Amechaguliwa kwenda Chuo, napata wakati mgumu

Hata ukimuoa wakati huu akienda huko chuo kama ataamua kubadilika atabadilika tu, wewe muamini labda kama kuna viashiria ambavyo amevifanya na vikakupa huo wasiwais vinginevyo unajitia jaka la roho bure japo wakat mwengine waswas ndio akili, wewe muamini mwache akasome muhim mawasiliano au ukiona hutaweza heri muachane mapema tu
umenena kiutu uzima asipouelewa uu ushauri basi akili kichwan mwake
 
Nina binti nilikuwa naye kwenye mahusino miaka 3 mpaka sasa, nilitarajia ndio awe mke wangu wa ndoa. Kinachonipa wasiwasi ni kuwa huyu binti mwaka huu amechaguliwa kusoma Chuo level ya Afya miaka 5, alikua na Diploma ya Afya.

Mambo makuu manne yananiumiza kichwa:

1. Umri wangu unasonga mbele
2. Nikiwaza mpaka amalize iyo miaka 5 nachoka kabisa
3. Nikiwaza vishawishi vya chuo anaweza kuvivuka salama, imani hainipi
4. Nikiwaza nimsubili ili nije kumuoa yeye nawaza je akija kubadilika siku za usoni itakuwaje?

Note: Kwao pesa ipo, si mwepesi kushawishika kwenye pesa. (Labda itokee kwao wafirisike kabisa ivi karibuni)

Note: Familia yake yote inanijua kama mimi ndio boyfriend wake

Note: Yeye hajanikosea chochote kile mpaka muda huu, ila mimi nimekuwa ni mtu wa wasiwasi sana sana

Naombeni ushauri wenu kwenye ili ndugu zangu, the niachane naye huyu binti aendelee na shule yake, nimvumilie na kwenda naye mdogo mdogo au nifanyeje

Karibuni
Nipe jina la chuo niwe chawa🏃🏃
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom