Amchinja Mkewe na Kwenda na Kichwa Chake Baa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amchinja Mkewe na Kwenda na Kichwa Chake Baa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280


  [​IMG]

  Mwanaume mmoja wa nchini Hispania alimchinja mkewe na kukiweka kichwa chake kwenye begi na kwenda nacho baa kunywa pombe huku akiwatambia marafiki zake kuwa amemchinja mkewe. Mwanaume huyo wa nchini Hispania alikunywa pombe na marafiki zake baa huku akiwa na kichwa cha mpenzi wake kwenye begi.

  Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la kila siku la nchini humo la ABC Daily, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 34, aliwatambia marafiki zake aliokuwa akinywa nao pombe kwenye baa moja mjini Cordoba, kusini mwa Hispania kuwa amemchinja mkewe mwenye umri wa miaka 30 na kichwa chake kipo kwenye begi alilokuwa amelibeba.

  Kwa jinsi alivyoonyesha utulivu hakuna mtu aliyemuamini mwanaume huyo kuwa amemchinja kweli mkewe pamoja na kwamba nguo zake zilikuwa na madoa ya damu.

  Taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo lililotokea jumanne wiki hii zilisema kuwa mwanaume huyo baada ya kupata ulabu na marafiki zake, alitoka nje ya baa na kuparamia mlingoti wa umeme wenye urefu wa mita 30. Alipigwa shoti ya umeme akiwa kileleni baada ya kugusa waya wa umeme alidondoka chini na kupelekea kifo chake alipofikishwa hospitali.

  "Muda mfupi baada ya watu kuanza kuondoka baa waliona dimbwi la damu barabarani na ndipo walipogundua kuwa mwanaume huyo hakuwa akitania, waligundua begi pembeni ya baa likiwa na kichwa cha mke wa mwanaume huyo", ilisema taarifa ya gazeti la ABC Daily.

  Polisi wamethibitisha kuugundua mwili wa mwanamke aliyechinjwa na pia walithibitisha kuwa muuaji wake aliyetambulishwa kwa herufi za majina yake MRTR alifariki dunia hospitalini baada ya kudondoka toka kwenye mlingoti wa umeme.

  Pembeni ya mlingoti wa umeme walikuta kisu ambacho kinaaminika kilitumiwa na mwanaume huyo kumchinjia mkewe, ilisema taarifa ya polisi.

  Polisi wanaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo.

  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Jamani tauacheni mambo ya ulevi sio mzuri Ehhh Kasheshe mtu unamchinja mke wako!!!!!!!!!!
   
Loading...