Ambatana au kaa karibu na Watu ambao wanaweza kukupa ramani ya mafanikio!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,518
6,497
Ni mazungumzo ya vijana wawili wanao fahamiana...ni uwanjani katika mchezo wa soka pale kitaa cha Tabata. Jioni hiyo niliamua kwenda kucheki mazoezi ya mpira kwani kiwanja Hicho hakipo mbali Sana na ninapoishi.

Na haya ndio mazungumzo Yao:
Kijana wa Kwanza '' Kaka hiyo fani yako ya umeme vipi umeshaifanyia kazi kidogo au bado?''
Kijana wa Pili '' bado Kaka..nilikuwa mkoa lkn hakuna Mishe Mishe yoyote ndo bro kaniita huku dar nije tufanye biashara''
Kijana wa Kwanza '' kwahiyo Kaka utasomeaje kitu halafu usikifanyie kazi huoni hapo utakuwa kama umepoteza Ada ya bure Tu?''

Mpaka hapo Kwanza hawa jamaa kama wakawa wamenifanya nifuatilie mazungumzo Yao Kwa karibu kidogo. Ikanikumbusha dada yangu ambaye alisomea wild life pale Sokoine University na mapaka Leo hajafanyia chochote Ile bachelor yake..na haya huwatokea watu wengi Tu..alichosomea Sicho anachokifanyia kazi sasa!

Msemaji wa Kwanza akaendelea na darasa lake ambalo hata Mimi likanivutia..akaendelea ujue mdogo wangu ebu jitahidi kujichanganya na watu wa fani yako huenda wakakupa ramani ya kuanzia na kufanyia kazi kile ulichosomea..unaona Mimi huwa napenda kujichanganya na mabroo ambao najua kabisa huenda wakanipa ramani na muongozo wa wapi nipite na hatimaye nifanikishe mambo yangu.

Msemaji akaendelea ambaye kwasasa naomba nimuite motivational speaker maana si Kwa darasa lile '' Mimi bwana huwezi kunikuta nakaa na watu ambao hawaeleweki eleweki lazima nikae vijiwe ambavyo vina mitazamo chanya na kusaidiana tuinuke katika Maisha yetu''...daah hakika lilikuwa darasa zuri Sana kutoka Kwa yule mdau..nilifaidika Kwa mambo mawili Kwanza kucheki vijana wakifanya mazoezi na pili kupata darasa la bure ambalo huenda wengine wanalipia huko duniani.

Basi akapita muuza kahawa pale tukapiga vikombe viwili vitatu na Mda wa mazoezi pamoja na lile darasa la bure kuisha then tukachapa lapa na kuelekea majumbani kwetu.

Ni hayo Tu.
 
Simulizi yako ni nzuri sana, ila imekuwa fupi sana, ina flow nzuri sana na yenye logic. Content ingekuwa pana, unaiandikia hata kitabu, kwa hakika ni yenye kufundisha. Nakutabiria kuwa, utakuja kuwa mwandishi mzuri sana wa makala na hata vitabu.
 
stars ...ubarikiwe Sana mkuu..asante Kwa maoni na maono yako
 
Simulizi yako ni nzuri sana, ila imekuwa fupi sana, ina flow nzuri sana na yenye logic. Content ingekuwa pana, unaiandikia hata kitabu, kwa hakika ni yenye kufundisha. Nakutabiria kuwa, utakuja kuwa mwandishi mzuri sana wa makala na hata vitabu.

Na kitabu chake kitauza sana,muhimu kutoa nakala za kutosha tu…
 
Back
Top Bottom