Amaliza mwaka kwa kifungo cha miaka 459 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amaliza mwaka kwa kifungo cha miaka 459

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jan 1, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::12/31/2008
  Amaliza mwaka kwa kifungo cha miaka 459
  Julius Sazia, Shinyanga

  MKAZI mmoja wa Shinyanga, Saimon Kulyama amemaliza mwaka 2008 kwa staili yake baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 459 kwa kubainika kufanya makosa mbalimbali yakiwamo ya kughushi hati za kusafiria na kuiba Sh5.5 milioni.


  Hakimu Issa Magori alitoa hukumu hiyo kwa mhasibu huyo msaidizi wa zamani wa Jeshi la Polisi, ili iwe fundisho kwa watu wengine wote wanaofikiria kufanya makosa kama hayo.


  Hakimu magori alitoa hukumu hiyo juzi baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka.


  Awali mwendesha mashitaka katika kesi hiyo, Samuel Kilabuko, ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi, alisema mshitakiwa alikuwa anakabiliwa na mashitaka mawili ya kughushi hati za kusafiria za serikali (warrant) na kuiba jumla ya Sh5,552,000.


  Alisema mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 1992 hadi 1999 wakati wizi huo ulipogunduliwa na ndipo alipokamatwa na kufikishwa mahakamani.


  Hakimu huyo, baada ya kuridhika na ushahidi, alitoa adhabu hiyo ya miaka mitatu jela kwa kila kosa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya makosa kama hayo.


  Akijitetea kabla ya hukumu hiyo, Kulyama alidai apunguziwe adhabu kwa sababu ana familia inayomtegemea na wazazi na kwamba tayari ameshapoteza kazi, lakini utetezi wake ulitupiliwa mbali na hakimu huyo.


  ''Kila kosa linajitegemea na hivyo utatumikia kifungo cha jumla ya miaka 459,'' alisema hakimu Magori na kumwacha mshitakiwa asijue la kufanya.


  Katika tukio jingine, mahakama hiyo imewahukumu watu wawili, Richard Mhoja, 29, mkazi wa Mshikamano na Bundala Mahona, 28, mkazi wa Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga, kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kosa la kuvunja na kuiba duka vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 607,000 kwenye duka moja.


  Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Elieza Luvanda.


  Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi, Shukrani kuwa Julai 9, 2008, majira ya saa 9:00 usiku katika eneo hilo la Mshikamano, washitakiwa hao na wenzao wawili, wakiwa wamejipanga vyema kutekeleza azma yao hiyo, walivamia duka la Hamidu Kisoya na kuiba mali mbalimbali zenye thamani ya Sh607,000.


  Alisema wakiwa katika harakati za kusafirisha mali hizo, walizingirwa na wananchi wenye hasira kali na wenzao wawili kupigwa vibaya hadi kufa na baadaye kuchomwa moto, wakati washitakiwa hao wawili waliokolewa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.


  Awali kabla ya hukumu hiyo, washitakiwa hao waliiomba mahakama hiyo iwapunguzie adhabu kwa vile ni kosa lao la kwanza na kwamba wana familia zinazowategemea, lakini hawakuweza kumshawishi Hakimu Luvanda.


  Katika tukio jingine, jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio moja la kuuawa mtu mmoja kwa tuhuma za kuiba gunia mbili za mpunga, katika kijiji cha Ihalo kata ya Kwesela wilaya ya Shinyanga.


  Kaimu kamanda wa polisi, Kilongo tukio hilo lilitokea Desemba 30, 2008 na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Mwandu Mayala, 40, mkazi wa kijiji cha Ihalo ambaye anadaiwa kuiba mpunga huo mali ya Zakaria Shija.


  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu Hakimu ana hasira sana.Kwa nini asiletwe Kisutu Mramba na kundi wakabidhiwe kwake ?Kama makosa haya tu miaka hiyo je makosa ya akina Mramba inakuwaje ?
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huyu hakimu ana lake jambo. Hii hukumu ni bora angesema kamuhumu maisha tu ikajulikana. Au anafukuzia dili la kuwa hakimu wa kesi za EPA. Maana kuteuliwa kuwa hakimu wa hizi kesi ni big deal kwa mahakimu wetu, nafikiri kila mmoja wao anazitolea macho kwa sasa.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu hakimu nadhani katoa onyo kama alivyo dai na ku set kesi yake iwe ref kwa watu wa aina ya huyo mfungwa wake , yaani alarm kwa Mramba , n a kundi lake
   
 5. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  saa nyingine inabidi kutumia common sense hata kama sheria inasema hivyo.Sasa kumfunga mtu miaka 459 manake nini?Utadhani tuko kipindi cha kina Nuhu walipokuwa wakiishi mpaka miaka 900 huko.
  Sasa life expectancy ya mbongo ni miaka (47?) halafu unamfunga mtu miaka 459?Hofstede umesema kweli.Angemfunga maisha tu ingeeleweka.
   
 6. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Aaaaargh, hiri rijamaa rimekoseaga. Ringetuma ujumbe turiwekeege dhamanaaaa.
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mwandishi wa hii habari hajaiweka vizuri. Ukisoma unakuta jamaa anakabiliwa na mashitaka mawili, kwa mujibu wa muendesha mashitaka. Na kila shitaka hakimu katoa miaka mitatu jela, sasa si ingekuwa miaka 6. Lakini kama ni hivyo alikuwa na mashitaka mengi mpaka ipatikane miaka 459, ambayo ni mashitaka 153 na si wawili kama alivyoandika mwandishi. Lakini iwavyo na iwe huyu asije fungwa miaka yote, na mijizi mikubwa kama ya EPA ije yote ishinde kesi!!!!.
   
Loading...