galatia
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 342
- 828
Wana jamvi habari za jioni?
Nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi sita, nilimpata mchumba kupitia Love Connect. Tumekuwa na mahusiano mazuri tu na tulipanga hata kutambulishana kwa wazazi. Katika mahusiano yetu tulikubaliana kutokusex mpka tutakapo funga ndoa, tumekuwa waaminifu kutunza makubaliano yetu kwa muda wa miezi minne.
Baada ya hapo akaanza kung'ang'ania nimpe tunda lakini sikuwa tayari kwasababu huu ni msimamo wangu wa muda mrefu. Amekuwa akinitishia kuniacha Mara kadhaa kama nitaendelea kumkatalia, sikujali niliendelea na msimamo wangu.
May Mosi alikuja nyumbani kwangu tukaongea mengi, baadae akanitaka nimpe tunda sikuwa tayari. Nilipokataa alinitukana na kuniambia ana wanawake wengi tena wanampa penzi kila atakapo kwahiyo hana haja na mimi tena.
Maneno yale yaliniuma sana, zaidi nilijilaumu kupoteza muda nikijua nina mchumba kumbe hakuwa na nia ya dhati. Zaidi tulishafanya mengi pamoja ikiwa kujenga nyumba ambayo tulishapauwa. Uzuri nyumba tulijenga kwenye kiwanja changu, sasa ananijia juu anataka nimrudishie pesa yake aliyotoa kwa ujenzi.
Nilipo sina pesa ya kumrudishia na yeye anadai nisipo mrudishia mpaka June 12 atauza nyumba tugawane pesa na mimi sipo tayari kwa hilo. Nipo njia panda sijui cha kufanya naomba ushauri wenu please.