george kessy
Member
- Jun 24, 2017
- 56
- 75
Habari wakuu
Me naamni ya kwamba Moja kati ya mahitaji muhimu sana ya binadamu katika maisha yake ya kila siku ni amani.katika kitabu cha George Kaithori cha Make Peace Your Target ,amani ya kwanza kabisa anayoihitaji mtu siyo ile inayotokana na kutokuwepo kwa vita.Amani ni ile hali ya utulivu wa akili na mtuamo wa moyo wake.hii ni hali ambay anaipata mtu anapokuwa hana usumbufu au mtibuko wa aina yoyote ile akilini na moyoni mwake.
Maurus mwandishi maarufu wa vitabu vya saikolojia wa india ,anatukumbusha kwamba ili mtu binafsi aweze kuishi kwa amani ya akili yake na mtuamo wa moyo wake inampsaa azingatie miiko ya misingi katika maisha.
Kwake iwe mwiko kujigamba,kujisifu ,kamwe asikimbilie kukaa kwenye viti vya mbele katika hadharaa yeyote ile Aidha kamwe asiwatumie watu wengine kwa faida zake binafsi,ni mwiko kuwanyanyasa au kuwadharau watu wengine.kwa ujumla makatazo yote hapo juu yanatuonyesha kuwa adui mkubwa ni ubinafsi. Mtu atakuwa na amani atakapoa acha ubinafsi na kuwajali watu wengine.
Picha ya amani
Hapo zamani za kale palitokea mfalme mmoja ambaye alitaka kuona amani inaonekajae machoni.hivyo aliagiza wasanii wote nchini kwake wamchoree picha inaonyesha amani kisha atatoa zawadi kwa picha atakayoipenda kuliko zote.Agizo lile lilisambaa katika ufalme wake wote,na wasanii wakaingia katika shindano.Baada ya muda mfalme akaletewa mamia ya picha .
Alizichambua kisha akabakiwa na picha mbili.
Moja ilionyesha madhari nzuri iliyotulia ambapo mlima ukiwa umejitokeza nyuma na ziwa lenye maji mazuri yaliotulia na yenye rangi ya bluu ,na mbingu yenye rangi ya samawati ilikuwa imefunikwa kwa mawingu mazuri yenye rangi nyeupe na bluu
Picha ya pili pia ilionyesha mandhari yenye mlima na ziwa ,lakini katika picha hii mbingu isiyopendeza ilikuwa ikigeuka rangi nyeusi,mvua nyingi zilikuwa zikileta kiza katika mandhari ile na mwanga wa radi ulikuwa ukionekana ukiwaka hapa na pale katika ziwa.Ziwa lilikuwa limevurugwa kwa maporomoko ya maji.Nyuma ya ziwa ,mbali kidogo na maporomoko ya maji yale,kulikuwa na kichaka kidogo ambapo ndege alikuwa ametengeneza kiota chake.Ndege alikuwa amekaa pale kimya akifanya kazi yake,alikuwa akilalia mayai katika dhoruba lile.
Katika picha zile mbili ,mfalme alichagua ile picha iliyokuwa ina vurugu nyingi.Alipoulizwa kwanini alipenda ile yenye kuonyesha vurugu alijibu "kwa sababu kuwa katika amani haina maaana kuwa mahali pasipokuwa na kelele,vurugu au kazi ngumu.Amani maaana yake kuwa katikati ya vitu vyote hivyo,lakini bado ukawa umetulia katika moyo wako,hiyo ndiyo maana ya amani.
Asante.