Amani ni kila kitu katika maisha, kuna watu wana miiba mbalimbali inayowazuia kusonga mbele

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Kulikua na baba mmoja alikua na shamba kuuubwa limejaa miiba. Kila akitaka kulisafisha.. Miiba ilikuwa kikwazo kwake.

Miaka mingi ilipita hakulima shamba lake sababu ya miiba. Kipindi cha njaa kubwa kiliingia kijijini kwake akaamua aliandae shamba lake kwa ajili ya kilimo hata kama miiba ni mikali. -

Akajitahidi kuondoa miiba na kufanikiwa, japo miiba ilimchoma Sana mpaka kutokwa damu na majeraha lakini alikuwa na nia ya kuandaa shamba lake ili asiathirike wakati mwingine wa njaa.

Wakati wa kumaliza kusafisha shamba lile miiba akaichoma moto. Akapanda mazao yake na shamba lake lilivuna Sana na kumletea heshima kijijini kwake. -


FUNZO

Amani ni kila kitu katika maisha, kuna watu wana miiba mbalimbali inayowazuia kusonga mbele.

Labda ni mahusiano yasiyoeleweka au kusumbua, vinyongo, watu kukukwaza kazini kiasi kwamba hupendi kazi yako na hutamani kwenda kazini, madeni mengi, kuchukiwa na watu bila sababu.. nk nk.

Hii yote ni miiba itakutesa sana na kukuacha na vidonda. Kama usipoamua kuichoma utabaki hapohapo na vizuizi.

Andaa shamba lako liwe safi, choma miiba yote.





Mungu Ibariki Tanzania Na Watu Wake.
 
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom