MAPITO Mwanza
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 3,684
- 5,011
Babu tangulia nasi kina Mapito Mwanza twaja ukifika msalimie Mkuu wa maraika mwambie tuna songa ki dgital
AiseePumzika kwa amani Babu wa kikombe cha miujiza.
Wasalimie sana wateja wako waliotangulia mbele za haki
View attachment 1874284View attachment 1874285
Hata wale ambao bado wangali hai watakumiss sana.
View attachment 1874292View attachment 1874293
MWENYE vyeti vya Mirembe alidhani kikombe Cha Babu kinatibu na kuponyesha kichaaDentist wetu alifariki kwa ajali mbaya sana akitokea Liliondo kwenye kikombe cha babu.
Mzee kuona jam inaongezeka, akadai ukinywa zaidi ya mara moja utakufa.Road to hell was paved with good intention...
Kipindi kile biashara hii ililipa kuliko hata utalii na kubeba wazungu.
Tulikuwa tunapeleka watu wamebebwa na madripu yao!
Wengine wako kwenye near death expirience...
Tuapeleka wagonjwa waliolipia go & return ila ukifa sio mgonjwa tena tunachaji km maiti..au huwezi zikia hapo hapo loliondo..
Kiukweli hata mi nilikunywa kikombe tena zaidi ya mara moja.
Ina maana siku hizi magonjwa mengine hayaui??Covid? 😳
Hivi wakati ule nchi nzima na watu wake walikuwa wamelogwa?Pumzika kwa amani Babu wa kikombe cha miujiza.
Wasalimie sana wateja wako waliotangulia mbele za haki
View attachment 1874284View attachment 1874285
Hata wale ambao bado wangali hai watakumiss sana.
View attachment 1874292View attachment 1874293
Alianza kuumwa muda mrefu sana hakuahiriki bunge karibu cha miaka 4Angali hai nadhani. Sina uhakika. Ila sijawahi kusikia tangazo la kifo chake
Wengi waliokwenda kupata kikombe cha babu wana magonjwa yasiyotibika yanayoambukizwa kwa zinaaPumzika kwa amani Babu wa kikombe cha miujiza.
Wasalimie sana wateja wako waliotangulia mbele za haki
View attachment 1874284View attachment 1874285
Hata wale ambao bado wangali hai watakumiss sana.
View attachment 1874292View attachment 1874293
Apumzike kwa Amani
Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo amefariki dunia akipatiwa matibabu Kituo cha Afya cha Digodigo baada ya kuzidiwa gafla leo Mchana. Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro, Waso.
Babu wa Loliondo aliugua muda mrefu na kujitibu kwa miti shamba, alipoenda hospitali akiwa amechelewa.
Babu wa Loliondo alipata umaarufu kwa dawa yake aliyodai inatibu magonjwa yote.
Alikuwa na akili kubwa kuwazidi watu wengi "create fear you will make money "hapo padogo tu aliwashika masikio watu kibaoPumzika kwa amani Babu wa kikombe cha miujiza.
Wasalimie sana wateja wako waliotangulia mbele za haki
View attachment 1874284View attachment 1874285
Hata wale ambao bado wangali hai watakumiss sana.
View attachment 1874292View attachment 1874293
Eeh!later ni mingapi kama soon ni 86years?Gone too soon....!
Top 5 ya wapigaji au waponyaji?Kwenye top5 yngu huyu ni #1
Ova
R.I.P Mchungaji.Ninalolikumbuka kwake ni moja tuu kwamba kumbe Tanzania tulikuwa na wagonjwa wengi sana waliokuwa majumbani.maana si kwa umati ule
Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo amefariki dunia akipatiwa matibabu Kituo cha Afya cha Digodigo baada ya kuzidiwa gafla leo Mchana. Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro, Waso.
Babu wa Loliondo aliugua muda mrefu na kujitibu kwa miti shamba, alipoenda hospitali akiwa amechelewa.
Babu wa Loliondo alipata umaarufu kwa dawa yake aliyodai inatibu magonjwa yote.
=======
UPDATE: July 30, 2021
Chanzo cha kifo cha Mchungaji Ambilikile Mwasapile (86) kimetajwa aliugua nimonia kali ambayo ilimsababisha kupata tatizo la upumuaji na homa.
Tangu afariki wasaidizi wake na majirani wamekuwa wakieleza kushtushwa na kifo hicho ambacho kimetokea akiwa anaendelea kutoa huduma ya tiba ya kikombe aliyoanza tangu mwaka 2011.
Mchungaji Ambilikile ambaye ataendelea kukumbukwa kwa kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2011 hadi 2013 kutokana na tiba yake ya kikombe alifariki jana saa 9:45 jioni.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala amesema kuwa taarifa za awali za madaktari zinaeleza chanzo cha kifo ni nimonia ambapo kwa takriban siku tano alikuwa anaumwa na kupata sindano za masaa.
"Jana asubuhi aliamka vizuri akiendelea na matibabu lakini majira ya saa nane alianza kujisikia vibaya ndipo ilitafutwa gari kutaka kumpeleka hospitali ya Wasso ambaye alitaka,"amesema
Hata hivyo amesema wakiwa wanampandisha gari alijisikia vibaya na kuanza kutapika ndipo walimkimbiza kituo cha afya Chadigodigo na alifika akiwa tayari amefariki.
Baadhi ya wasaidizi wa mchungaji Mwasapile walisema kabla ya kuzidiwa na ugonjwa alikuwa akiendelea kutoa tiba ya kikombe kwa wagonjwa kadhaa ikiwepo wa corona.
Hivi karibuni akizugumza na vyombo vya habari Mwasapile aliomba kupelekewa wagonjwa wa corona kupata tiba kwani hakuna ugonjwa ambao Mungu unamshinda.
"Wiki mbili zilizopita alikuwa vizuri anatoa tiba japo kwa watu mmoja mmoja waliokuwa wanakuja lakini hali yake iliendelea kubadilika," amesema.
James Richard jirani wa Mchungaji huyo amesema hadi anafariki hakuwa na hali mbaya na ameacha mali kadhaa ikiwepo magari, nyumba na kiwanja ambacho alikuwa anaandaa kwa kutolea tiba
"Babu bado alikuwa anasema watu watakuja Samunge maelfu kupata tiba na alipata eneo kubwa ambalo alikuwa anaendelea kuliandaa,"amesema.
Mmoja wa waliowahi kuwa wasaidizi wababu wake Poul Dudui amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa kwa uratibu wa Serikali na wanasubiriwa ndugu na watoto wake kujua atazikwa wapi na lini.
James Leyani mkazi wa Loliondo, amesema msiba umetokea wakati kuna janga la corona na kuna chanjo imeanza kutolewa hivyo muhimu watu kusikiliza maelezo ya wataalam wa afya na Serikali.
"Tunakubaliana na tiba za asili na imani lakini sasa muhimu kufuata maelezo zaidi ya wataalam wa afya na Serikali ili kukabiliana na janga hili,"amesema.
Hiyo si hoja, cha msingi ni kwamba anapokea rambi rambi, hivyo aweke account number yake hapa au namba za simu kazi ianze!!Wewe ni mwanae au mjukuu wake?