopo katika moja ya shamba lake. Mzee ana tabia ya kwenda shambani kwake akiwa na kisu au panga.

Kama ilivyo ada leo mzee kaenda ila kwa bahati mbaya kakuta nyuki wamevurugwa haijulikani na nini kwani mzee anavyo dai kitendo cha kukaribia tu kwenye moja ya mizinga yake nyuki walianza kumshambulia kwa wingi.

Katika kujihami huku akiwa na kisu chake mkononi akaanza kukimbia aliko tokea huku akiwa anarusha rusha mikono kwenye kichwa ambapo nyuki walikuwa wakimshambulia kwa sana na ndipo alipo jikata sikio lake la upande wa kulia.

Kutoka na makali ya kisu alicho kuwa amebeba kipande cha sikio hapa hana hivyo kwa sasa tunasubiri nyuki watulie huko shambani tuingie kutafuta hicho kipande cha sikio pamoja na kisu chake kwani alikitupa.
 
Nyuki wamekasirika wanasema hawataki kulishwa na badalayake watatafuta wenyewe chakula. Iwe ni funzo siku nyingine. Nyuki ni wadogo lakini wanauma sana.
 
Mimi kwangu tukio hili nachukulia kuwa ni habari njema sana, hakipo kitu cha kuisikitisha hapa. Bora amepoteza sikio atapata jingine hata kwa plastic surgery, kuliko angepoteza uhai! Nampa pole sana pia!
 
Mimi kwangu tukio hili nachukulia kuwa ni habari njema sana, hakipo kitu cha kuisikitisha hapa. Bora amepoteza sikio atapata jingine hata kwa plastic surgery, kuliko angepoteza uhai! Nampa pole sana pia!
Japo ungesema kwanini habari njema uwenda ukawa na point kuliko kuachia uwanja wa watu kukutoa akiri.
 
Back
Top Bottom