Amchana mtoto wa mdogo wake kwa viwembe mwilini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amchana mtoto wa mdogo wake kwa viwembe mwilini

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja mkazi wa Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam, anashikiliwa na polisis kwa tuhuma za kumkatakata mtoto wa mdogo wake mwilini kwa kutumia wembe.
  Mwanamke huyo anashikiliwa katika kituo cha Buguruni ambapo alifikishwa hapo jana baada ya polisi kupata taarifa hizo.

  Kituoni hapo kulidaiwa kuwa polisi walipata taarifa hizo kutoka kwa walimu anaposoma binti huyo anayeitwa Rukia Kassim anayesoma darasa la saba katika shule ya Buguruni Kisiwani.

  Maelezo aliyotoa Rukia kituoni yalidaiwa kuwa alipatwa na dhahama hiyo baada ya kusahau kufunga mlango nyumbani kwao hapo alidai.

  Awali kabla ya mama yake mkubwa kufikishwa kituoni hapo, Rukia alionekana kama mgonjwa na wanafunzi wenzake na alipohojiwa na wanafunzi wenzake ndipo alipowadokeza kwua alikuwa amejeruhiwa na mama yake mkubwa anayeishi nae nyumbani ka kuchanwa na viwembe baada ya kusahau kufunga mlango.

  Ndipo alipowafunia sketi aliyovaa na wanafunzi wenzake hao kuona majeraha na kuogopa na kwenda kutoa taarifa kwa walimu wao shuleni hapo.

  Alipofikishwa kwa walimu ndipo alipowasimulia kuwa usiku wa juzi wa tukio mama yake huyo alimgombeza kwa hasira kwa kusahau kufunga mlango nipo alipoanza kumpiga kwa makofi akaona haitoshi akachukua na wembe kuanza kumchanachana nao mwilini.

  Walimu wa shule hiyoi walipokea tarifa kwa masikitiko kwa kuwa binti huyo alikuwa ni yatima na mama yake huyo mkubwa ndio alikuwa mlezi wake toka aondokewe na wazazi wake.

  Hivyo polisi wanaendelea kumshiklia mama huyo na binti huyo alipatiwa fomu ya matibabu na anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Amana.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4217502&&Cat=1
   
Loading...