Ambaka mtoto wa darasa la sita hadi kumuua, ajisalimisha Polisi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mponjoli Lisa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumbaka binti wa darasa la sita Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni hadi kumuua.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Zuberi Chembela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wanne wanashikiliwa na polisi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Pugu Bombani, Amanzi Bungara amesema tukio hilo limetokea Jumapili Desemba 8, 2019 na kudai kuwa Lisa baada ya kufanya tukio hilo alijisalimisha kituo cha polisi Stakishari na kukiri kufanya kitendo hicho.

“Lisa alikwenda nyumbani kwa huyo binti na kuomba amsindikize dukani na walipokuwa njiani alimfanyia unyama huo. Tumemzika leo jioni katika makaburi ya Mwakanga.”

“Kutokana na tukio hili limewaagiza wakazi wa mtaa wangu kuorodhesha majina ya wapangaji wao ili niwajue, lakini tumepanga kuanzisha ulinzi shirikishi,” amesema Bungara.

Chanzo: Muungwana
 
RIP binti, hivi hawa wanaofanya vitendo hivi wanakuwa na akili kichwani kweli???
 
Halafu wananchi wakiwatoa Uhai shetani kama hao mnaleta ujuaji mwiiingi humu jamvini.
Lkn huko Luanda Mbeya kuna mfungwa wa aina hiii kapewa msaada na Mhe Rais baada ya kukidhi vigezo na kagoma kutoka gerezani.
 
Mbaya zaidi wahalifu wanaachiwa warudi uraiani...huku watakutana na maisha magumu watarudia tu uhalifu...
 
“Kutokana na tukio hili limewaagiza wakazi wa mtaa wangu kuorodhesha majina ya wapangaji wao ili niwajue, lakini tumepanga kuanzisha ulinzi shirikishi,” amesema Bungara.


Brainless
Alikuwa wapi kutimiza wajibu siku zote!?
 
HAKIMU; mtu humiwa jitete
MTUHUMIWA; Mhe hakimu shetani alinipitia tu 😂😂😂 hapa shetani anasingizwa tu.
 
Ndo maana mimi naunga mkono hukumu ya kifo kwa wanaizaya, wana watoka pabaya na kenge wengineo kwa 100%. Unafikiri wazazi wa huyo mtoto hawatamani hao kenge nao wadedishwe? Halafu anajitokeza mwanaharakati uchwara wa haki za binadamu anaanza kutetea hayo mapimbi eti "Ooooh hawa pimbi wana haki ya kuishi..".Swali ni je, hao wabakaji + wauaji hawakujua kuwa huyo binti naye alikuwa na haki ya kuishi?

Nyinyi wanaharakati njaa acheni kutetea majitu ya ajabu ajabu kwa kuwa tu nyinyi hamjawahi kutendewa unyama na hayo majitu.

Mhe.Rais, nakuomba zile hukumu uendelee kuzisaini. Kama huruma imekuelemea basi nakuomba uniruhusu mimi niwe nazisaini. Na kule gerezani kama wanyongaji wamekaribia kustaafu naomba hiyo kazi unipe, na niko tayari kuifanya kwa ujira mdogo ili kupunguza gharama za serikali. Na nitaanza na hao 'pimbi' 4 na kisha yule wa Kigamboni aliyemchoma mkewe kwa magunia 2 ya mkaa, utadhani alikuwa anatengeneza matofali ya kuchoma.

I hate murderers, I hate them bitterly. God hates them too, and He'll cast them in a fiery hell. 😬😠
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom