Ama kweli wawekezaji watatutia vigole machoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ama kweli wawekezaji watatutia vigole machoni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Jan 20, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Korti yaamuru Mzungu kucharazwa viboko kumi Send to a friend Wednesday, 19 January 2011 21:52 0diggsdigg

  Phinias Bashaya, Bukoba
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukoba, imemhukumu Robert Maintland (42), raia wa Ugiriki kutumikia kifungo cha miaka miwili jela na kucharazwa viboko kumi, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini kinyume cha sheria.
  Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Peter Matete.

  Hukumu hiyo inaweza kuwa faraja kwa wananchi wapatao 100 wa kitongoji cha Bujenjeke, Kijiji cha Ruhija, Kata ya Ijumbi mkoani Kagera ambao walikuwa wakivutana na Mgiriki huyo ambaye alikuwa akituhumiwa kuwanyanyasa akishirikiana na polisi.

  Polisi mkoani Kagera walikuwa wakilalamikiwa kwamba wanamkingia kifua raia huyo wa kigeni ambaye manyanyaso yake dhidi ya raia yaliwafanya baadhi yao kukimbia nyumba zao na kulala vichakani.

  Wakazi wa Bujenjeke waliwahi kuwaambia waandishi wa habari kuwa walikuwa wakilala na kushinda porini, kukwepa kupigwa na askari polisi na mgambo ambao walikuwa wakivaa mavazi ya kufunika nyuso zao maarufu kama mavazi ya kininja.

  Lakini juzi, Mahakama ya Bukoba iliridhika na ushahidi uliotolewa dhidi ya mtuhumiwa, hivyo hakimu Matete alimtia hatiani kwa kosa la kuwepo nchini bila kibali na kumhukumu kwenda jela miaka miwili na viboko kumi au kulipa faini ya Sh80,000.

  Hata hivyo, Maintland alilipa faini ambayo haikumuondolea adhabu ya kuchapwa viboko ambayo ilikuwa itekelezwe jana.
  Mapema hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Idara ya Uhamiaji, Gerald Mardai ilidai kuwa, raia huyo alikamatwa Februari 23, mwaka jana, akiwa Kituo cha Polisi Bukoba bila kibali halali cha kuingia nchini.

  Pia ilidaiwa kuwa, Maintland alikuwa na hati tatu za kusafiria zikiwa na majina tofauti, ambazo alizitumia kuingia nchini isivyo halali.

  Katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani, hati za Uingereza na Afrika Kusini zilikuwa na jina la Robert John Rubeinstein, huku vielelezo vingine vya Ugiriki vikionyesha kwamba alikuwa akitumia majina ya John Robert Penesis na Robert John Maintland.

  Maintland amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na wanakijiji wa Ruhija wilayani Muleba, mwaka jana aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwachapa viboko wananchi waliodaiwa kuingia katika ardhi yake.

  Baadhi ya familia kijijini hapo na Bujenjeke waliondolewa kwa kuvunjiwa nyumba zao kwa madai ya kuvamia eneo la “Buguma Estate” ambalo mzungu huyo alidaiwa kumiliki kihalali kwa shughuli za uwekezaji.

  Miongoni mwa wakazi wa Kijiji cha Bujenjeke waliomlalamikia mzungu huyo, ni Leonida Pancras (54), aliyemtuhumu kufukua kaburi la marehemu mume wake na kubomoa nyumba akimshinikiza kuhama eneo hilo.

  Pia, miongoni mwa waliomtuhumu mzungu huyo kwa kuwacharaza viboko ni Geniva Romward (30), aliyedai Novemba 2, 2008 alichapwa kwa ushirikiano wa mgambo na polisi wa Muleba.

  Mmoja wa walinzi wa mzungu huyo, Joas Kyatuka, anadaiwa kushiriki matukio ya kubomoa nyumba na kufukuza wananchi waliojenga karibu na eneo hilo, Romward ni miongoni mwa wananchi wengi waliofunguliwa mashtaka ya kuvamia eneo la mwekezaji huyo.

  Akizungumza mwaka jana kujibu malalamiko ya wananchi hao, Maintland alisisitiza kuwa eneo hilo analimiliki kisheria na kudai kuwa, mgogoro huo ulikuwa unakuzwa na wanasiasa wilayani Muleba.

  Kwa mujibu wa wananchi hao, Maintland alifika kijijini hapo mwaka 2003 na kuanza kuweka uzio katika eneo mojawapo la kijiji hicho bila kuishirikisha jamii husika, lakini baadaye aliondoka kurudi kwao.

  Mwaka 2008 Maintland alirejea tena nchini na hapo ndipo mgogoro ulipoanza kwani aliwaamuru wananchi hao kuondoka katika eneo hilo, huku akijigamba kwamba alikuwa tayari kuwalipa fidia kati ya Sh100,000 na Sh350,000, malipo ambayo hata hivyo wananchi hao waliyakataa.

  Source: Korti yaamuru Mzungu kucharazwa viboko kumi

  My take:

  Bila kulishughulikia tatizo la ufisadi kwa uadilifu nchi hii ama itaingia kwenye migogoro ama itakuwa koloni la walowezi muda siyo mrefu.. Mbarali wananchi wanalia kunyang'anywa ardhi yao, haya ya Kagera nayo ni aibu tupu.

  Yaani mgeni anaingia kama mwekezaji kumbe ni tapeli tupo, na baada ya muda anaanza kututia viboko na vidole machoni kama ambavyo wawekezaji wa Dowans wanavyoiyumbisha nchi
   
 2. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Inauma ukizingatia yapo matokeo mengi yahivyo..........
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  una uhakika kuwa ni machoni tu?
   
Loading...