Ambrose Dunga: Producer aliyezivunja vunja Bongo Records, MJ Records kwa ma-beat makali yenye 'back vocals'

Huyo dogo ndio yule kwenye ngoma ya Komaa Nao anachanika verse ya pili kutoka mwisho (kabla ya Snare) anasema:

Ni mkoleza moto namna hiyoo..
Upanga mashariki kisiwa cha burudani...
Hamfanani na sisi tunavovaa...
Hamfanani na mimi ninavong'aa...
Sijidai hata kwetu nikila pilau...

Ndio huyo dogo?

Ama ni yule kwenye ngoma hiyo hiyo anafoka:

We muongo usizushe...
We mtata ah ah usiniguse..
Chora mstari nivuke, niruke...
Mwingine aige apasuke...
Huyu ni Sharifu alikuwa ana staili ya kuimba mashairi ya kibabebabe hivi,nilipenda sana staili yake. Huyo anayemzungumzia mdau hapo ni Stan Boy ameimba pia na AY katika wimbo Wa "Mademu watafutaji" kama sikosei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio huyo kwenye komaa nao.

Huyu Stand Boy alikua kama anafanya r&b zaidi, sidhani kama amewahi rap.

Skiliza 'itikadi zetu ni kusaka mshiko', ameimba chorus humo then akapiga ka bridge flani kabla ya verse ya mwisho ya wimbo ambayo imeimbwa na GK

Sent using Jamii Forums mobile app
Stan Boy ndugu siyo Stand. Yeah dogo alikuwa anaimba rnb hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka habari za jmosi.
Kuna comment yako moja naona umeifuta.
Reason behind? Umegundua kuwa ulikunya pumba?
hukunielewa mkuu, comment yangu ilikua kukupongeza ila kinyumenyume. Niliandika 'NDO MAANA WATU WANAKUSHUTUMU MWANAUME KUTOKANA NA MAMBO UNAYOANDIKA IKIWEMO TOPIC HII YA DUNGA UMETUMIA KNOWLEDGE KUBWA TOFAUTI NA WANAWAKE WENGI WANAVYOFUATILIA MAPRODUCER WA MZIKI'
So nilikusifu tu wala sikukushutumu kama ulivyodhani. Ila sorry maana hili jambo laonekana limekukera.
 
hukunielewa mkuu, comment yangu ilikua kukupongeza ila kinyumenyume. Niliandika 'NDO MAANA WATU WANAKUSHUTUMU MWANAUME KUTOKANA NA MAMBO UNAYOANDIKA IKIWEMO TOPIC HII YA DUNGA UMETUMIA KNOWLEDGE KUBWA TOFAUTI NA WANAWAKE WENGI WANAVYOFUATILIA MAPRODUCER WA MZIKI'
So nilikusifu tu wala sikukushutumu kama ulivyodhani. Ila sorry maana hili jambo laonekana limekukera.

Nimekusoma nimekusoma kiongozi!
Unatumia browser ku-access JF?
Unaionaje hii "outlook' mpya. Mie sijaipenda kwa kweli. ipo ovyo ovyo
 
Nimekusoma nimekusoma kiongozi!
Unatumia browser ku-access JF?
Unaionaje hii "outlook' mpya. Mie sijaipenda kwa kweli. ipo ovyo ovyo
Japo aliyeulizwa si mimi, lakini najibu swali, mabadiliko sio romantic kabisa. Natumia browser naona muonekano huh hauko poa, wameondoa mpaka zile trending thread, na hata aina ya maandishi (font) sio nzuri. Iliyoondolewa ilikuwa nzuri sana kuliko hii mpya
 
Bila shaka back vocal ya chege nyimbo ukimuona mwanayumba ile vocal pale mwisho kasimama yeye inakwenda ivi MWANAYUMBAAAAAA kuna vocal la kibabe pale ni dunga yeye bila shaka√√√√√√√ hatari sana.
 
Japo aliyeulizwa si mimi, lakini najibu swali, mabadiliko sio romantic kabisa. Natumia browser naona muonekano huh hauko poa, wameondoa mpaka zile trending thread, na hata aina ya maandishi (font) sio nzuri. Iliyoondolewa ilikuwa nzuri sana kuliko hii mpya
Hata app hivyohivyo tu

Time will Tell!
 
Timberland mtu mbaya sana kwenye beat na back ground vocal.
Kwenye beat yeye na Dr. Dre wana kitu flani cha kipekee, ile ukisikia tu unajua huyu flani.

BTW, umechambua vizuri sana.
Unaijua game ya muziki kama wadada flani amazing, Salama Jabir na Dj Fetty.
Nahisi wewe ni mmoja wa hao wadada, hiyo rangi yako kwenye pic uliyo tuma, white flani kama ya Dubai na uelewa wako wa game ya music ndiyo vimenishawishi kukufaninisha na hao watu.
Dj Fetty!? Acha mzaha Ndugu. Anajua nini?
 
