Ameamua kuvunja uhusiano nifanyeje

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
jamani wana jf nina mpenzi wangu tumekaa nae kwenye uhusiano kwa muda wa miaka miwili na tulikuwa tunapenda sana ila muda ukafika nikaamua nianze mikakati ya kuoa,nilipomwambia tu kuhusu ndoa akaanza kupunguza uhusiano wetu mpaka sasa amesema tuachane
nifanyeje na ninampenda na sina mtu mwingine kwani nilimtegemea yeye?

Ndugu,angalau kwa kidogo sana ungechanganyikiwa kama ungekuwa umemfanyia jambo ambalo sio zuri,but kumuoa ni ndoto za mabint wengi,huna haja ya kuwa kichaa,jaribu kumuuliza sababu kama iko nyingine akionesha ukaidi achana nae!Huo ndo utakua uamuzi wa busara kwako!

Acha kuumiza kichwa chako kwa mtu asiekupenda mkuu...achana nae na tafuta akupendae kwa dhati.

hapo hakuna mapenzi wewe chapa mwendo tuu tafuta wa kukufaa na kufunga ndoa nae
maana inavyoelekea hapendi kufugwa fugwa na ndoa

Mapenzi hayana kanuni na kila mmoja alikua na malengo yake ktk huo uhusiano wenu hakywa tayari kwa ndoa achana naye

Mm nipo kidogo na mtazamo wa wenzangu ninachoweza kukwambia hebu jalibu kumfatilia ujue kwann au ni sababu zip ninazomsababisha yeye kukataa kuingia kwny ndoa. Unaweza kukuta ni mdogo kiumri au anawashaur wabaya au pengne anamtu ambaye anamsababisha usifungenae ndoa au ni tegemez kwao hvyo anaogopa akiingia kwny ndoa itakuwa ameitenga familia. Na namna ya kuweza kumjua mtu kama huyu jalibu kuondoa suala la ndoa katika akili yako na ujalibu kumfatilia mara kwa mara anamawazo gan. Japo itachukuwa muda lakn kama unampenda utafanikiwa kumteka akili lakn lazma ujishushe kwanza kwake

kaa nae muongee uweze kuelewa nini kimemsibu maana inawezekana wewe ni tatizo au yeye ni tatizo au wote ni tatizo

jamani wana jf nina mpenzi wangu tumekaa nae kwenye uhusiano kwa muda wa miaka miwili na tulikuwa tunapenda sana ila muda ukafika nikaamua nianze mikakati ya kuoa,nilipomwambia tu kuhusu ndoa akaanza kupunguza uhusiano wetu mpaka sasa amesema tuachane
nifanyeje na ninampenda na sina mtu mwingine kwani nilimtegemea yeye?
Mshukuru Mungu

Kusoma hujui, napicha nayo huoni!!!

Labda ameona hawezi kuishi na wewe maisha yake yote, siyo taip ya mume ampendaye, shukuru Mungu usilazimishe ndugu

nkuulize msani we mwanamke au mwanaume? matukio mengi kama haya huwakumba wanawake ni nadra sana mwanamke akatae ndoa, tupe gender yako, hata hivo usinganganie penzi kwani ndoa ni hiyari na kila kitu kina tarehe ya kwisha mda wake, tafuta mwingine na shukuru mola hujui kakuepeushia nn

sa si amesema muachane we untaka nni zaidi..................utashauriwa umbembeleze mwisho wa siku bomu linakulipukia

Acha kuumiza kichwa chako kwa mtu asiekupenda mkuu...achana nae na tafuta akupendae kwa dhati.

We unadhan ni rahisi hivyo

vipi salio la intanet kimeisha nini mbona haupo tena mkuu msani..
ingekuwa mimi zamani sana nilishamuweka trash na subiri lini nikatupe uchafu..

Kama unaona anakufaa na anakufikisha si ungemuoa yeye, sasa umemtosa halafu unataka akushobokee. Acha kumgeuza mwenzako kama fungu la nyanya alaaa.
jamani wana jf nina mpenzi wangu tumekaa nae kwenye uhusiano kwa muda wa miaka miwili na tulikuwa tunapenda sana ila muda ukafika nikaamua nianze mikakati ya kuoa,nilipomwambia tu kuhusu ndoa akaanza kupunguza uhusiano wetu mpaka sasa amesema tuachane

nifanyeje na ninampenda na sina mtu mwingine kwani nilimtegemea yeye?

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom