Amchana mwanae na viwembe mdomoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amchana mwanae na viwembe mdomoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE Salima [28] amejikuta akipelekwa kituo cha polisi na mume wake baada ya kumchana mwanae na kiwembe mdomoni.
  Salima alipelekwa kituoni baada ya mumewe kukasirika na kitendo alichokifanya cha kumuadhibu mtoto kwa kumchana na viwembe

  Salima alichukua umamuzi huo, baada ya mtoto wake huyo kumtukana tusi la nguoni na kushikwa na jazba na kumuadhibu kwa nia hiyo ili iwe fungisho kwa mtoto huyo asirudie kutamka tusi hilo

  Alichukua uamuzi huo wa kumuadhibu mtoto huyo wa kumzaa mwenyewe kwa kukasirika na kutamka tusi ambalo hakutegemea kama angetamka mtoto wake huyo

  Aliagiza kiwembe dukani na kuanza kumchana na kiwembe katika midomo yake hali iliyopeleka kuzua varangati kati ya wazazi hao wawili baada ya baba kushindwa uvumilivu kuona mwanae anaugulia kwa maumivu ya vidonda

  HAta hivyo mume wa mwanamke huyo aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na mwanamke huyo kutakiwa kufika kuituoni kwa mahojiano

  Mtoto aliyejeruhiwa na mama yake huyo alitambulika kwa jina la Ramadhani [6.5]
   
Loading...