Ambaye ana uzoefu na biashara za Dar-Zanzibar

Basmati rice..

Sio kweli sana mkuu. Ule ni kwaajiri ya mapishi ya biriani. Ila unapotaka kupika pilau au wali wa kawaida then mchele mzuri ni huu wetu wa bara especially ile mbegu ya Mchele wa mbeya au shinyanga huwa inadatisha sana.

Yuko sahihi Zanzibar mchele ni basmat kwa pilau na birian wali wa kawaida ambao ndio chakula cha kila siku mchele unaotumika ni jamsin rice kutoka Asia
 
Mkuu Zanzibar nauli Tsh 60,000 kata maji ukajionee mwenyewe.

Hivi karibuni nilikuwa Handeni, nilikuta kuna wazanzibar wengi tu wanakuja kununua mbuzi minadani. Wanabeba kwenye mafuso mpaka Tanga mjini then wanapandisha boti kwenda Zanzibar.
Mkuu ivi mbuzi tanga bei gani maana kuna chimbo la mbuzi sehumu inaweza ikawa fulusa
 
Mkuu, mimi sina uzoefu na biashara za zenji ila kama uko serious karibu pm nikwambie nini unaweza kufanya haswa kuanzia mwezi wa sita, utakuja kushuhudia hapa..
Kwani ukishare hapa inakuaje mkuu...
Dondosha madini hayo isifanye ubaguzi mapema ivi
 
Huo mchele super kyela kwa dar tu, huwa unafika 3000!!kuna super na suoer kyela!!sembuse zanzibar?au unaongelea kipindi hiki ambapo mchele ni bei ndogo?
huu super kyela ndo ule kama mtamu ivi ukiula na una harufu sana na mafuta futa ivi? Maana nimeutafuta sn huu mchele huku zenji but sijawahi kubahatika kuupata, huwa nakula siku moja moja nikienda kutembea Dar...
 
Mkuu ivi mbuzi tanga bei gani maana kuna chimbo la mbuzi sehumu inaweza ikawa fulusa
Unaweza kununua kwa Tsh 50,000 na ukauza hapo hapo kwa Tsh 65,000 hapo hapo mnadani kutegemeana na ukubwa wa mbuzi.

Kwahiyo unaweza kusafirisha kuleta Dar au kupeleka Zanzibar ukapata zaidi.
 
Shukrani snaa, nimekuwa nikiutafuta sana huu mchele na jina lake, ila nimeukosa..nazani hii mbegu imeanza kuadimika....mwisho wa siku nimeamua kuula wa Shinyanga tu, mana kuna muuzaji mmoja alinishawishi kwmb na wenyewe sio mbaya, na kweli ni mchele mzuri ila haujafikia hiyo kyela.
Ni kweli mkuu ata wa shinyanga ni mzuri Ila wa kyela ni special, ule ukipika nyumba nzima inanukia wali, tofauti kidogo na mchele mwingine mtu kujua kama Unatoa hashimu lungwe hadi aone umepalia Moto juu ya mfuniko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom