Amani Karume: Nilishangaa wana-CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, Uchaguzi 2015 Zanzibar nilisikitika, niliwauliza hawa wenzetu si Watanzania?

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,693
2,000
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
View attachment 2002278
Sifa kubwa ya Rais Aman Karume aliyokuwa nayo ni ULEVI. Anapiga maji kama Pierre Liquid mpaka Bi Kidude akampachika jina AHMADA na kumtungia wimbo maarufu wa "AHMADA Umelewa".

Nahisi aliyaongea hayo maneno akiwa AMELEWA
 
shabiki

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
925
1,000
Tunaendeleza unafiki wetu wa kiafrika,
Marehemu husifiwa,
Nadhani huyu pia ni mwoga, Asingesema haya yote lile jabali la miraba minne lingekuwa Madarakani
 
Jagina

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
999
500
Ndugu zangu "watanganyika"?!!!

Wewe ni miongoni mwa kundi la watu wenye nafsi za kibaguzi ,kujikweza kusiko uhalisia?!!!

Umeishi tu Zanzibar na kutembelea tu huku bara kuyaona hayo tu ya ubaguzi wa watu weusi?!!

Tembea uone ubaguzi wa wahindi ,wazungu na waarabu........ama hawa neno XENOPHOBIA haliwahusu bali sisi tu watu weusi ?!!!

Pengi "minorities" wanapata shida......ukiona huko Zanzibar watu wanabaguliwa basi ujue ni hizo tabia za ubaguzi za WALIO WENGI....

Mathalani umefanya ubaguzi wa kuwabugua(XENOPHOBIC) Watanganyika kuwa wanafanya BIASHARA MBAYA NA MBOVU.....kwako wewe biashara hizo hazifanywi na walio wengi(Wazanzibari)...🤣🤣

Chief nimeishi Malindi Kenya.....kilomita 120 kaskazini huko kutoka Mombasa.....kule walio wengi wana TABIA ZA KINAFKI SANA.....FULL UNAFIKI wa kuwasema wengine-wachache "wauzaji"....cha ajabu WAZAWA wanauza kisirisiri tena wakiwa na NGUO ZA HESHIMA KABISA......ukiwa mgeni/mtalii unafuatwa na "pimps" na kukuuliza iwapo unahitaji "wari"...ukiwatip chapaa wanakuletea hotelini wakiwa wamevaa mavazi ya heshima na ya "kujificha"....wari wabichiii....wari wazawa kabisa.......

Tembea hata Lamu....kule Langoni na Mkomani.....japo Lamu ni kwa kificho kifichoo mnooo ......

So don't pretend to be too innocent and stop putting blame and cross fingers on our few sisters of mainland particularly from Dar and Tanga region wanaofanya hizo mambo......

Kullul Haqqu lau kanna murra!

Naona unachanganya nazi na makumbi yake ,

kama kutembea kijana wangu mimi nimetembea nchi nyingi na zaidi yako wewe naweza kusema hivyo. Kenya sijawahi kufika wala India lakini Asia nimefika na Europe nimekaa sana tu na kusoma pengine hata hujazaliwa.

Hebu soma tena huu uzi unazungumzia kitu gani ???

Hayo mambo yanayotokea hapo Kenya na hapa kwetu Zanzibar yalianza lini na vipi ??
Hao masheikh wako wa Bakwata hakuna muislamu asiyewajua

Mimi sijakuambia niko innocent , umeanza wewe kuniambia mimi ni mbaguzi na nikakuambia ubaguzi mnao nyinyi watu weusi wa bara la Afrika zaidi kwani tunaona wanayofanyiwa CHADEMA na WAZANZIBARI
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814

Sawa mzee wangu nimekupata ashaikhul muadhama .....

Wazanzibari wanabaguliwa na akina nani?!!

Wazanzibari wanabaguliwa kwenye kipi?!!!

Chadema ni chama cha siasa....unapoongelea kubaguliwa hapa ni lazima uende kiutulivu na utuchambulie...

Na je siasa zetu za AFRIKA zikoje?!!!

Kwani kila watu wana siasa zao....hivi nchi za kifalme na kisultani hususani bara Asia na Arabu zina siasa zinazofanana na za nchi za magharibi ?!!!

Je China ,Urusi ,Korea Kaskazini Kuna siasa zinazofanana na nchi za Magharibi ?!!!

Sawa wanalazimishwa kufuata mdundo wa siasa za magharibi....je tayari wamebadilika,wako mbioni kubadilika ?!! Ni hivi karibuni ?!!

Umeniambia nimechanganya nazi na makumbi sawa ila ni wewe uliyeniambia "nikakojowe na kulala" baada ya kuandika maelezo marefu kushabihisha UTHAMANI wa mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964......
Hi
Hapa nakazia hoja kuwa SERIKALI ZOTE ZILIZOPATIKANA KWA MAPINDUZI zina aina yake ya siasa....zote duniani.....

Nilipoongelea hayo uliniambia nije jumba namba 7 michenzani uje "kunishughulikia"....nikakujibu mimi ni mgeni Zanzibar...wala si mkazi wa hapa Zenji....ukanifananisha na "wauzaji" wanaotoka bara....ndio nikakujibu kuwa "wauzaji" wako kokote kule duniani.....nikakumbusha binadamu mwema HUJIHESHIMU...ukanijibu niwaambie "Watanganyika wenzangu walioko hapa Zenji wajiheshimu" yaani mimi mpita njia niwaambie WATANGANYIKA WAJIHESHI U.....hapa ndipo nilipokuambia kuwa je wewe ni mbaguzi?je una ubaguzi wa XENOPHOBIA?!!!

Hapa hukuchanganya nazi na makumbi kuwashambulia Watanganyika na kuwaweka kapu moja....hunijui ila kwa kuwa nimekuja kutembea Zenji ukaniingiza kuwa nami MUUZAJI....huu si ubaguzi?!!!!!
 
citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
1,157
1,500
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
View attachment 2002278
Hatasielewi ni wa chama gani huyo. Ila historia haiongopi. Ni wale wale wa kuleeeeee
 
Naona umeleta topic zenye kuhitaji nyuzi nyingi,
Maelezo yako yanaonyesha ulinisoma kwa jaziba Na ukaandika kwa jaziba , ni wapi nilisema watu wa bara wanajiuza ?
Mbona unatia maneno kinywani mwangu?
Hivi huelewi ubaguzi wanaofanyiwa CHADEMA Na Wazanzibari ? Hicho ulichokiandika huko mwanzo ni kitu gani Kama Si ubaguzi? Au ndio Mapinduzi ya kipekee duniani ?
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,012
2,000
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumsikitisha ni kuitishwa kwa uchaguzi wa marudio mwaka 2015, wakati wakiwa kwenye kikao cha kujadili yaliyotokea katika uchaguzi huo akisema yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa CCM waliokuwa wakifanya majadiliano na Maalim Seif baada ya uchaguzi ili kujua hatma ya Zanzibar.

Uchaguzi huo ulifutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakati huo Mwenyekiti wake akiwa Jecha Salim Jecha aliyeamua kufuta matokeo yaliyokuwa yakiendelea kutangazwa kisha ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 2016 ambao Maalim Seif aliususia.

"Nilishangaa hata wana CCM wenzangu wanahofia wapinzani kushinda, niliwauliza kwani hawa wenzetu si Watanzania? Hawataki haki na usawa? Niliwaambia Maalim Seif ni mtu muungwana kuliko hata walivyokuwa wakimuona na kumpa majina mabaya"-Karume.
View attachment 2002278
Wanasubili mpaka jambo lipite ndio wanasema,
Kama wamehongoka ki ukweli kweli,
Waseme neno kuhusu shambulio la kigaidi zidi ya Tundu lisu,zile risasi 19 alizopigwa Dodoma,na Kesi ya kubambikiwa ya Mbowe.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Naona umeleta topic zenye kuhitaji nyuzi nyingi,
Maelezo yako yanaonyesha ulinisoma kwa jaziba Na ukaandika kwa jaziba , ni wapi nilisema watu wa bara wanajiuza ?
Mbona unatia maneno kinywani mwangu?
Hivi huelewi ubaguzi wanaofanyiwa CHADEMA Na Wazanzibari ? Hicho ulichokiandika huko mwanzo ni kitu gani Kama Si ubaguzi? Au ndio Mapinduzi ya kipekee duniani ?
Mkuu unayakana maandishi yako ?!! 🤣🤣

Huko juu mbona yako....baada tu ya mimi kuongelea mapinduzi ukaniambia nikalale huko juu Michenzani....nilikueleza nimefikia Michenzani?!! Hapa ndipo lugha yako ikaendelea kuwa ya KEDI juu yangu....ukaendelea....njoo jumba namba 7.....hii inaonesha una "kisununu" moyoni dhidi ya hao unaowaona "wageni"...

Mapinduzi yoyote yana gharama zake kipindi yatokeapo.....baada yake.....kuyalinda.....
 
Soma vizuri niliyokuandikia ,punguza jaziba.
Yaani Mapinduzi ayajue zaidi mtanganyika ambaye hayajamfika? Sawa tupe elimu zaidi mtaalamu wa Mapinduzi
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Soma vizuri niliyokuandikia ,punguza jaziba.
Yaani Mapinduzi ayajue zaidi mtanganyika ambaye hayajamfika? Sawa tupe elimu zaidi mtaalamu wa Mapinduzi
Sawa......

Mapinduzi yamemfika Mzanzibari. ...ni lazima ataielewa historia vyema ya mwaka 1964 zaidi yetu wengi wa huku bara.......

Unataka kuniambia kuwa wazanzibari wote/walio wengi wanasimulia STORI ya mapinduzi INAYOFANANA?!!!!
 
Jagina

JF-Expert Member
Jan 29, 2019
999
500
Sawa......

Mapinduzi yamemfika Mzanzibari. ...ni lazima ataielewa historia vyema ya mwaka 1964 zaidi yetu wengi wa huku bara.......

Unataka kuniambia kuwa wazanzibari wote/walio wengi wanasimulia STORI ya mapinduzi INAYOFANANA?!!!!

Story kitu chengine Na yaliyomfika mtu kitu chengine , Kila mtu atakusimulia Kile kilomkuta
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Story kitu chengine Na yaliyomfika mtu kitu chengine , Kila mtu atakusimulia Kile kilomkuta
Sawa.....

Ndio mapinduzi hayo......

Yameshatokea........

Si bora hayo ya Zanzibar....Yale ya familia ya Al Saud kule Saudia ni makubwa zaidi......

Mapinduzi yakifanywa na kutokea....wakishasimamisha UTAWALA wao....kuupinga huwa ni muhali.....ni muhali kwa kweli....
 
nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,106
2,000
Jamani ,CCM haina uwezo,na Haitakuwa nao...Wakushinda Uchaguzi kwa njia halali ....
 
Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
7,910
2,000
Kuna watu naamini wanakaa Zanzibar lkn Mambo ya Zanzibar hawayajui au labda wanapretend hawayaoni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom