Ambwagia mtoto kwa kutopewa fedha za matumizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ambwagia mtoto kwa kutopewa fedha za matumizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Mwanahamisi Shomari [25], mkazi wa Temeke Sandari, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kutelekeza mtoto wa miezi minne nyumbani kwa mzazi mwenzake. Tukio hilo limetokea jana mishale ya saa 3 usiku, huko katika maeneo ya Mtaa wa Mkogo, Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam.


  Akisimulia tuiko hilo kwa waandishi wa habari jijini, Kamanda Sabasi amesema kuwa mwanamke huyo alimchukua mwanae huyo wa miezi minne na kwenda kumtupa nje ya nyumba anayoishi mzazi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Msiro [29].

  Amesema baada ya muda majirani walisikia sauti ya mtoto akilia kwa sauti ikiashiria kuwa hakukuwa na mtu karibu ya mtoto huyo.


  Ndipo majirani hao walipotoka nje na kumkuta mtoto huyo na kumtaarifu kijana huyo na kijana huyo kutoka na kukuta mtoto wake na kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kilicho karibu naye.


  Polisi walifanya msako wa kumsaka mwanamke huyo na kupatikana na kuhojiwa ni kwanini alifanya kitendo hicho na kuieleza polisi kuwa “kweli mtoto huyo ni wangu ila sikumtupa naomba nisamehewe, ila nimeamua kufanya kitendo hicho kwa kuwa Ramadhani amenitelekeza toka anizalishe motto huyo, hanihudumii hata ukimpigia simu anaahidi tu ila hatekelezi lolote, na hampelekei fedha za matumizi”


  Ndio mana nimeamua kufanya kitendo hicho kwa kuwa mimi sina uwezo wowote wa kumuhudumia mtoto huyo na yeye alinilazimisha nishike mimba anamtaka mtoto sasa nashangaa hanihudumiii”  Kamanda Sabasi amesema mtoto huyo amechukuliwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili kwa ajili aende kulelewa huko na polisi wanaendelea kuwashikiliwa wazazi hao kwa mahojiano ya kina.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3563910&&Cat=1
   
Loading...