Amchoma mkewe kisu kwa kuhisi kaambukizwa ukimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amchoma mkewe kisu kwa kuhisi kaambukizwa ukimwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WANANDOA wawili majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, wamejikuta wakiishia hospitali ya Mwananyamala baada ya mume kumcharanga kisu cha tumboni mkewe na kisha na yeye kujichoma kisu tumboni kutokana na hasira baada ya kuhisi mkewe amemuambukiza ukimwi.
  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana huko maeneo ya Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam ambapo wanandoa hao waliokolewa na wasamaria wema na kupelekwa hospitalini.

  Imedaiwa na mashuhuda wa tukio hilo kuwa, wanandoa hao walionekana nje ya nyumba ya kulala wageni na mume huyo alimchoma kisu mkewe kwa hasira na watu waliokuwa wakaribu waliwahi kumzuia mwanaume huyo kwa kuwa alitaka kuendelea kumcharanga kwa kisu mkewe huyo.

  Alipoona anazuiliwa na watu kuendelea kumshambulia mkewe, mwanaume huyo alichukua uamuzi wa kujichoma kisu cha tumbo yeye mwenyewe kwa kuhisi mkewe huyo alikuwa amekufa na ndipo wasamaria waliporipoti kituo cha polisi na wawili hao kukimbizwa hospitalini.

  Hata hivyo maelezo ya awali yaliyopatikana yalidai kuwa mume huyo alipandwa na hasira kwa kugundua kuwa mkewe wake huyo alikuwa ni muathirika na alikuwa akiishi na ugonjwa huo bila yeye kutambua.

  Hasira zake zilimpelekea kufanya hayo kwa kuwa alihisi na yeye alishaambukizwa na mke wake huyo.
   
Loading...