Mkuu mimi sijaridhika kabisa Mama Debora kumfananisha Timbaland na producer yoyote. Kwenye swala la production "Timbaland is a God" hana wa kufananishwa nae! Mimi nina collection ya nyimbo zote alizo produce huyo jamaa. Kuna wimbo mmeusahau wa Missy Eliot unaitwa "Cant stand the rain" daaah yule jamaa ni mtu mbaya sana.

"The Rain (Supa Dupa Fly)" by Missy Elliott sampled Ann Peebles's "I Can't Stand the Rain". Hii ndio Moja kati ya ngoma Kali nazozielewa kutoka kwa Missy Elliot.
 
Huyu jamaa aliwagongaga beat kali sana kwenye 'itikadi zetu' ya East Cost.

Pia kuna dogo mmoja mwenye melody nzuri sana aliyefanya chorus ya itikadi zetu nadhani alikua anaitwa 'Stand boy'(kama skosei). Huyu bwana mdogo alifanyiwaga beat moja very heavy na huyo Effector kwenye wimbo wake 'sweet girl'...sijui huyu bwana mdogo alikujaga kuishia wapi

Sent from my TECNO B1f using Tapatalk
Huyo dogo nilisikia alienda zake USA
 
Jana usiku wakati nachapa code za JavaScript (hii language siipendi basi tu!!) huku nasikiliza album ya Joyner Lucas -ADHD kuna wimbo mmoja unaitwa 10 Bands uli-popup. Ndani ya ngoma hii ameshirikishwa the Legend Producer Timberland.

View attachment 1451643

Kwa ambao hamumjui producer Timberland tafuteni ngoma za marehemu Aaliyah (sio huyu wa Wasafi), Aaliyah msanii aliyefariki kwa ajali ya ndege akiwa na crew yake wakitoka ku-shoot video ya "Rock the Boat" kule visiwa vya Bahamas. Karibu 98% ya nyimbo za Aaliyah zilitengenezwa na legendary Timbeland 'Mzee wa Back vocals'.

Karibu nyimbo zote alizotengeneza Timberland, kuna kitu 'common' na very 'unique' kwenye beats za Timberland, zile 'back vocals' ambazo alikua anaimba Timberland mwenyewe. Okey tufanye hivi, tafuta nyimbo zifuatazo sikiliza halafu utagundua nachoongelea:

Aaliyah - Try Again
Aaliyah - Are you that somebody
Aaliyah - More than a woman
Justin Timberlake - My love
Missy Elliott - Get Ur Freak On (Napenda zile back vocals 'Piki piki donsee')
Ginuwine - Same OL G (Aisee ukiwa na stress sikiliza hii ngoma, Timberland nyoko!!)

Sikiliza beats za hizo nyimbo hapo juu. Umesikia hizo back-vocals? Basi huyo ndio Timberland mzee wa ma-beat!

Hii ikanikumbusha miaka ya 2004 mpaka 2012 kipindi Bongo Records na MJ Records bado wanatawala 'music production industry' ya Bongo, kuna producer Mkenya alikuja kuleta mapinduzi akawavunja vunja kina P-Funk Majani na Master Jay wakapotea kwenye production ya muziki wa Bongo-Fleva mpaka kesho!!

Unakumbuka miaka ya 2005 - 2010 karibu kila ngoma mpya ya Bongo-Fleva unasikia wanataja "Mandugu Digitoooo" au wakati mwingine unasikia "41 Recordssssss". Kama umesahau basi sikiliza ngoma ya Prof. Jay "Hapo Vipi" au ngoma ya Mwasiti na Chid Benz "Hao" utasikia hizo jingles. Nyuma ya pazia alikuepo 'Timberland wa Bongo' Ambrose Dunga.

Jamaa kwa muonekano ni kama mshamba mshamba hivi, lakini kazi zake zilikuwa ni nyoko!

Unaikumbuka ngoma ya Nakaaya - Mr. Politician? Basi yule 'Mr. Politician' kwenye video ndio Producer Dunga huyo! Unacheki alivo na msuti ule!! Mshamba kweli.

View attachment 1451649

Fanya hivi, angalia video ya Matonya - Anita pale beat linaanza yule anasema "Tusichongole chongole" ndio Producer Dunga huyo. Umecheki anavookena mshamba na hilo Tishet lake la njano nyuma ya nyumba yenye ukuta wa tofali za kuchoma halafu inataka kubomoka?

View attachment 1451647

Ikafika kipindi wasanii wote waliokua wateja wazuri wa Bongo Records na studio zingine wakawa wanamiminika Mandugu Digital. Producer Lamar nae akaona isiwe tabu, akamkimbia P-Funk ajifie na Bongo Records yake akaenda kuongeza maufundi kwa Producer Dunga. Aisee Lamar na Dunga waliunda 'Duo" moja kali sana.

Akina Prof. Jay wakaona isiwe tabu, wakafuata midundo yenye "back vocals' kwa 'Timberland wa Bongo'. Marehemu Ngwair aliyekua msanii 'Loyal' kwa P-funk na yeye akaona isiwe tabu. Kwanza alikua ameshapotea hasikiki tena, lakin alivoenda kwa 'Timberland wa Bongo' ndipo akaja na "Nipeni Dili Masela" ndio akarudi kwenye mainstream. Hii ngoma ukisikiliza zile 'back vocals' za Dunga utaelewa kwanini Dunga namfananisha na "Timberland wa Aaliyah"

Chini ni baadhi ya ngoma zilizopikwa na producer Dunga akisaidiwa na Lamar (kabla ya kuiva na kuunda 'Fish Crab'):

1. MB Dogg - Natamani (Kule mwishon Dunga anaimba "dumba dumba dumba dumbe")
2. Mwasiti ft. Chid Benz- Hao (Utamsikia Dunga anaimba "Tunadunda dunda duundaaa")
3. Nakaaya - Mr. Politician (Utamsikia Dunga "Nipeni kura zenu.. Nivotieni.. Put your hands up")
4. Prof Jay - Hapo Vipi
5. Ngwair - Nipeni Dili
6. Nako 2 Nako ft Loon - Bayeyo (beat linadunda hili ni nyoko)
7. Matonya - Anita (Tusichongole chongole)
8. Noorah - Baba styles
8. Ngwair ft. TID - She Performs ("Thi..This should be played at high volume")
9. Temba ft. Ray C - Nipe Mimi
10. Fatma ft. Jay Moe - Chozi la kusimuliwa

Kila kitu kina muda wake. Nani anaikumbuka match ya EPL iliopewa nickname ya "Battle of the Buffet"?

October 29, mwaka 2004 katika uwanja wa Old Traford, mabao mawili kutoka kwa Ruud van Nistelrooy na Wayne Roon yali-hitimisha "49 unbeaten record" ya washika mtutu wa London Arsenal. Mechi hiyo ilitawaliwa na vurugu kama zoteee. Hadi kupelekea Cesc Fabregas kumrushia kipande cha Pizza kocha Alex Ferguson wakat wanatoka uwanjani. Na ndio sababu ya mechi hiyo kubatizwa "Battle of the BUffet".

Leo hii May 16, 2020 mechi kati ya Man U na Arsenal inaonekana kama Aston Villa anacheza na Norwich. Mechi haina tena impact. Hakuna ile amsha amsha kama ya 2004.

Kila kitu na muda wake. Battle of the Buffet imehamia kwa Man City vs Liverpool.

Producer Dunga hatimaye (sijui kwa sababu zipi) alisepa Bongo akarudi kwao Kenya.

Lamar nae akafungua Studio yake Fish Crab. Uzuri akaendeleza ufundi aliopata kutoka kwa 'Timberland wa Bongo' kwa kutengeneza beats za kipekee zenye identity, zenye "back vocals' na jingles. Ukisikia tu "Talk of the town... Lamar.. Aaaaaaaaauu" unajua huyu ni Lamar.

Siku hizi mambo yamebadilika. Hakuna tena 'monopoly' ya music production.

Studio na Producers wamejaa Bongo yoteee... Hakuna tena 'Timberland wa Bongo' kama ilivokua miaka hiyo.

Ngoja niendelee kusikiliza ngoma za Joyner Lucas hapa, kuna ngoma inaitwa Will. Anamsifia na kumu-appreciate mwanamuziki na muigizaji Will Smith akielezea kuwa Will Smith ndio 'Role Model' wake tangu enzi hizo Joyner Lucas ana struggle kutoka.

Ingia Youtube search Joyner Lucas - Will, uone alivojivika uhusika kwenye movies za Will Smith alizoigiza zamani!!

-------- UPDATES--------
Kuna mdau kachangia amesema Dunga yupo Tanga bado anafanya production (japo sio intensive kama enzi zile). Nimeangalia video ya msanii Galatone - Samaki (ipo Youtube) nimemuona Dunga kama kawaida yake na 'back vocals' :D :D:D:D
View attachment 1451874


-------------UPDATES 2--------------
Asante mdau josephmasamaki kwa kunipa update nilikua sijui kama ngoma ya Chege na Temba - Go Down ya mwaka 2017 imetengenezwa na Dunga. Nimeicheki Youtube 'back vocals' zake kama kawaida. "Mama yanguuu.. Tembelee"
Dunga ananifurahisha sana halafu amekula suti kaliii :D :D:D
View attachment 1452188

Mama Debora
Unajua wanawake kama ww ni adimu maana unajua history ya Music kuna mmoja nlikutana nae yan ww kaeka like it anajiangalia anavokatika nkaona dah sio poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jina la yule jamaa alikuwa anaitwa Stan Boy, kuna video aliiweka youtube mwaka 2009 akiwa USA, alikuwa anatangaza muziki wake na kusema unapatikana myspace.com ambayo kwa sasa haipo file zilikuwa corrupted zote na tovuti ikafa kabisa (hata mimi nilipoteza baadhi ya kazi zangu huko). Ukiangalia video anasema pia anapatikana facebook na site nyingine


Mbali ya track za ECT kama crew pia alifanyaga collabo na AY ile track ya mademu watafutaji

Najiuliza hapa vipi YouTube haiwezi files ku-corrupt na kila kitu kupotea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom