Uchaguzi 2020 Amani na utulivu utawale; Baada ya uchaguzi kuna maisha

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
340
500
Mimi kama raia mwema natambua zimebaki siku 3 kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wetu ninaombea taifa langu livuke kikazwo hiki. Aidha ninatoa wito ufuatao:

1. Kama alivyokwisha ahidi Rais wetu mapema kuwa uchaguzi huu utakuwa wa haki na uhuru naomba vyombo vyote vya serikali na dola kwa ujumla vitimizeajukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na miongozo ya uchaguzi.

2. Vyama na Wagombea nao watimize wajibu wao kwa kuzingatia sheria za nchi na uchaguzi. Iwapo zitakuwa hazikuridhika na mchakato na matokeo zifuate sheria na taratibu nyinginezo kupata haki badala ya kuchukua sheria mkononi

3.Wananchi tuzingatie Amani na Utulivu muda wote kuna maisha baada ya uchaguzi ndugu zangu

4. Atakayeshindwa akubali matokeo
kwa kutamguliza maslahi ya nchi na taifa kwa ujumla. Tumtangulize Mungu wa Amani ili tubaki Taifa lenye Umoja na Upendo.

Ninawatakia uchaguzi mwema.
 

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,940
2,000
Hakuna kitakachobadilika

Rais Magufuli atashinda kwa kishindo na maisha yataendelea kama kawaida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom