Amani imetoweka kwenye ndoa yangu kisa kukosa mtoto

kamla

Senior Member
May 16, 2017
169
106
Naomben ushauri wenu wa mawazo wapendwa maan nipo katk kipindi kigumu sana. Nimeolewa takiban huu hi mwaka wa tatu sasa natimiza kwenye ndoa niliolewa 2015

Mwaka ule ule niliofunga ndoa nilifanikiwa kubeba ujauzito pasi na mim mwenyewe kujua kama ni mjamzito sema kun dalili nilikuwa nasikia nikimwambia mume wangu anasema huenda ikawa Malaria basi na mimi sikukitilia mkazo sana

Siku hiyo niko na shughuli zangu za nyumbani nikaona nimepata period ya ghafla na Tumbo likiuma sana yaan mpk nikashawishika kumwambia mume wangu ile hali yangu nayojisikia
Ikabidi tuende hospital baada ya kufika hospital dokta akanifanyia utra sound ndipo aliponipa majibu haya kuwa nimepata miscarriage akanipa dawa za kutumia akanambia sina tatizo.
Nikamuuliza naweza pata mimba nyengine akanambia inawezekana ten bila tatizo ila hakikisha unameza dawa
Basi tiba nikaimaliza yote kama dokta alivyonielekeza lakini pinde ikaja hapa kila nikijaribu kutafuta mtoto kwa mara nyengine inashindikan sijawahi fanikiwa mpaka hii leo navyoandika hap sina amani ndugu wa mume wangu wameanza kunitolea maneno mabaya jamani nateseka sana mwenye uwezo wa kunisaidia jamni na afanye hivyo

Naombeni jamani mwenye kuweza kunisaidia ktk hili nitashukuru san nivumilieni kwa huu uandishi mbaya nahitaji msaada mnoo sitak kejeli wala matusi jamani nachohitaji ni msaada wapendwa maana maji yameshanifika shingoni
 
Pole hiyo ni changamoto ya maisha pia..Ikishindikana Hospitalini ujaribu pia na wataalamu wa mitishamba wanaweza kukusaidia tatizo lako la kutokupata mtoto...Vumilia ipo siku itakubali tu....Mtegemee Mungu yeye hajawahi kushindwa na chochote
 
Mkuu umeshaenda kupima kujua tatizo ni nini? maana kuna matatizo ya kutokupata mtoto yanayotibika na yasiyotibika...yasiyotibika mara nyingi yanakuwa ni ya kuzaliwa nayo, ila kwa kuwa wewe ushapata ujauzito ukatoka naona matumaini yapo, ni Hospitali tu kujua tatizo
 
Basi tiba nikaimaliza yote kama dokta alivyonielekeza lakini pinde ikaja hapa kila nikijaribu kutafuta mtoto kwa mara nyengine inashindikan sijawahi fanikiwa mpaka hii leo navyoandika hap sina amani ndugu wa mume wangu wameanza kunitolea maneno mabaya jamani nateseka sana mwenye uwezo wa kunisaidia jamni na afanye hivyo

Rudi kwa daktari bingwa.
 
Pole sana, imani inahitajika. Hali Kama yako ilimkumba mama yangu pia, mimi nilipatikana miaka 17 baada ya ndoa yao.

Mama alinisimulia baada ya kuoa na kunitaka niwe na subira kama aliyokuwa nayo baba R. I. P.

Kama mumeo anakuelewa haina tabu achana na mawifi na mama mkwe.
 
Pole Sana kwa tatizo, hayo maneno potezea binadamu hatuna shukran utafanikiwa kupata mtoto bado maneno yataendelea tu. Ushauri wangu nendeni wote mkacheki vipimo lakin usitoke nje kufanya sex.
Nimekuekewa mkuu
 
Nenda kwa specialist wa kina mama masuala ya uzazi atakupa antibiotics

Ukishindwa kuna dawa za miti shamba ni nzuri sana zitakusaidia ambazo zimemsaidia dadaangu sana baada ya kukaa miaka saba bila mimba alipotumia tu akapata mimba na kwa sasa ana watoto wawili anafurahia sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom