Amani: Maandamano ya CHADEMA, maumivu makali kwa CCM na makuwadi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amani: Maandamano ya CHADEMA, maumivu makali kwa CCM na makuwadi wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Mar 4, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimefuatilia Matamko mbalimbali ya Viongozi wa Serikali na wale vyama vya Upinzani.

  1. Alianza Rais kueleza kwamba CHADEMA kinachochea Vurugu katika Maandamano yake kinachoyafanya nchi nzima

  2. Akaja Wasira kueleza kwamba CHADEMA kinachochea Vurugu katika Maandamano yake kinachoyafanya nchi nzima

  3. Akaja Mrema kueleza kwamba CHADEMA kinachochea Vurugu katika Maandamano yake kinachoyafanya nchi nzima

  4. Akaja Cheyo kueleza kwamba CHADEMA kinachochea Vurugu katika Maandamano yake kinachoyafanya nchi nzima


  Nimejarabu kutafakari ni nini hasa kimewatuma hawa watu kutoa kauli hizo hapo juu

  Je ni Uzalendo na Uchungu wa Kweli walio nao dhidi ya Watanzania Maskini ambao kila siku Serikali inaendelea kuwatia Umasikini kwa maagizo yao yasiyozingatia haki za Kibinadamu?

  Je ni Kweli katika Maandamano yalianza Mwanza ya CHADEMA kuna mtu hata mmoja aliyelalamika kupigwa au hata kuvunjiwa duka lake na Waandamanaji?

  Je baada ya Maandaamno, waandamanaji wamevamia ofisi yeyote ya Serikali ya ya Mtu Binafsi na kufanya Uharibifu?

  Majibu ya Maswali yote hapo juu ni HAPANA

  Sasa kama ni Hapana ni nini kimeisukuma Serikali kuja Hadharani na Kutoa Matamko ya Vitisho dhidi ya CHADEMA?

  Jibu ni Rahisi sana,

  SERIKALI inaumbuka

  1. Sasa Inasali kila Kukicha Waandamanaji wa CHADEMA wafanye Vurugu

  2. Inasali kila kukicha Viongozi wa CHADEMA wawachochee wafuasi wao kufanya Vurugu

  Bahati Mbaya Sala zao hazijibiwi na SHETANI na Siku zinakwenda hakuna Machafuko wala Uvunjifu wa Amani, Wanaona Haya, Wanajisikia Aibu, Wanajisikia wana Hatia ya Vifo vya Waaandamanaji wa Arusha, Wanatamani Vurugu zitokee waseme "si Mnaona hawa jamaa ni watu wa Fujo, Tuliwaambie msiende kwenye Maandamano yenu"

  Je Unafikiri Serikali imekata tamaa juu ya Kutengeneza Fujo katika Maandamano ya CHADEMA? kama unafikiri hivyo unajidanganya sana. Sasa watafanya nini?

  1. Kutoa kauli za kuwa provoke Viongozi na Mashabiki wa CHADEMA ili nao wakijibu wapate mahali pa Kuanzia

  2. Kuweka mitego ya kisheria kama ilivyotokea juzi Malampaka ili kuwakamata Viongozi wa CHADEMA, waamshe Hasira za Wananchi, wawapige Risasi halafu waje na Visingizio vya " Walitaka kuvamia kituo cha Polisi kutoa Viongozi"

  Ushari wangu kwa CHADEMA na Viongozi na Mahabiki wake

  1. Stay Focus on the Issue, Wahimizeni Mashabiki wenu wasilete Fujo na si vibaya mkawatahadharisha juu ya Mitego dhali ya Serikali

  2. Msiwajibu akina Wasira, Mrema, Cheyo acheni Uma uwajibu kama Ulivyomjibu JK kule Bukoba ( Mkulu ameumia sana na Mwitikio wa watu baada ya kaauli yake ya kuwataka wawapuuze)


  Asanteni
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hili neno maandamano yawe kwa amani tu ni kweli wanajaribu kuweka mitego lakini kumbe wananchi wameshajua kwa hilo nawapongeza sana CHADEMA waandamane kwa amani kama wanavyofanya!!
   
 3. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndicho nimejua ni kwa nini chadema walikataa kujumuika na vyama vingine vya upinzani kwani wanamtazamo hasi dhidi ya wananchi wao.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Kwa serikali za kiimla, ukisema JIUZULU wanaona umefanya kosa la uhaini. Hawajui ni haki na wajibu kwa vyama vya upinzani kuitaka serikali ijiuzulu kama serikali ikishindwa kuongoza vizuri.

  Kuwaongoza wananchi katika maandamano ya kuitaka serikali ijiuzulu ni njia ya amani ya kuleta mabadiliko. Ukiingilia hayo maandamano na kuwakamata watu au kuwapiga risasi kama alivyofanya Mwema kule Arusha, unavunja amani, na huenda ukafikishwa ICC kama Taylor baadaye.
   
 5. Sabode

  Sabode Senior Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Serikali iko juu ya kuti kavu na chini kuna moto hii balaaaaaa.
   
 6. W

  We can JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nini maana ya maandamano ya amani? Mimi nilichoona ni hiki, ktk maandamano ya CHADEMA, hata viwete na walemavu wanaandamana bila kuumia. Mfano BK, mama mlemavu (kiwete) na mwanae, wameshiriki maandamano.....
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu ninachotaka kukionesha ni kwamba Serikali na Baadhi ya Watu wanaumia sana wanapoona Wat wanaandamana kwa Amani
   
 8. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  wanaogopa kwani wananchi wanazidi kufumbuka macho na kupata mwamko.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama mko makini, kuna Kiongozi wa walemavu, ambaye pia amepandikizwa, ameongea kwenye Taarifa ya habari ya jana na leo,ITV, anasema kuwa in case kukitokea vurugu nchini, watakaoumia ni wao walemavu, maana hawana uwezo wa kukimbia!..

  Ninachojiuliza , kwanini hawa watu hawaongelei kabisa kipengele cha Ufisadi, ugumu wa maisha, Umeme na sakata la Dowans,...wanachoona wao ni fujo kutokea tu?..
  Mambo haya kweli nakubali ni mageni hapa Tasnzania!, na serikali inatumia mwanya huo kutisha watu kwa kuwatumia puppets wake.
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Na mwaka huu kwa maandamano haya , serikali ikae macho watu wanaanza kufumbuliwa macho na kuona ukweli.
  Ukizingatia maisha yanabana kila kukicha heri ya jana!
  SUKALI BEI JUU
  Petrol bai juu
  Kila kitu kinapanda jinsi wauzaji wanavyo jisikia

  Kwa kweli TZ ya leo!
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii Safari ni Ngumu sana maana hata Katika Msafara wa Mamba na Kenge nao wapo, so Jiandae kusikia Mengi sana cha Msingi ni Maandamano yanakuwa ya Amani tu
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa naangalia Sakata la Vijana wa Big Brother kuvunjiwa Vibanda vyao kinyume na Utaratibu, Lile soko lilifunguliwa na Sumaye sasa najiuliza ina maana Sumaye alifungua Soko lilijengwa Barabarani? Kwa nini ukiukwaji huu wa sheria uwaaumize wananchi peke yao ilihali wale waliohalalisha Ujenzi wa lile soko wanaachwa wakila bata?

  1. Haya ndiyo mambo yatayoleta Vurugu Katika hii nchi na si CHADEMA

  2. Hizi ndizo sababu zianazowafanya Wanachi waichukie Serikali na si kwa sababu ya Maandamano ya CHADEMA

  3. Kukaaa katika Luninga ukiwa umevaa suti kali na Kupulizwa na kiyoyozi huku ukitoa Vitisho hakutawafanya wanachi WAOGOPE Kuichukia Serikali
   
 13. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kuna formula niliisoma jana kwenye gazeti la MwanaHalisi sikumbuki mwandishi wake lakini nikaipenda.
  Formula hiyo inakwenda hivi
  MAANDAMANO - INTELENGESIA = UTULIVU
  Hiyo formula imekuwa proved kwenye maandamano ya Mwanza, Msoma, Shinyanga na Kagera.
  Kwa wale mliojifunza hesabu kidogo, hivyo basi
  MAANDAMANO + UTULIVU = INTELENGESIA
  INTELENGESIA = VURUGU

  Kwahiyo basi mimi ninaona card ya mwisho iliyobaki kwa CCM ni kuzuia maandamano ya amani ya CDM kwa kisingizio cha
  intelengesia ili kuamusha hasira za watu ili vurugu zitokee. Hiyo formula imekuwa proved Arusha (M + U = I, I stands for vurugu)

  Kuwashika viongozi wa CDM it is too late JK hana ubavu huo unless aache kutembeza bakuli kwa wahisani. Hivyo turufu ya JK na CCM
  imelala kwenye intelengesia ya Said Mwema, kupiga marufuku mikutano na maandamano ya CDM ili polisi waanzishe vurugu na kuwapiga raia risasi za moto.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135


  Just wait and you will see
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  ccm wanaendeshwa kwa propaganda za kijinga... badala ya kutake advantage na kuyachukulia masuala yanayoongelewa kwenye mikutano/maandamano ya cdm kama challenge na kuact fast kujinusuru wao wanafikiria njia potofu za kuwafunga macho watz ambao kwa sasa wana macho mwili mzima. tatizo mwenyekiti wa chama nae ndio hivyo naskia anahudhuria mkutano ambao washiriki watatu tu ndio marais wengine ni mabalozi na mawaziri sasa sijui priority zake ziko wapi..

  we are doomed
   
 16. m

  mtimbwafs Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa nasikiliza Idhaa ya Kiswahili ya BBC London na nikashitushwa na neno hili:
  " UTII WA WANANCHI WA KIAFRIKA UNAPIMWA KWA UWOGA NA UAMINIFU WAO KWA VIONGOZI WALIOKO MADARAKANI HATA KAMA MAAMUZI YAO MENGI HAYAWASAIDII WANANCHI. NA WAKIJARIBU TU KUDAI HAKI YAO WANAONEKANA WANACHOCHEA VURUGU HIVYO VYOMBO VYA DORA HUTUMIKA KUWAKANDAMIZA WANANCHI HATA KAMA WANACHOKIDAI NI SAHIHI" mtangazaji akamalizia kuwa ni MADHIRA, MATESO, MACHOZI, JASHO NA DAMU kwa Wananchi ilhali viongozi wa kiafrika wakijineemesha kwa utajiri wa ghafla usioelezeka.

  Kwa nini nimesema maneno hayo hapo juu, kwa kweli sasa namuona Mh. Mrema na Bwana Mapesa kama si Wazalendo tena wa Nchi hii bali wamekuwa ni Vibaraka wa CCM na hawana tena nia ya kuona Mtanzania akiitetea haki yake katika njia zilizo sahihi bali ni kujikomba kwa watawala waliopo ili waendelee kuwakandamiza wananchi na wao wakijiinemesha nafsi zao. Hii ni dhuluma kubwa kwa sisi Watanzania.

  HONGERA sana CDM kwa kujitoa muhanga ili kututetea WATANZANIA tulionyonywa na kudhulumiwa haki yetu kwa kuda Mrefu.

  GO CHADEMA GO WE ARE BEHIND YOU!!!. Ila naomba tu CDM wawe Wapole waendelee kuhubiri AMANI, UMOJA na MSHIKAMANO kwa Watanzania kwa kuwa hizi ndio silaha pekee za kumng'oa KABURU CCM na vibaraka wake!.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!.

  CHADEMAAAA!!!!!!!!!!............PEOPLESSSS..........POWER!!!!!!!!!!!!.
  IDUMU CDM.
   
 17. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Usisahau kuwa MREMA na CHEYO ni mbwa wa boss
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Amin Amin Nawaambieni hawa Jamaa wasiposoma Nyakati ya Nini Uma Unahitaji basi Uma utawahukumu 2015, wawaulize akina Mramba, Lau Masha, Dialo, Marmo ( Huyu jamaa alikuwa ana nyodo na mpaka sasa siamini kilichompata Mbulu), batlda na wengine wengi
   
 19. S

  SUWI JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haya maandamano ya CDM sikujua kama yatawanyima usingizi mafisadi kiasi hiki!!! Hawa mafisadi wa CCM wanataka Watanzania wawe wajinga milele!!! Hivi sasa wanafumbuliwa macho na upinzani wa kweli (CDM) roho zao juu wanapumulia machine.. Mpaka rais wa nchi anajikuta anakosa staha na kuanza kutoa kauli zisizokuwa na msingi hadharani. Eti wananchi wapuuzeni CDM.. KWA NINI WANANCHI WASIKUPUUZE WEWE RAIS UNAETOA HOTUBA ZISIZO NA SULUHU YA MATATIZO YANAYOWAKABILI WATZ kila mwisho wa mwezi??????!!!! Mkilala mnabuni mbinu za kuzuia maandamano.. Sasa mnatumia hata vilema kutimiza matakwa yenu... Shame on you:A S 13:
   
 20. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nijuavyo mimi wanaoanzisha vurugu ni serikali kupitia jesh la polisi. Mbona kote huko ambako jesh halija fyatua mabomu kuko shwari?
   
Loading...