Amani Karume aliijua nguvu ya karma, akatubu, akatafuta suluhu na Maalim Seif na Serikali ya Mseto Z'bar ikaundwa. Komandoo Salmini kulikoni?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,019
Uzi huu ni swali. Tuelimishane kwa tunaojua jibu la swali.

Viongozi wakuu SMZ wanaomaliza muda wao mwaka huu 2020 na wapya waliotangazwa kushinda kwenye uchaguzi uliomalizika visiwani Zanzibar yawapasa warudi nyuma kidogo, watafakari kwa kina na kujifunza kutokana na historia ya chaguzi za Zanzibar huko nyuma ambazo ziliambatana na umwagaji damu.

Kama kuna ukweli katika kinachoripotiwa na mitandao ya jamii, viongozi wa vyama vya upinzani na vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu mauaji ya raia yaliyotokea/yanatokea huko visiwani then viongozi wanaomaliza muda wao na wapya wote yawapasa warejee mauaji yaliyotokea January 2001 baada ya uchaguzi ambao Amani Karume alitangazwa kuwa mshindi dhidi ya Maalim Seif.

Chama kikuu cha upinzani visiwani humo wakati huo (CUF) kiliyapinga matokeo hayo kwa nguvu zote ikiwemo kuitishwa kwa maandamano ya amani ambayo yalishambuliwa na vyombo vya dola na kusababisha maafa makubwa.

Lilikuwa ni doa kubwa jeusi kwa nchi ya Tanzania, na haishangazi kuona Benjamin Mkapa (apumzike anapostahili) akikiri kukereka na tukio hili miaka takribani 20 baada ya kutokea.

Amani Karume alikuwa rais zao la umwagaji damu huo. Komandoo Salmini Amour alikuwa ndiye rais aliyempa kijiti Karume katikati ya umwagaji damu huo. Mkapa alikuwa ndiye amiri jeshi mkuu.

Baada ya miaka kadhaa ya kutafakari haya yote, Amani Karume alikuja kujirudi na kuomba poo na Maalim Seif na kupelekea uundwaji wa serekali ya mseto iliyojumuisha CCM na CUF.

Hadi kufikia leo, Amani Karume ametokea kuwa ni mmoja wa marais wastaafu wa Zanzibar waliojijengea heshima kubwa si kwa Wazanzibari pekee bali kwa jamii yote ya Watanzania.

Hatutamwongelea Mkapa kwani hatunaye tena.

Komandoo Salmini yupo lakini sina uhakika Watanzania wengi wanajua haswa yuko wapi, anafanya nini na ana hali gani maana hata kwenye hadhara zinazojumuisha viongozi wastaafu wa kitaifa haonekani (au ni nadra kumuona).

Je, Komandoo Salmin Amour yu wapi? Nini kimemsibu? Kulikoni Komandoo? Ya January 2001 yanahusu?

Tutafakari.
 
Kuna video nimeiona Twitter... hiki kiburi hiki! Hiki kiburi hiki; acha tu!!

Kwa state aliyokuwa nayo kwenye ile video, kisha pale umweke na mlemavu anaye-move kwa kutambaa (kiwete) kisha uwaambie atakayemaliza wa kwanza kwenye "mbio" za 100 m, basi atazawadiwa Sh.100 Billion!!!

Pesa/zawadi itaenda kwa kiwete!!!
 
Hakuna kitu kizuri duniani kama madaraka na pesa na hakuna kitu kibaya duniani kama pesa na madaraka.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kuna video nimeiona Twitter... hiki kiburi hiki! Hiki kiburi hiki; acha tu!!

Kwa state aliyokuwa nayo kwenye ile video, kisha pale umweke na mlemavu anaye-move kwa kutambaa (kiwete) kisha uwaambie atakayemaliza wa kwanza kwenye "mbio" za 100 m, basi atazawadiwa Sh.100 Billion!!!

Pesa/zawadi itaenda kwa kiwete!!!
Ndiyo maana nikauliza......Komandoo kunani?? Ni karma, ama?
 
Huwa nasema afadhali Salmini bado yupo hai tasbihi haitoki mkononi akiomba toba kwa mola wake. Huenda maradhi alokuwa nayo ni adhabu kutoka kwa mola wak akiwa hapa duniani ila kwa Akhera akawa amesamehewa. Kuna hawa wanaotoka madarakani saiv km balozi, kidogo kidogo anaelekea kupooza na kuna uwezekano mkubwa wa kuja kukata kauli na kusahaulishwa kutubu.
 
Salmini Amur Juma yupo kwao Mkwajuni (kiambo chá Kidombo), huyu mtu na kama wengine wengi , serikali wanakutumia unafanya uovu na wanakusahau, huyu hata ccm wenzake hawendi hata kumualisa, kama kupitiwa labda na mpwa wake JUMA DUNI HAJI wa ACT, tukumbuke kuwa huyu Juma Duni (babu) aliswekwa ndani pamoja na Seif Sharif (Maalim) kwa mda wa miaka kadhaa,
Huyu Salmini atakumbukwa kwa kusimama dhidi ya Mwalimu Nyerere na kumwambia "hamna baba wa taifa au babu wa taifa, kama huutaki Muungano wewe sema nitauvunja" Nyerere na ubabe wake hakuijibu kitu.
La 2001 hakuhusika (ninavyohisi mimi, kwani tayari alikuwa Karume keshakabidhiwa na kuapishwa rasmi )Kipindi chake cha mwanzo kilijaa unyang'aji ila alijirudi na kutaka wakae pamoja na CUF kipindi kile. Na huyu Karume hakuwa akitokea sana kwenye mambo ya ccm / smz ya Shein sijui kama alipigwa pande au kajipiga pande mwenyewe, kuna video moja hataki hata kusalimiana na Balozi , inavyosemekana haziwivi Hawa watu.
 
Huwa nasema afadhali Salmini bado yupo hai tasbihi haitoki mkononi akiomba toba kwa mola wake. Huenda maradhi alokuwa nayo ni adhabu kutoka kwa mola wak akiwa hapa duniani ila kwa Akhera akawa amesamehewa. Kuna hawa wanaotoka madarakani saiv km balozi, kidogo kidogo anaelekea kupooza na kuna uwezekano mkubwa wa kuja kukata kauli na kusahaulishwa kutubu.
Salmini alipoacha tu madaraka alifikwa na majanga. Kwanza mkewe alimkimbia, pili alipoteza uwezo wake wa kuona.

Kiufupi Salmin a.k.a Komando wa udongo alifanya mambo mengi yasiyopendeza kama vile kuvunjia watu majumba, kuwatoa makazini wote wenye mrengo wa upinzani, kuwabambikizia wafuasi wa CUF kesi ya uhaini, alivoombwa awatoe akasema waache wakae ndani si mapapai hayo. Pia kulikua na vitendo vya kutia vinyesi kwenye visima n.k

Haya yote kwa ujumla ni makosa dhidi ya binaadamu ambayo Mungu mwenyewe amejivua mamlaka ya kusamehe mpaka binaadamu wenyewe wakusamehe.
 
Kuna video nimeiona Twitter... hiki kiburi hiki! Hiki kiburi hiki; acha tu!!

Kwa state aliyokuwa nayo kwenye ile video, kisha pale umweke na mlemavu anaye-move kwa kutambaa (kiwete) kisha uwaambie atakayemaliza wa kwanza kwenye "mbio" za 100 m, basi atazawadiwa Sh.100 Billion!!!

Pesa/zawadi itaenda kwa kiwete!!!
Tuwekee hapa hiyo video Mkuu
 
Muasisi wa Serikali ya Mseto Znz ni Jakaya Mrisho Kikwete

Serikali ya Karume ilikuwa inapinga wazo hilo na hata kwa kejeli Waziri wake maarufu Ali Juma Shamhuna akawa anakebehi anasema anajua Mseto wa Chakula sio wa Serikali

Jakaya akaitisha kikao cha NEC kikafanyika Butiama 2009 akaingiza na kuipitisha kibabe hoja ya Serikali ya Mseto Znz kina Karume wakatoka vichwa chini na kwa kuwakomesha mahafidhina akampitisha Mpemba kwa mara ya kwanza
 
Masikin Shamhuna. Apumzike alipostahili.
 
Salmini alipoacha tu madaraka alifikwa na majanga. Kwanza mkewe alimkimbia, pili alipoteza uwezo wake wa kuona.

Kiufupi Salmin a.k.a Komando wa udongo alifanya mambo mengi yasiyopendeza kama vile kuvunjia watu majumba, kuwatoa makazini wote wenye mrengo wa upinzani, kuwabambikizia wafuasi wa CUF kesi ya uhaini, alivoombwa awatoe akasema waache wakae ndani si mapapai hayo. Pia kulikua na vitendo vya kutia vinyesi kwenye visima n.k

Haya yote kwa ujumla ni makosa dhidi ya binaadamu ambayo Mungu mwenyewe amejivua mamlaka ya kusamehe mpaka binaadamu wenyewe wakusamehe.
Kuna mmoja anajiita jiwe aka chuma, laiti kama angesoma hapa kiburi na majivuno yake huenda angepunguza.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom