Amapiano ni Ushamba wa wasanii wetu au fasheni?

Unajua kwanini wasanii wa bongo wanakimbilia amapiano sababu ni mziki ambao hawaumizi sana kichwa kuandika au kutafuta mada ,wanatafuta tuu maneno matatu wanatembea na beat la dakika 4
Yawena ewee , Yibiyiyibi yah, Yibiyiyibi yoo ... hapo umepatia🤣
images (93).jpeg
 
Sijawahi kuielewa Amapiano, japokuwa naona kama midundo hii inatrend Africa kuliko midundo ya Kinaija, ila mimi bado mpaka sasa hamna hata nyimbo niliyo ielewa.
Una matatizo wewe tafta ngoma inaitwa Vula Vala uone balaa lake!

Usipoelewa utakuwa mnywa juisi wewe, siku ukianza ulabu utaelewa!
 
Huezi kumkuta King Kiba anaiga huo upuuzi,. Kuna visanii vinapenda kuigaiga kila kitu ili mradi waonekane wametoa kazi

Kila nchi kuna wasanii wanaimba tatizo naloona kwanini naija na amapiano inafanya vizuri sababu kubwa ni ushirikiano pia kuwa na uchumi kuwa mkubwa South Africa na naija waliacha kupiga nyimbo za wasanii kutoka nchi nyingine ili kukuza mziki wao
Sisi hatufanyi hivyo ndio ata wasanii wanashindwa kuwa na msimamamo
 
Huezi kumkuta King Kiba anaiga huo upuuzi,. Kuna visanii vinapenda kuigaiga kila kitu ili mradi waonekane wametoa kazi
Bora unyamaze huyo mnafiki aliyejaa chuki na wivu, wakati Mondi akitumia biti za kinaija kwa baadhi ya nyimbo zake aliponda sana "...mimi naimba bongo fleva ..naiwakilisha bongo fleva.....king of bongo fleva".

Kavumilia kaona isiwe tabu kuanzia DODO, SALUTE na JELOUS zote biti za kinaijeria, bongo fleva kaipiga kapuni na yeye baada kuponda sana wasanii wanaolipia instagram kwa ajili ya kuzitangaza nyimbo zao, juzi nae kaanza kulipia insta kwa ajili ya kupromoti nyimbo zake ya Jelous.

Huyo ni mnafiki husishangae kesho nae akaimba Amapiano.
 
Kama ndo hela ipo hapo kwenye style za amapiano akuna shida,watu wanatazama fursa iko wapi kisha wanaichangamkia.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
wasanii watanzania kila mmoja kukimbilia kuimba Amapiano ambayo ya SA ni ushamba wa kiwango cha lami.

Nimependa sana Msaanii wa Singeli Kinata MC katoa nyimbo na mwanadada wa Uganda anaitwa Azawi nyimbo inaitwa Do le mi Go remix,
Taratibu singeli imeanza kueleweka East Africa.
Azawi ana ngoma inaitwa quinamino naikubali sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom