VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Natoa onyo tu la kichama. Kama kada kindakindaki wa CCM tangu miaka ya themanini. Najionea mchezo wa hatari wa kutaka kumchokoza Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume. Karume sasa amekuwa 'target' ya wana-CCM wasioitakia mema CCM huko Zanzibar. Karume hadi amezomewa na vijana waliondaliwa kwa ajili hiyo.
Nasema huku nikihema kuwa Karume ni mboni ya CCM na utulivu wa Zanzibar. Ni Karume ndiye aliyeifikisha Zanzibar kwenye muafaka wa kisiasa unaotumika hadi sasa. Ni Karume ndiye aliyewafanya CCM na CUF wawe wamoja Zanzibar kuiongoza nchi yao kwa pamoja. Ndiye aliyemaliza mgogoro mbaya wa kisiasa Zanzibar.
Karume si mtu muoga. Husema anachokiamini. Anaposimama kusema, kwa sauti yake ya kukwaruza, husema anayoyaamini na kufikisha ujumbe anaokusudia. Karume aliwahi kuwalipua baadhi ya wana-CCM, kwenye kikao Dodoma, kuwa wana akili za samaki. Karume ni mtu jasiri. Kumchokoza ni kutaka mapambano yasiyo na mfano.
Kwa Wazanzibari, Karume, pamoja na mapungufu yake ya hapa na pale, bado anasikilizwa. Kichama, Karume bado ni mtu muhimu kwa siasa za Zanzibar. Ni mboni ya CCM kule Zanzibar. Kumghafilisha Karume ni hatari kuliko kumchokoza chatu. Umuhimu utageuka kuwa udhalimu.
Anayewatuma wafuasi wake wamchokoze Karume, ajiulize tena na kujirudi. Aache mara moja. Ni amri kwa ajili ya uhai na ustawi wa CCM na amani ya Zanzibar!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Last edited: