Ndugu wanajukwaa na watanzania kwa ujumla, naamini kwa pamoja tunakubaliana kwamba amani ya nchi yetu ni muhimu kuliko mgombea yeyote na nafasi yoyote.
Sasa kutokana na umuhimu wa amani hasa katika kipindi hiki tukielekea kufanya uchaguzi mkuu ili kuwapata viongozi wetu wa kisiasa katika ngazi ya udiwani, ubunge na urais, ni vema watanzania kwa umoja wetu bila kujali mapenzi yetu kwa vyama vya siasa au kwa wagombea, tusimame kama taifa kuhakikisha tunailinda amani yetu kwa gharama ya busara na kusimamia haki.
Najua na kama nilivyosema hapo juu, wengi wetu tuna itikadi za vyama, tuna mapenzi na wagombea fulani na tunatamani washinde kwa uchaguzi huu.
Kuwa na itikadi ya chama au kumpenda mgombea fulani na kutaka ashinde si dhambi na wala haijawi kuwa dhambi.
Lakini ushindi mzuri ni ule wa kushinda kwa haki bila kulazimisha na pengine kupelekea machafuko.
Mgombea wa chama A akimshinda mgombea wa chama B kwa haki, basi sisi watanzania kwa umoja wetu tuutambue huo ushindi na tumpongeze aliyeshinda.
Halikadhalika mgombea wa chama B akishinda basi mgombea wa chama A akubali kuwa kashindwa na isitokee akaona kwamba ni yeye tu ndio anastahili kuongoza taifa hili na akapelekea machafuko kwa kulazimisha ushindi uwe wake.
Mimi naamini wagombea, na tume ya uchaguzi wakijaliwa busara ya kuheshimu matakwa ya wapiga kura basi uchaguzi huu tutavuka salama na pengine hata nchi zingine zitatamani kuja kujifunza kutoka kwetu.
Tukubaliane kwamba wagombea wetu wote bila kujali vyama vyao, lakini wote ni watanzania na wote wanastahili kuongoza nchi yetu.
Asitokee mtu wa kusema eti fulani hastahili kwa vile tu anatokea chama fulani.
Atakayeshinda iwe ni Tanzania imeshinda.
Mungu atujalie tuvuke salama.
Sent from my A37f using JamiiForums mobile app